A-Z Kardinali Rugamba alivyovikwa Pallia Takatifu/Akiri imani na kula kiapo mbele ya Balozi wa Papa.

  Рет қаралды 3,480

Radio Maria Tanzania

Radio Maria Tanzania

4 күн бұрын

IFAHAMU PALLIUM TAKATIFU
▪ Pallium ni neno la Kiswahili lililotoholewa kwa Lugha ya Kingereza Pallium au kwa Kilatini Palla, likimaanisha vazi linalovaliwa juu ya (Chasuble - vazi la Kiliturujia) na Papa, Maaskofu Wakuu na baadhi ya Maaskofu katika Kanisa Katoliki la kiroma.
Mwanzoni lilitumiwa na Papa wa Roma tu, lakini baadaye alianza kuwatunuku Maaskofu Wakuu kuonyesha Mamlaka waliyonayo juu ya Maaskofu kwa kushirikishwa na Upapa wa Roma.
Pallium hutokana na sufu (manyoya ya kondoo) yaliyokatwa kutoka kwa kondoo wakati wa sherehe ya Mt. Anyesi ambayo huadhimishwa Januari 21 kila mwaka. Jina Anyesi (au Agnes) limetokana na neno la Kilatin “Agnus” lenye maana ya “Mwanakondoo”. Kwa nini hutengenezwa kutokana na sufu ya kondoo? Kwenye Agano Jipya Kristo anatambulishwa kama “Mwanakondoo wa Mungu” (rejea Yn. 1:29, 36). Kama ambavyo kondoo wanatoa sufu kwa ajili ya kutengeneza Pallium.
▪ Pallium huenda ilianza kuvaliwa na Wagiriki wa zamani waliovaa nguo ambazo Warumi waliziita Pallium kama nguo iliyovaliwa nje yenye umbo la kimstatili kuzunguka mwili wa mtu ikiwa imetupwa mabegani kama mtandio wa kuzuia baridi.
Ila kadiri ya miaka ilivyoenda Pallium ikawa nyembamba ikifanana na skafu/mtandio mrefu. Baadaye Karne ya Saba (7) Pallium ilibadilika na kuwa na umbo la herufi Y (Ikionekana hivyo mbele na nyuma) ikiwa na misalaba meusi sita, nne kuzunguka shingo, moja mbele na moja nyuma.
▪ Matumizi ya Pallium kikanisa yalianza enzi za tamaduni za zamani za Wafalme na baadhi ya maafisa waliovaa skafu maalumu kama vitambulisho vya ofisi bug.
Pallium ilivaliwa na Maaskofu kwenye karne ya 4 na 5 na karne ya 6 Papa akawa anawatunukia (conferring) wao kama alama ya heshima au sifa. Kuanzia karne ya 9 ikawa kwamba Askofu Mkuu asingeweza kuonyesha mamlaka ndani ya Jimbo Kuu bila kutunukiwa Pallium na Papa. Aina hii ya vazi huvaliwa shingoni wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu katika Jimbo Kuu na majimbo ya Kanda yake, ila Papa huvaa duniani kote kuonyesha hadhi yake kama Mchungaji Mkuu wa kundi lote la Kristo kadiri ya imani ya Kanisa Katoliki.
.

Пікірлер: 7
@MatildaRafael
@MatildaRafael 3 күн бұрын
Tunamubee sana adumu katika kulipigania kanisa katika kweli
@paulrwechungura4284
@paulrwechungura4284 2 күн бұрын
Mungu milele amina
@MsalabaniReko
@MsalabaniReko 3 күн бұрын
Amina baba
@MatildaRafael
@MatildaRafael 3 күн бұрын
Tunamubee sana adumu katika kulipigania kanisa katika kweli 5:14
@radiomariatanzania
@radiomariatanzania 2 күн бұрын
Amina
@kevinkatima4975
@kevinkatima4975 3 күн бұрын
Mungu amsaidie adumu katika njia njema pamoja na watawa wengine wote Amina🔥
@radiomariatanzania
@radiomariatanzania 2 күн бұрын
Amina
MAKAMU WA RAIS TEC AFAFANUA KWA KINA MAANA YA PALLIUM ATAKAYOVALISHWA KARDINALI RUGAMBWA
14:14
孩子多的烦恼?#火影忍者 #家庭 #佐助
00:31
火影忍者一家
Рет қаралды 43 МЛН
Мы никогда не были так напуганы!
00:15
Аришнев
Рет қаралды 5 МЛН
FAHAMU KUHUSU UGONJWA WA GANZI, DALILI NA MATIBABU YAKE.
18:36
MUHIMBILI MLOGANZILA TV
Рет қаралды 76 М.
MAOMBI YA ASUBUHI by Innocent Morris
16:53
Holy Spirit Connect
Рет қаралды 691 М.
Sunday Mass Quiapo Church Live Mass Today July 07, 2024
56:40
Team Tajmal Naizi
Рет қаралды 8 М.
Tabia 10 Muhimu za Mafanikio
30:39
Success Path Network
Рет қаралды 376 М.
БОЛЬШОЙ ПЕТУШОК #shorts
0:21
Паша Осадчий
Рет қаралды 8 МЛН
1❤️
0:17
Nonomen ノノメン
Рет қаралды 13 МЛН
ЕНЕШКА 2 СЕЗОН | 2-бөлім | ТОКАЛ АЛЫП БЕРЕМІН
23:12
Не трогайте эту ВОЛОСАТУЮ ШТУКУ! 😱
0:24
Взрывная История
Рет қаралды 2,6 МЛН
Хитрая МАТЬ делит НАСЛЕДСТВО между ДЕТЬМИ 😱 #shorts
1:00
Лаборатория Разрушителя
Рет қаралды 1,1 МЛН