Рет қаралды 18,161
Chanda chema imebaki kuwa neno hakuna tendo moyo umekosa lengo vimetoweka shangwe vifijo na nderemo oooouoooh.
Kuna watu Roho wanayo ya chatu,kweli wapo watu na viatu huhuhu
Mtu bila utu si mtu huyo
Siambiliki sisemeki mtima wangu umedungwa mkuki
Moyo wangu ndakindaki mwenza wa ndani hawaminiki
Tamu ikawa shubiri wangu Rafiki kuwa adui
Natunza lako Siri kwangu wageuka mui Rafiki mnafiki huyo.
########
Binadamu tuishi kufaana,kupendana kutakiana mema.
########
Umdhanie Rafiki kwako chukizo
Mnafiki ndiye mchawi chetezo
Tamalaki ufikiri kikulacho ki nguoni mwako we
Hivi ukawa Petero kwake mwokozi
Ama Daudi rafikiye uraya?
Au Judasi wakubusu mwaaaah!!!!
Ama Saulo ama Yakobo?
We ni Nani?
We ni nani?
Nikulinganishe na Penina wa Hannah?