Рет қаралды 11,705
HISTORIA FUPI YA PAROKIA YA MT. ANTHONY WA PADUA
MBAGALA- ZAKHEM
Parokia ya Mbagala iliyoanzishwa mwaka 1954 ikiwa ni mojawapo kati ya Parokia kongwe katika Jimbo Kuu la Dar Es Salaam. Kipindi hicho Jimbo kuu la Dar lilikuwa pamoja na Vicariet ya Jimbo la Mahenge likiongozwa na Hayati Askofu Edgar Marantha.
Parokia ya Mbagala ilianzishwa katika eneo ambalo sasa ni kituo cha kiroho (Mbagala spiritual Centre) eneo la Parokia lilikuwa kubwa ambalo ni kusini mashariki ya Jimbo kuu la Dar Es Salaam kuanzia Mbagala hadi Kilwa Kipatimu; kwa sasa ni eneo la Parokia za Kizuiani, Kijichi, Kizinga, Mbagala Kuu, Mbande, Kongowe, Toangoma, Vikindu, Mkuranga, KisijuPwani, Kibiti na baadhi za Parokia za Jimbo la Lindi.
Parokia hii tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikihudumiwa na mapadre na watawa wa Shirika la Wafransiskani Wakapuchini. Mwaka 1984 Parokia ya Mt. Anthony wa Padua ilihamishiwa eneo la Mbagala Zakhem kufuatia kupatikana kwa eneo hilo na mahitaji ya kuanzishwa kwa kituo cha kiroho na baadaye nyumba ya watawa wadada wadogo.
Parokia yetu imejaliwa kuwa na mashirika ya watawa wanawake matano ambayo ni Masista Wafransisko Utawala wa Bwana, Masista wa Holy Union, Masista wa Mkombozi, Masista Wakamaldolesi na Masista Wabenediktini wa Chipole. Mashirika haya yamekuwa chachu ya uinjilishaji na pia msaada mkubwa katika huduma za kijamii katika Parokia yetu.
Tangu mwaka 1954 hadi 2018 Parokia ya Mbagala imepitia hatua mbali mbali za kukua kimwonekano, kiimani na kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuzaliwa kwa Dekania za Kigamboni na Kilimahewa zenye zaidi ya Parokia 17.
Parokia imesimamia uanzishwaji wa parokia mpya kadhaa ambazo zilihitaji miundo mbinu mipya ili kupata sifa za kuteuliwa kuwa parokia, michango ya waumini, ufadhili na msaada kutoka kwa Jimboni ilifanikisha miradi kukamilika kwa wakati na kupata nafasi ya kuanza mingine mipya.
Mapadre wanaohudumia parokia ya Mbagala Zakhem kwa sasa ni:-
1. Raphael Henry Chiligwalwa (paroko) 0754 563 639
2. Nolascus Charles Mwandambo 0756630684/0655 630 684
3. Prosper Anthony Kessy 0755 444 471
Tunashukuru Mungu kwa zawadi ya mapadre wa shirika la Ndugu wadogo wa Wafransiscani Wakapuchini kwa huduma zao kwenye Parokia yetu, ambao wanatupa huduma zote kwa kadri ya mahitaji na maelekezo ya Kanisa Katoliki.
IDADI YA WAAMINI
Parokia ya Mbagala Zakhem in jumla ya waamini 12,250 kutokana na sensa ya mwaka 2018 wanaotoka katika kanda 42 na jumuia 118 ambazo zinaunda vigango vitatu vya Chamazi, Vigoa na MajiMatitu. Ndani yake kuna kituo cha sala kimoja; Vigozi kilichopo eneo la Mponda, Parokiani.
i. Waamini wanaozunguka eneo la Parokia wako katika kanda 24 na jumuia 63 zenye jumla ya waamini 5,719. ii. Waamini wanaozunguka kigango cha Maji matitu wako katika kanda 5 zenye jumla ya Jumuia 12 na waamini 1,265
iii. Waamini wanaozunguka kigango cha Chamazi wako katika kanda 13 zenye jumla ya Jumuia 43 na waamini 5266.
Parokia yetu naweza kusema haijaishiwa na shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi katika vigango vyetu na vituo vya sala. Waamini wamekuwa msingi wa miradi yote hiyo tunawashukuru sana.
Mawasiliano:
JUGO MEDIA,
Sokoine Drive, Posta
P. O. BOX 34014,
Dar es Salaam.
For Bookings and other Enquiries
Phone Number +255757560764/657790405
#jugomedia #kanisakatoliki #familiatakatifu #wawata #uwaka #viwawa