Рет қаралды 12,501
MWENYEKITI CHADEMA MBEYA ATEMA CHECHE AKITANGAZA UONGOZI WA MUDA "NI KIBURI, WANATAFUTA NJIA YA KUONDOKA"
Mwenyekiti wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Mbeya Joseph Mwasote amesema hata sita kufanya maamuzi dhidi ya viongozi wanaofanya mchezo ndani ya chama wenye lengo la kugawa wanachama.
Mwasote ameeleza hayo katika mkutano na viongozi wa chama Cha CHADEMA kutoka katika Kata zote za Jimbo la Mbeya Mjini uliokua na lengo la kutangaza kamati tendaji mpya itakayo fanyakazi Kwa muda baada ya kuvuliwa uongozi Kwa kamati tendaji iliyopita chini ya aliyekua mwenyekiti John Mwambigija.
Amesema kitendo kinachofanywa na aliyekua mwenyekiti wa chama hicho John Mwambigija kupinga maamuzi ya chama ngazi ya Kanda ni kufanya fujo za makusudi kitu alicho kiita ni kiburi na kutafuta njia ya kutaka kuondoka ndani ya chama.
Cc @enocksaimon
#WasadiDigital