MBIU YA PASAKA | Easter Exultet

  Рет қаралды 19,300

Lucid tv

Lucid tv

2 жыл бұрын

Mbiu ya Pasaka
Sasa jeshi la malaika wa Mbinguni wafurahi. Yafurahi mambo ya Mbinguni, na mbiu ya wokovu ipigwe kutangaza ushindi wa mfalme mkuu. Nayo nchi iliyoangazwa na nuru kubwa sana ifurahi na kwa kuwa imemulikwa na mwanga wa mfalme wa milele, itambue ya kuwa imeondolewa na giza la ulimwengu.
Naye Mama Kanisa aliyepambwa vizuri kwa taa nyingi zenye kuwaka afurahi na sauti za watu zivume katika ukumbi huu.
Bwana awe nanyi
Awe rohoni mwako
Inueni mioyo
Tumeiinua kwa Bwana
Tumshukuru Bwana Mungu wetu
Ni vyema na haki
Ni vyema na haki tuziimbe sifa za Mungu Baba Mwenyeziasiyeonekana, na za Mwanaye wa pekee, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa moyo wote na akili zetu zote na kwa sauti zetu, Yeye alitulipia deni la Adamu kwa Baba wa milele, na kwa damu yake takatifu akafuta mashtaka ya ile dhambi ya kale.
Hakika hii ndio sikukuu ya Pasaka, anapochinjwa yule mwana kondoo halisi ambaye kwa damu yake milango ya waamini inabarikiwa.
Huu ndio usiku ulipowatoa Misri mara ya kwanza baba zetu, wana wa Israeli, ukawavusha pakavu katika Bahari ya Shamu.
Huu basi ndio usiku uliondoa giza la dhambi kwa nuru ya ile nguzo ya moto.
Huu ndio usiku ambapo leo popote duniani wenye kumsadiki kristu wanatengwa na maovu ya dunia na giza la dhambi, wanarudishiwa neema na kushirikishwa utakatifu.
Huu ndiyo usiku, ambapo Kristu alikata minyororo ya mauti, akatoka kuzimu ameshinda, kwa maana kuzaliwa hakungalitifaa kitu, tusingali kombolewa.
Lo, jinsi gani wema wako ni waajabu kwetu sisi!
Lo, wema gani wa upendo usiopimika wa kumtoa Mwanao upate kumkomboa mtumwa!
Lo, dhambi ya Adamu hakikaililazimika ikafutwa kwa kifu cha Kristu!
Lo, kosa lenye bahati, lililostahili kumpata Mkombozi mkuu kama Huyo!
Kwahiyo utakatifu wa usiku huu, wafukuza dhambi, wafuta makosa, huwarudishia usafi walioanguka na furaha wenye huzuni.
Basi ee Baba mwema, kwa ajili ya neema ya usiku huu upokee sadaka ya jioni ya kukusifu. Kanisa takatifu linakupa sadaka hii kwa mikono ya watumishi wake, linakutolea mshumaa huu wa nta ya nyuki.
Lo, usiku uliobarikiwa kweli, yalipounganishwa ya Mbingu na ya nchi, ya Mungu na ya mwanadamu.
Basi, ee Bwana, tunakusihi, mshumaa huu uliobarikiwa kwa heshima ya jina Lako, uendelee kuwaaka na kuondoa giza la usiku huu.
Tena uupokee kama harufu nzuri, uchanganyike na nuru za Mbinguni.
Nyota ya asubuhi iukute unawaka yaani nyota ile isiyotua kamwe, ndiye Kristu Mwanao, aliyetoka kuzimu, akawaangaza wanadamu kwa utukufu, naye anaishi na kutawala daima na milele.
W. Amina

Пікірлер: 11
@muthenyamagda8921
@muthenyamagda8921 4 ай бұрын
So solemn, I could follow the words so clearly. Praise you Jesus
@lucidtv95
@lucidtv95 4 ай бұрын
Amen🙏🏾🙏🏾
@Kannyjeannette
@Kannyjeannette Жыл бұрын
Très bien chanté
@kelvinbonface3399
@kelvinbonface3399 2 жыл бұрын
Such a nice paschal song
@julienaganze8216
@julienaganze8216 Жыл бұрын
Bonne fête de Pâques.
@catherinemakena9016
@catherinemakena9016 2 жыл бұрын
Amen. Blessed
@lucidtv95
@lucidtv95 2 жыл бұрын
Amen🙏
@emilykatabi378
@emilykatabi378 2 жыл бұрын
Good
@lucidtv95
@lucidtv95 2 жыл бұрын
🙏🙏
@anodearsulusi7536
@anodearsulusi7536 2 жыл бұрын
🙏🙏🙏🙏
@lucidtv95
@lucidtv95 2 жыл бұрын
🙏
Praeconium Paschale - Exsultet
10:14
PapalMusic
Рет қаралды 762 М.
Sigma Kid Hair #funny #sigma #comedy
00:33
CRAZY GREAPA
Рет қаралды 41 МЛН
Useful gadget for styling hair 🤩💖 #gadgets #hairstyle
00:20
FLIP FLOP Hacks
Рет қаралды 11 МЛН
ЧУТЬ НЕ УТОНУЛ #shorts
00:27
Паша Осадчий
Рет қаралды 10 МЛН
Llegó al techo 😱
00:37
Juan De Dios Pantoja
Рет қаралды 60 МЛН
SEKWENSIA  (PASAKA)
7:59
ANGELS SINGERS
Рет қаралды 19 М.
Dominika ya Tatu ya Kwaresma | Mahubiri
9:29
Lucid tv
Рет қаралды 591
Ni Salama Rohoni Mwangu - Tenzi za rohoni lyrics
5:24
Lyrics Captain
Рет қаралды 1,6 МЛН
ASKOFU NIWEMUGIZI APIGA MBIU YA PASAKA
19:26
Radio Mbiu
Рет қаралды 12 М.
MBIU YA PASAKA KWA KADRI YA MISALE MIPYA YA KIROMA, 2023...
14:50
INJILI YA FURAHA
Рет қаралды 3,5 М.
MBIU YA PASAKA
11:59
Imani Kuu
Рет қаралды 1,4 М.
Erkesh Khasen -  Bir qyz bar M|V
2:43
Еркеш Хасен
Рет қаралды 1,3 МЛН
Umar Keyn - Ever 2024
3:10
Umar Keyn Music
Рет қаралды 304 М.
KeshYou x Snoop Dogg - Forever Sunday (Official Music Video)
3:06
BM PRODUCTION
Рет қаралды 239 М.
Jaloliddin Ahmadaliyev - Erta indin (Official Music Video)
4:32
NevoMusic
Рет қаралды 2,8 МЛН