Mgambo ashushiwa kipigo na machinga kisa matikiti, akimbilia kanisani

  Рет қаралды 5,927

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

19 күн бұрын

Askari wa Jeshi la Akiba maarufu kama 'mgambo' ambaye jina lake halikutambulika amekimbilia kanisani kunusuru maisha yake baada ya kushushiwa kipigo na wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga.
Tukio hilo limetokea leo Jumatano Julai 10,2024, eneo la Soko la Buhongwa jijini Mwanza, wakati kikosi kazi hicho cha mgambo kilipokuwa kikikamata matunda ya machinga wanaofanya biashara katika eneo hilo.
Mwananchi imefika eneo la tukio saa 3:20 na kukuta umati wa machinga wakiwa wamezingira uzio wa Kanisa Katoliki Kigango cha Buhongwa wakishinikiza mgambo huyo atolewe nje ili waendelee kumshushia kipigo kwa kile wanachodai ni kuchoshwa na tabia ya mgambo hao kuwanyang’anya na kuharibu bidhaa zao.
Akisimulia mkasa uliomkumba mgambo huyo, machinga katika eneo hilo, Abdallah Mohammed amesema kikosi kazi hicho kimewasili Buhongwa saa 3:00 asubuhi ya leo na kuanza kuchukua matikiti na mananasi ya mfanyabiashara eneo hilo ndipo kikazingirwa na machinga na kuanza kushushiwa kipigo.
Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Пікірлер: 46
@msafirlaizer2368
@msafirlaizer2368 17 күн бұрын
Kichaa akianza kuoga, Ujue karibia anapona 🙌
@leokamil6284
@leokamil6284 17 күн бұрын
🎉
@PrinceHendry-hp8vv
@PrinceHendry-hp8vv 17 күн бұрын
Safii anzeni kuacha uboya km wakenya
@phankaphares7134
@phankaphares7134 17 күн бұрын
Lazima serikali iwasikilize wananchi kwa kile wanachokihitaji hili kuleta amani ya nchi yetu
@ANRAHIMKADUMA
@ANRAHIMKADUMA 17 күн бұрын
Safi Sana piga kweli kweli kama Kenya
@kessydieselengineers3205
@kessydieselengineers3205 17 күн бұрын
Mliambiwa muhamie Burundi kwa hiyo msilalamike sana ila inauma sana kupitia ccm hata rais anajua
@wemaMichael-fr4th
@wemaMichael-fr4th 17 күн бұрын
wangemuua ningefurahi sana wanamwaga sana chakula hawa
@tinnahagustinolyelu4247
@tinnahagustinolyelu4247 17 күн бұрын
Vipi kama Ni mtoto wako tema mate chini na shetani huyo akutoke
@aishaabrahaman9957
@aishaabrahaman9957 17 күн бұрын
​@@tinnahagustinolyelu4247wamezidi
@OmariNgurangwa
@OmariNgurangwa 17 күн бұрын
Mama anaupiga mwingi uyooooo
@emanweljohn1240
@emanweljohn1240 17 күн бұрын
Hiyo ndio serikali ya ccm mama haoni viongozi wa sisi çcm wao marafiki waoni matajiri ccm hoyeeee
@kennycathles
@kennycathles 17 күн бұрын
Jeshi la Mgambo livunjwe!!!
@marcynhumbi3534
@marcynhumbi3534 16 күн бұрын
Machinga nyie mmenifurahisha sana,hakuna watu wanakera kama mgambo,mara wanapiga watu hadi wanakufa yaan mmetufurahisha,Limekimbilia kanisani kuomba huruma ya Mungu Aaaaah
@user-je2cr9su8q
@user-je2cr9su8q 17 күн бұрын
Amekimbilia kwa YESU amefanya vizuri bila hivyo angekufa na nadhani alikua ustaadhi amechukua hatua nzuri ya kuokoka .Bwana YESU asifiwe
@user-qi6ql1lp9k
@user-qi6ql1lp9k 17 күн бұрын
Nyie wagambo mbona mnanyasa watu
@user-cv4jb1bm6i
@user-cv4jb1bm6i 17 күн бұрын
Mtu mnyonge akichoka mateso huwaga mtu mbaya sanaaaaa!yaaan maskini kwa maskini tunarudishana nyuma mtu anatafuta buku mgambo anaenda kuchukua buku kwa mtafuta buku
@ilynpayne7491
@ilynpayne7491 16 күн бұрын
Ukiona hivyo ujue nchi hii watu wana anza ku choka mama ana semwa kila pahala
@KarumeKindamba-lk1px
@KarumeKindamba-lk1px 17 күн бұрын
Mimi sishangazwi na kazi za mgambo ni mambo ambayo yanafanyika ktk miji na pembezoni mwajiji.
@leokamil6284
@leokamil6284 17 күн бұрын
Waonevu sana
@DiwaniMwafongo
@DiwaniMwafongo 17 күн бұрын
Mbegu ya Kenya inasambaa.... Yafanyikea Kenya , na kwingineko .... Enough is enough...piga vita kuonewa!!
@LameckZakaria-qg9vv
@LameckZakaria-qg9vv 17 күн бұрын
Safi sana tumechoka bora tucheze nao
@SimulizinaPerfect
@SimulizinaPerfect 17 күн бұрын
Mimi mgambo namsubir nilivyo vurugwa iv natoka na shingo ya mgambo
@petercostakisoka
@petercostakisoka 17 күн бұрын
Uyo mtendaji anatamani kucheka
@kaaakwakutuliaa5179
@kaaakwakutuliaa5179 17 күн бұрын
hayo ni malengo ya raisi kwasababu ni wafanya kazi wake
@pancrasmalamla9799
@pancrasmalamla9799 17 күн бұрын
Hili ni Moja Kati ya Matukio yanayoumiza wamachinga ipo siku watu watachoka kama unachukua biashara zao je wakafanye wapi kazi zao waishije mambo na Baadhi ya Askali kiukweli ni chukizo Kwa watu uhasama hautaisha
@hawahussein137
@hawahussein137 16 күн бұрын
Wagambo wananyanyasa sana watu
@MurekateteNjeni
@MurekateteNjeni 17 күн бұрын
Daah na amepewa asee...wambieni na uyo kaka wa tikiti wamrudishe wameondoka nae asbh
@MichaelBruno-zy8ff
@MichaelBruno-zy8ff 17 күн бұрын
Iz centa zimekuzwa na hao hao wafanyabiashara wadogo Leo zimekuwa na kuendelea mnawafukuza ayo ni mambo ya upuuz tu
@MadilishaSimon-sb9kk
@MadilishaSimon-sb9kk 17 күн бұрын
Mwanza home mmewakilisha
@user-zu8ou2oe4c
@user-zu8ou2oe4c 16 күн бұрын
Eti ni vurugu ya kawaida niya kawaidae kichaa akianza kuoga kaanza kupona sasa ww afande sema ni vurugu ya kawaida siku moja mtaelewa tu subirin majiran zetu walifanya ujingaaa sa iv wanakoma watu wamekuwa sugu hawaogop mabom wanajesh wala nn sasa haya
@sylvestercameo6263
@sylvestercameo6263 17 күн бұрын
Eti "tunaiomba serikali itusaidie...." Kwani hao mgambo wametumwa na nani? Au kwenu serikali ni nini?
@leokamil6284
@leokamil6284 17 күн бұрын
Si umemsikia wametumwa na Serekali ya CCM wawatoe ila wanawafuataka kuwalaghai uchaguzi ukifika
@user-zu8ou2oe4c
@user-zu8ou2oe4c 16 күн бұрын
Shid ya nchi yetu viongoz wetu wanaona wao ni mabosi wetu na jeshi la polis badala yakulinda raia na mali zake wanalinda raia na kulinda wanasiasa alafu wakipanga jambo wanafanya ni lazma kama tozo za cm miamala na nk
@kaaakwakutuliaa5179
@kaaakwakutuliaa5179 17 күн бұрын
saivi ni dozi hakuna kuonewa kenya wametupa mfano mzuri sana
@kessydieselengineers3205
@kessydieselengineers3205 17 күн бұрын
Waende wapi? Acheni manyanyaso
@MenaldMbilinyi
@MenaldMbilinyi 17 күн бұрын
Mbele kwa mbele
@filbertagrey4078
@filbertagrey4078 17 күн бұрын
😂😂😂 nani anaona kama mimi, askari kabanwa kidole na mlango wa gar.
@mugishamajeba9628
@mugishamajeba9628 17 күн бұрын
😂😂😂😂😂
@Niika870
@Niika870 17 күн бұрын
Jezi ya Yanga 😂😂😂
@FurahaChano
@FurahaChano 17 күн бұрын
Safi sana tumechoka jamani watu wa buhongw
@majebelemathis9991
@majebelemathis9991 17 күн бұрын
Huyu ndiye mama samia hajuwi shida za wananchi kwa sababu yeye analindwa JPM alisema mtanikumbuka kipindi cha JPM mgambo hawakuonekana mjini yako wapi mapenzi ya mama?
@aishamwalimu4816
@aishamwalimu4816 16 күн бұрын
Uwaga mzazi wakike ndoanaekua na uruma kumbe wapi
@alexsuleiman3795
@alexsuleiman3795 17 күн бұрын
saf sana akome
@kaaakwakutuliaa5179
@kaaakwakutuliaa5179 17 күн бұрын
kumanina na bado mnapigia kura ccm
@AmosPaul-k4m
@AmosPaul-k4m 16 күн бұрын
Machinga buhongwa wanateseka sana kwakwel sio hili tu mengi tunaona yakiendelea lkn serikali hatuoni wakilifanyia utatuzi inauma sana 😭
@juliuskitaluka1206
@juliuskitaluka1206 16 күн бұрын
Usiku umeendelea Sana asubuhi imekaribia sana
Hoja kuhusu jina yaibuka shauri kuhusu Kombo, Wakili Madeleka afunguka
7:24
Spot The Fake Animal For $10,000
00:40
MrBeast
Рет қаралды 159 МЛН
Mama vs Son vs Daddy 😭🤣
00:13
DADDYSON SHOW
Рет қаралды 32 МЛН
MAZITO YAIBUKA SAKATA LA KARIAKOO, MACHINGA AONGEA KWA HASIRA
8:47
At the Point of Collapse
14:19
Herman Manyora
Рет қаралды 20 М.