Рет қаралды 15,804
Kuna mistari ukisoma unajua Mungu alikua katika hali gani, ya furaha, hasira ama huzuni.
Ingekuwa ni kwenye Agano Jipya angesema "Kanisa langu, linaangamia kwa kukosa maarifa"
Maarifa ni taarifa sahihi juu ya jambo fulani.
- Mungu anapozungumzia kuhani anazungumzia kila mtu aliyeokoka 1 Petro 2:9, kila mtu ambaye ameokoka katika ulimwengu wa roho anaonekana kama kuhani. Kwahiyo kama wewe ni kuhani na hauna maarifa, Mungu atakukataa kwa sababu maarifa ndiyo yanakusaidia kufanya kazi yake kwa usahihi na kwa ubora.
MAARIFA ndiyo haya mafundisho unayosikiliza, ni neno la Mungu unalosoma.
Mungu anataka makuhani wake wawe na maarifa kwa sababu adui yetu anafanya kazi kwa HILA. Waefeso 6:10-11.#PastorSunbella#Nguvu#Hila