UFUGAJI WA NYUKI;zijue mashine za kuvuna na kuchakata asali

  Рет қаралды 4,894

Shamba Darasa TV

Shamba Darasa TV

3 жыл бұрын

Ufugaji Nyuki kwa Njia ya Kisasa kutoka chuo cha nyuki Tabora
jinsi ya kulina asali
jinsi ya kutambua asali ya nyuki
mavazi ya nyuki
asali ya nyuki
Ufugaji wa nyuki unaweza kuwa chanzo kizuri cha kipato cha ziada kwa wakulima wadogo wadogo. Uzalishaji wa asali nchini Tanzania umekuwa ukitegemea sana wafugaji wadogo wadogo, wanaotumia njia za kiasili kama vile mizinga ya magogo au vyungu, kwa nyuki wa kiafrika ambao ni wengi sana kwenye mapori.
Mkulima ambae anahitaji kufuga nyuki ni lazima awe na uelewa wa mzunguko wa maisha ya nyuki. Anaye anza ni lazima aulize wafugaji wenzake ambao wana uzoefu wa kutosha, au kujiunga katika kikundi cha ufugaji ili apate ufahamu zaidi juu ya ufugaji wa nyuki.
Tafuta sehemu salama kwa ajili ya mzinga
Ni vizuri kutafuta mahali pazuri, salama, na penye sifa ya kufugia nyuki. Vifaa vyote vikishapatikana jambo linalofuata ni kuchagua mahali gani pa kuweka mzinga. Ni vizuri sehemu hii ikawa mahali ambapo makundi ya nyuki hukusanyika mara kwa mara.
Ni wapi pa kuweka mzinga!
Mara nyingine kupata eneo sahihi ni tatizo. Ni vizuri kuzingatia yafuatayo:
• Kulingana na hali ya kujilinda ya nyuki wa Afrika, haishauriwi kuweka mzinga shambani au karibu na shamba (weka umbali wa mita 150-200 kutoka kwenye mazao au nyumbani)
• Mzinga ni lazima uwekwe sehemu ambayo haitasababisha upotevu wa nyuki wanaporudi kutoka nje ya mzinga (wasiingie kwenye kundi lisilokuwa lao)
• Mizinga isiwekwe mbalimbali sana ili kuepusha usumbufu wa kutembea mbali kwa mfugaji wakati anapokagua. Eneo la kuweka mizinga ni lazima liwe :
• Kimya na mbali ya jumuia (hospitali, shule, na viwanja vya michezo) na maeneo ya biashara au viwanda.
• Karibu na maji masafi-kandokando ya mto, mabwawa ya samaki, mabeseni ya maji au sehemu ya matone.
• Iwe karibu na chakula cha nyukimimea inayochanua, miparachichi, nazi, euculptus, migunga n.k
• Iwe sehemu ambayo ni kavu na isiwe sehemu ya tindiga kwani unyevu unyevu husababisha ugonjwa wa ukungu (fungal disease) na pia huzuia utengenezaji mzuri wa asali.
• Iwe mbali na watu waharibifu na iliyojificha kuepuka waharibifu.
• Sehemu ya mizinga ni lazima iwe inafikika kirahisi kwa kipindi chote cha mwaka ili iwe rahisi kuhamisha nyuki pale inapohitajika.
• Kuwe na kivuli cha kutosha hasa wakati wa mchana jua linapokuwa kali, na kusiwe na upepo mkali.
• Iwe mbali na mashamba, ambapo dawa za kuulia wadudu zinatumika.
Vichaka au wigo unaotenganisha mizinga na kuzuia wavamizi ni muhimu ili kupunguza ukali wa nyuki.
Jinsi ya kuweka mzinga
Baada ya sehemu ya kuweka mizinga kupatikana, kinachofuata ni kuandaa mizinga kwa ajili ya kuweka panapotakiwa.
• Safisha mzinga kuondoa uchafu wote, utando wa buibui na aina nyingine za wadudu.
• Weka chambo kwenye mzinga (waf ugaji wa nyuki mara nyingi hutumia nta) kwa kuipaka katika kuta za mzinga kwa ndani.
• Mzi nga unaweza kutundikwa kwenye mti, kwenye nguzo, kuweka kwenye jukwaa au kwenye miamba. Hii inategemea mkulima mwenyewe anapendelea njia ipi.
Aina za mizinga ya nyuki
Kifuniko juu (Top bar)
Hii ni aina ya mizinga inayotumika sana. Gharama yake ni karibi shilingi elfu hamsini za kitanzania. Ni aina nzuri sana kwa mtu anaeanza ufugaji wa nyuki kwa kuwa ni wa gharama nafuu. Hata hivyo mfugaji wa nyuki anaweza kutengeneza mzinga mwenyewe kama ana utaalamu wa useremala.
Faida
• Ni rahisi kukagua asali iliyo tayari.
• Ni rahisi kuvuna asali kuliko kuvuna toka kwenye mzinga wa kienyeji.
• Ni rahisi kuwatunza nyuki wakati wa kiangazi na inapokuwa hakuna maua. Mfugaji anaweza kuwapatia nyuki chakula ili kuongeza uzalishaji wa asali.
• Kurina asali ni rahisi sana ukilinganisha na mizinga ya magogo inayotundikwa juu ya mti, kwa kuwa haihitaji vifaa maalumu.
• Aina hii ya mizinga huwekwa kwa kuninginia jambo ambalo siyo rahisi kushambuliwa na wadudu/wanyama wanaokula asali. Inajaa haraka sana wakati ambao ni msimu wa asali kutengenezwa kwa wingi.
Hasara
• Kichane kwenye mzinga wa boksi hakina kishikizo hivyo huvunjika kwa urahisi sana kama hakitashikwa kwa uangalifu.
• Masega huvunwa pamoja na asali, jambo linalolazimu nyuki kutengeneza tena masega mengine na husababisha kupungua kwa uzalishaji wa asali.
Mzinga wa Langstroth unaweza kukupatia asali zaidi
chuo cha nyuki arusha
#mkulimasmart
#shambadarasa

Пікірлер: 19
@israeldonatus3397
@israeldonatus3397 Жыл бұрын
Bei za Vida zipoje
@danielmoses2244
@danielmoses2244 3 жыл бұрын
Wonderful wonderful wonderful .... very nice demonstration ... hakika wafaa kabisa kuwa mkufunzi .... you exactly know what you're doing .... so competent & courageous too HONGERA SANA
@shambadarasaTV
@shambadarasaTV 3 жыл бұрын
karibu
@ISSACKNHELEGANI
@ISSACKNHELEGANI 4 ай бұрын
Mashine bei gani
@prosperremmy1737
@prosperremmy1737 2 жыл бұрын
Habari za leo, Hongereni sana kwa hatua hii. Mimi niko kilimanjaro naomba nijulishwe namna yakupa mtalamu kwani nimeanzosha shamba lakini sina utalamu wa nyuki. Naomba msaada.
@shambadarasaTV
@shambadarasaTV 2 жыл бұрын
whatsapp us 0713178868
@MKULIMASMART
@MKULIMASMART 3 жыл бұрын
Good
@honoratussalvatort8700
@honoratussalvatort8700 3 жыл бұрын
GOOD
@noelmwigomelo9202
@noelmwigomelo9202 Жыл бұрын
Nahitaj mavaz na vifaa vya kulinia asal nipo mbeya
@amosicronery7730
@amosicronery7730 Жыл бұрын
ulipata?
@user-mm8ym1id5d
@user-mm8ym1id5d 9 ай бұрын
Zinaunzwajenazinapatikanawapi
@stanlehsanga3151
@stanlehsanga3151 Жыл бұрын
Mashine sh ngap,? taf
@bokeyemarwa5038
@bokeyemarwa5038 3 жыл бұрын
God demonstration, Kudos🙏. The machine for pressing honey while still in combs ,is available at your place? and how much you are selling it. Cheers.
@shambadarasaTV
@shambadarasaTV 3 жыл бұрын
karibu
@shambadarasaTV
@shambadarasaTV 3 жыл бұрын
KARIBU
@fridamugarula9325
@fridamugarula9325 3 жыл бұрын
Hii mashine ya kuchuja asali inapatikana kwa bei gani?
@amosicronery7730
@amosicronery7730 Жыл бұрын
Itakuwa zaidi ya million 4 (nakisia)
@yustusmngengale9396
@yustusmngengale9396 2 жыл бұрын
Nawezaje kupata mashine hizi ?'
@amosicronery7730
@amosicronery7730 Жыл бұрын
SIDO Tabora na manual kutoka Njombe
НЫСАНА КОНЦЕРТ 2024
2:26:34
Нысана театры
Рет қаралды 682 М.
ЧУТЬ НЕ УТОНУЛ #shorts
00:27
Паша Осадчий
Рет қаралды 9 МЛН
Who has won ?? 😀 #shortvideo #lizzyisaeva
00:24
Lizzy Isaeva
Рет қаралды 65 МЛН
Recycling Trash Aluminum in Afghan Factory || Manufacturing process
18:53
Smart Farming
3:26
KickStart International
Рет қаралды 15 М.
Bubut Kayu...Akar Sampah Tapi Mewah
8:06
Gitasel DIY
Рет қаралды 647
AUTOMATIC NIPPLE DRINKING SYSTEM/Economy keji
2:45
Shamba Darasa TV
Рет қаралды 63
KWANINI ECONOMY CHICKEN KEJI NI BIASHARA?
2:39
Shamba Darasa TV
Рет қаралды 238
Hay Day of Struggles
15:52
Sonne Farms
Рет қаралды 16 М.
НЫСАНА КОНЦЕРТ 2024
2:26:34
Нысана театры
Рет қаралды 682 М.