Рет қаралды 3,748
Wakaazi wa eneo la Tezo Mbuyuni kaunti ya Kilifi sasa wanaitaka serikali kuelezea bayana walioidhinisha kungo’lewa kwa miti ya mibuyu na kusafirishwa hadi nchini marekani. Wenyeji wamedai kushangaza na hatua hiyo na kusema mbuyu ni mojawapo ya tamaduni na historia ya jamii ya Mijikenda. Na kama anavyoarifu Francis Mtalaki, wakaazi waripotiwa kulipwa shilingi laki moja kwa mbuyu uliokuwa hapo kwa zaidi ya miaka 200.