Рет қаралды 88,973
Watu 45 wamethibitishwa kufariki huku makumi wengine wakijeruhiwa kufuatia mafuriko katika eneo la Mai Mahiu kaunti ya Nakuru. Hii ni baada ya mto eneo hilo kuvunja kingo na kusababisha kusombwa kwa kijiji kizima cha Kamuchiri. Juhudi za uokoaji na uopoaji zinaendelea kwa sasa eneo hilo.