AMBWENE MWASONGWE - ALIKUTA IBADA (OFFICIAL MUSIC VIDEO)

  Рет қаралды 1,266,986

Ambwene Mwasongwe

Ambwene Mwasongwe

2 жыл бұрын

Ambwene Mwasongwe presents the music video for "Alikuta Ibada"
Wimbo huu ni maalumu Kwa ajili ya kulikumbusha kanisa la Bwana kuwa tumefikia Hali ileile ya Mafarisayo na Masadukayo ya unafiki.....
Nakukumbusha tunapaswa kumwabudu Bwana kwa roho na kweli.....
Tuondoe na kuyaacha mambo mengi ya mwili tuliyoyaingiza kanisani, turudi kwanza msalabani Kisha tuendelee na safari....
Mungu akubariki utayeuona huu wimbo na nisaidie kuwatumia link na wengine ili ujumbe umfikie kila MKRISTO
Watch All Music Videos by Ambwene Mwasongwe: • Ambwene Mwasongwe All ...
Follow Ambwene Mwasongwe
Instagram: / ambwenemwasongwe_
Subscribe to Ambwene Mwasongwe: / @ambweneobadiamwasongwe
Digital Branding & Marketing By:
Black Ozen Entertainment Limited: / blackozenentertainment...
Alikuta Ibada - Ambwene Mwasongwe (Lyrics)
Alikuta ibada zinaendelea
Ila zina tatizo
Alikuta maombi yanafanyika
Ila yana kasoro
Alikuta mifungo inaendelea
Ila ina dosari
Akakuta sadaka zinatolewa
Ila zina makandokando mengi
Akashangaa mwili umetawala
Badala ya Roho!
Akawafundisha ibada za Rohoni
Jinsi zitakiwavyo
Muombapo msiombe sala ndefu
Ili watu wawasifu
Mtoapo msitoe kwa matangazo
Ili watu wawaone
Mfungapo msijionyeshe
Ili watu wawasifu
Ila baba yenu aliye sirini
Yeye atawajazi
Mungu ni roho
Na wote wamwabuduo
Imewapasa kumwabudu
Kwa roho na kweli
Yeye huona kile ambacho jicho haliwezi kuona
Yeye hushika kile ambacho mkono hauwezi kukishika
Yeye hutafsiri lugha ya moyo hata mdomo usiposema
(Kwake hakuna siri)
Akawakemea Viongozi wa dini
Na washika sheria
Waandishi na mafarisayo
Na masadukayo
Hawakutaka-Walikasirika
Wakaleta vitabu
Kwa mamlaka ya nani wafanya haya?
Wapate kumshitaki
Wakadhani kiroho ni shule
Ili wamfedheheshe
Akawatazama akawapima
Walikuwa weupe
Wakamletea mwanamke mzinzi
Aliyefumaniwa
Wakataka wasikie neno lake
Atakavyomuhukumu
Akainama akachora chini
Akaandika majina yao
Ardhi ikageuka "video touch"
Wote wakakimbia
Mzee wa kanisa alipojiona
Akilewa na wake za watu
Shemasi kaona aibavyo sadaka
Naye akakimbia
Wanakwaya wakaona wanavyosengenyana
Na kupiga majungu
Yesu alipoinuka
Wote wamekimbia
Akasema na mimi sikuhukumu
Nenda usitende dhambi tena!
Ole mafarisayo na masadukayo
Mwaosha vikombe kwa nje
Ila ndani ni vichafu
Mwapaka makaburi chokaa
Ndani yake ni mifupa
Mwawabebesha watu mizigo
Ninui hambebi
Ole!
Mwawatungia wengine sheria ninyi hamzifuati!
Ey!
Akalikaribia kapu la sadaka
Aone wanachotoa
Ghafla akamwona mwanamke mjane
Anatoa kichache
Akasema huyu ametoa vingi
Kuliko ninyi nyote
Maana kwa Mungu wingi sio idadi
Ni ukamilifu wa jambo
Wengi mmetoa kwa mbwembwe
Vimeonekana vingi
Ila mlivyobakisha nyumbani ni vingi
Sio kama mwanamke huyu
Akaona wanagawana chenji ibadani
Akakasirika
Wanauza vitu kama mnada hekaluni
Mahali pa ibada
Akachukua fimbo akawachapa
Akapinduapindua
Nyumba yangu itakuwa ya sala
Sio nyumba ya biashara
Uko wapi moyo wa ibada?
Uko wapi moyo wa kicho!?
Ule moyo wa kutetemeka
Tusikiapo neno la Bwana
Mambo haya Je yamo kanisani leo basi tujiulize
Akija yule mwenye kanisa
Je hatatuchapa?
Mungu ni Roho
Na wote wamwabuduo
Imewapasa kumwabudu kwa roho na kweli
Maana yeye huona kile ambacho jicho
Haliwezi kuona
Yeye hushika kile ambacho mkono
Hauwezi kukishika
Yeye hutafsiri lugha ya moyo hata mdomo usiposema
Tunatakiwa tumwabudu Bwana
Tusichonge sanamu
Tuangalie tusije kujiabudu wenyewe
Pamoja na vitu vyetu
Tukicheza ili watu watuone
Tumejiabudu wenyewe
Tukiimba ili watu watufurahie
Tumetwaa utukufu
Tukigeuka nyuma na kutafuta maoni ya watu
Tumejichuuza wenyewe
Hicho ndicho kilichomponza lusifa
Alitaka asifiwe
ooh!
#AmbweneMwasongwe #AlikutaIbada

Пікірлер: 1 600
@nakilingwembele9504
@nakilingwembele9504 8 ай бұрын
Jaman tunapoandka jina Mungu tusianzie na herufi ndogo,anza na herufi kubwa maana ndo Mungu aliyehai,ukiandika kwa herufu ndogo c Mungu aliyehai
@user-cr4eu4zc6u
@user-cr4eu4zc6u 2 ай бұрын
Mungu nijalie kuyafany mapenzi Yako wewe uonae moyoni mwangu😭😭😭😭
@SupajrChagaa
@SupajrChagaa 2 ай бұрын
Huu wimbo kila nikikaa niangalie TV lazima nianze na huu wimbo najiona kama nahubiriwa na mtume Paulo,ambwene Mungu wa mbinguni azid kukutumia uendelee kuomba kirohoo
@JanethMgeni-cr4wl
@JanethMgeni-cr4wl Ай бұрын
Ubarikiwe mtumishi wa munngu kwa ujumbe wa mungu kwa mataifa naamini wengi tumefunguliwa ubarikiwe sana
@user-fv9tu2pe8s
@user-fv9tu2pe8s 3 ай бұрын
Endelea kutumikia KUSUDI LA MUNGU kwa kicho. BWANA YESU anaona utumishi wako
@pasteurelizabethruzoviyo3978
@pasteurelizabethruzoviyo3978 Жыл бұрын
mungu akubaliki ambwene mwasongwe mimi wakati nime anza kusikia nyimbozako nili amuwa kuokoka kwa sasa niko bishop wakanisa inchi burundi🇧🇮
@israelmbedule3897
@israelmbedule3897 Жыл бұрын
Barikiwa sana
@ziadaambanjaula8900
@ziadaambanjaula8900 Жыл бұрын
Du umeokoka aya ubalikiwe
@elizabethleonard1809
@elizabethleonard1809 Жыл бұрын
Glory be to God 🙏
@cizajean-marie7223
@cizajean-marie7223 Жыл бұрын
Wahisemwo neza ncuti y'umusaraba
@wafabian8116
@wafabian8116 Жыл бұрын
God is great hallelujah
@japhetmichael7608
@japhetmichael7608 Жыл бұрын
Kaka Mungu akubariki waimbaji wa Tanzania nadhani wajifunze kwako miaka mingi upo unamtukuza Mungu lakini hauchoshi my brother Yesu akubariki Sana
@lazarozebedayo4948
@lazarozebedayo4948 Ай бұрын
Amen wimbo mzuri Sana unaponya moyo
@Bryson883
@Bryson883 8 ай бұрын
Huu Wimbo ni Mawaidha, huu wimba ni mahubiri, huu wimbo ni Ibada, huu wimbo ni Misa takatifu...ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu...endelea kutimiza jukumu la Mungu kukuleta Duniani🙏
@Ijusthavequestions
@Ijusthavequestions Жыл бұрын
True worshipers will worship in Spirit and Truth.
@christinamwangoc4779
@christinamwangoc4779 Жыл бұрын
Namshukuru MUNGU kwa ajiliyako kwamaana katikati ya mabadiliko ya dunia Sayansi na tecnolojia lkn bado nakupata kakaangu unaemwimbia MUNGU ktk roho na kweli, MUNGU AKUTUNZE !
@nellykobadi8142
@nellykobadi8142 Жыл бұрын
Uko wapi moyo wa ibada, moyo kutetemeka aiseeeh Mungu nipe moyo wa ibada nikuabudu katika roho na kweli
@rebeccan2321
@rebeccan2321 2 ай бұрын
Uko wapi wa moyo wa Ibada ,ee Mungu wangu nanyenyekea kwako nope Moyo wa Ibada nikuabudu ktk Roho na kweli.❤
@martinchambai5460
@martinchambai5460 Жыл бұрын
Wimbo mzuri sana. Picha pia iko vizuri sana. Mungu aibariki huduma yako
@yuzzob
@yuzzob 20 күн бұрын
Nyimbo za hivi ni signature ya Ambwene. Bwana Yesu asifiwe sana 🙏🙏
@mackrinaerenesto6402
@mackrinaerenesto6402 Жыл бұрын
Amina baba ubalikiwe San nabarkiwa San na nyimbo zako na haipit sku nimeskilza nakpenda san maana nyimbo zako nazielewa sana 🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽❤️❤️❤️❤️❤️
@citovunjabeilimitedcompany4455
@citovunjabeilimitedcompany4455 Жыл бұрын
Naomba jina lako kamili nikutumie muchango mdogo imekuwa muda ume nibariki sana
@ambweneobadiamwasongwe
@ambweneobadiamwasongwe Жыл бұрын
Mungu akubariki Sana 0767619931 au 0713619931 Ambwene Mwasongwe
@ZaiElias
@ZaiElias Ай бұрын
Amina🎉🎉❤
@jannethjohn747
@jannethjohn747 Жыл бұрын
Kaka Ambwene wewe endelea hivyohivyo kumsikiliza Mungu ktk huduma yako, hubiri kupitia uimbaji, tulio wengi chanzo cha kuokoka ni kupitia uimbaji, achana nao hao wanaoifuata dunia, wewe mtumikie Mungu kikamilifu
@Gwa-Kayaga
@Gwa-Kayaga Ай бұрын
Hapa comment za wakenya ni chache na sababu ni za kiroho,,, hongera sana mtu wa rohoni kaka🎉
@lucywilson5875
@lucywilson5875 Жыл бұрын
Hizi ndizo nyimbo tunazohitaji kusikiliza. Barikiwa Ambwene
@mzurikwaorevocatus2972
@mzurikwaorevocatus2972 Жыл бұрын
Kwel yan
@givasmwananzumi5941
@givasmwananzumi5941 Жыл бұрын
@@mzurikwaorevocatus2972 kabisaaa hi nyimbo nzuri xn
@REHEMAMGENI
@REHEMAMGENI Ай бұрын
Amen ambwene
@AnnaMasangula-h5e
@AnnaMasangula-h5e 13 күн бұрын
Mungu nisaidie mengi yanautesa moyo wangu, from now nimeachilia
@nasramtuluma3949
@nasramtuluma3949 Жыл бұрын
Nasikiliza huku nasisimka...asante kwa msg nzur
@jamesbavo
@jamesbavo Жыл бұрын
Namshukuru Mungu kwa kutupatia zawadi hapa Tanzania 🇹🇿 ambayo ni #Ambwene_Mwasongwe na #Boaz_Danken kiukweli nyie watu mna Mungu ninaemuabudu mimi na mnaongozwa na Roho wa kweli
@nancygilliad2883
@nancygilliad2883 Жыл бұрын
Wimbo huu unanibariki sana san haya ndio mambo yapo leo makanisan Mungu atusaidie kweli,ubarikiwe Ambwene
@magrethmkongwee8512
@magrethmkongwee8512 Жыл бұрын
Katika watumishi wa Mungu tuliobaki nao Tz wanaoimba katika roho na kweli! Barikiwa saana Mtumishi! Unaponya saana mioyo ya wengi!
@mzurikwaorevocatus2972
@mzurikwaorevocatus2972 Жыл бұрын
N kwel
@jeanettekikonde987
@jeanettekikonde987 Жыл бұрын
Kwel kabisa nyimbo zake. Pamoja na mavazi yake inapendeza Sana ubarikiwe sana maombi ni silaa tosha
@franksentiyongo8803
@franksentiyongo8803 Жыл бұрын
Ninapo sikiriza wimbo huu najifunz kitu mungu akubark ambwene mwasongwe ukyala utufighwe fihjo kangi fihjo
@robertwaichigo2553
@robertwaichigo2553 Жыл бұрын
Huu ni zaidi wa Wimbo. Ujumbe wa Yesu Kristu.
@faithikenda
@faithikenda Жыл бұрын
Natamani sasa Mungu akupe neema ya kuanza kufundisha na semina, seems you have more and we need to hear more!! Una hazina kubwa moyoni mwako .. Ikimpendeza Mungu akupe namna nyingine ya kutufikishia kwa wingi. Stay blessed
@beatricemwasunda5027
@beatricemwasunda5027 Жыл бұрын
Jehovah aonaye Sirini braza azodi kukuweka makumbusho kwa ajili ya UTUKUFU WAKE...Ahsante nimepokea ujumbe wangu
@ZawadiAndongwisye
@ZawadiAndongwisye 16 күн бұрын
Wimbo una ujumbe mzur sana MUNGU akubariki sana umeenda kimaandiko
@brendakinenekejo8464
@brendakinenekejo8464 Жыл бұрын
Nmejikuta nanena kwa lugha barikiwa mtumishi wa bwana
@daynesnyoni2715
@daynesnyoni2715 Жыл бұрын
Kuna vile hii nyimbo inatuonesha bible ni kitabu kizuri sana, kitachotufanya tukutane na watu walioshi maisha kama yetu , ILa walikuja kubadirika na kuwa watu wema sana, mungu akubariki na kukutunza sana kaka ambwene, akuweke ili kupitia wewe wengi kati yetu tumrudie mungu🤲 na kuijua kweli🙏.
@farajaemanuel1992
@farajaemanuel1992 Жыл бұрын
Tenashara wa kizazi hiki. Yesu angekuchagua kuwa tenashara kaka,, Coz angeutazama moyo wa Utumishi ndani Yako.
@ozanasylvester3663
@ozanasylvester3663 Жыл бұрын
Ee Mwenyezi Mungu tunaomba utusaidie masikio ya Rohoni tunapo hubiriwa mafundisho kama haya kwa nyimbo tusiyapuuze bali yakalete mabadiliko ndani ya mioyo yetu.Amina
@eliufoosimonchuri4160
@eliufoosimonchuri4160 Жыл бұрын
Mtumishi wa Bwana ubarikiwe. Tumepata ujumbe toka Yohana 4:24 kwa njia ya nyimbo. Kiukweli huwa unaimba theologia, tunapona kwa nyimbo zako. juzi mwana wa Azali, leo tena ujumbe huu muhimu.Mungu atusaidie tuabudu katika roho na kweli 🙏🙏🙏
@emmasanga4279
@emmasanga4279 Жыл бұрын
Ubarikiwe sana Kaka endeleaa mbele .
@giftasifiwe
@giftasifiwe Жыл бұрын
Hii nyimbo imenikumbusha mwaaka 1984.kanisani.turivyofundishwa.
@daudicherehanis
@daudicherehanis Жыл бұрын
mungu akuzidishe katika huduma yako
@johnmgaya2280
@johnmgaya2280 Жыл бұрын
Nataka like zenu kama huna kinyongo na mwenzio ( moyo mweupe)
@moseskipawua9548
@moseskipawua9548 6 күн бұрын
😢😢😢😢😢😢😢😢😢
@afisaardhi7310
@afisaardhi7310 13 күн бұрын
You are a true and complete definition of Gospel Music in East Africa.
@vedastomtasha
@vedastomtasha Жыл бұрын
Hakika wew ni mwamna imara daaaa nyimbo nmeikuta TikTok daa nmeifata ujumbe mzito sana najivunia kua na wew tz
@ebenezerdayan3797
@ebenezerdayan3797 Жыл бұрын
Duh!!!kuna wakati Daudi akiona kile Mungu amekiweka ndani yako anafarijika sana huko mbinguni na anatabasamu akijua kapata pacha aliyebaki hapa duniani. Ninampenda Mungu kwa ajili yako Ambwene🙏🙏🙏
@maggishillah4847
@maggishillah4847 Жыл бұрын
Kabisaa yaani... It's a Powerful Song!
@juliananicodemus2746
@juliananicodemus2746 Жыл бұрын
Wimbo mzuri mungu akubariki sna kaka Ambwene
@joellumala3206
@joellumala3206 Жыл бұрын
Our own Ambwene,. Kanisa letu la Tanzania lina baraka sana kuwa na mtu wa aina yako,. Umebarikiwa ulikumbushe kanisa na watu wa Mungu kuhusu maisha halisi ya Rohoni kabisa kabisa,.😌
@neemakitano5894
@neemakitano5894 Жыл бұрын
Kaka Ambwenee nabarikiwa Sana nanyimbo zako. MUNGU akubariki sanaaaa sanaaaa 🙌🙌🙌🙌
@rosadinahjoseph9137
@rosadinahjoseph9137 Жыл бұрын
Wimbo huu hunifanya ni barikiwee sanaa .... Mungu akutunzeee mtumishi
@mariampatrick3479
@mariampatrick3479 Жыл бұрын
Hakika mwenyez MUNGU amekubarik kipaji MUNGU aendelee kukutumia
@vickynduku4753
@vickynduku4753 Жыл бұрын
Ambwene mwasongwe is underated his music is beyond international level ...God bless you MoG ...my favorite artist
@milkajm4762
@milkajm4762 Жыл бұрын
😭😭😭😭 Mungu tusaidie kurudi katika Neno na tuishi katika Roho.
@esthermwaigwisya1775
@esthermwaigwisya1775 Жыл бұрын
Ambweneeee ndaga fijooooo utukufu kwa YESU. Naitwa Happy Mwaigwisya. Prophetess of the most high God.
@kelvinkijo7500
@kelvinkijo7500 Жыл бұрын
Amen sana ubunifu mkubwa mtumishi wa BWANA, zidi kubarikiwa!
@pardonmwalyego9947
@pardonmwalyego9947 Жыл бұрын
Kwa nyimbo zako tunamtukuza Mungu....live long life in music!! Stay blessed.
@josephinemwambe3385
@josephinemwambe3385 Жыл бұрын
Huu wimbo umasema yanayotendeka kwa makanisa siku hizi Mtumishi wa mungu kakangu Ambwena kwa kweli nyimbo zako za nitia nguvu sana.. Wimbo mtaamu mno..Barikiwa sana South Africa 🇿🇦 Cape Town tunabarikiwa Ujumbe ufikia watoto wetu nchini Kenya 🇰🇪
@geitandelwa299
@geitandelwa299 Жыл бұрын
Ameni tuna Mambo MENGI Ila Sio ya MUNGU
@sarahnyamwendo2118
@sarahnyamwendo2118 Жыл бұрын
Nyimbo niipendayo kila sku lazma niiskize Mungu akubariki sana kweny huduma
@gwamakamwakipesile5884
@gwamakamwakipesile5884 Жыл бұрын
GOD Bless you my brother. Humu ndani hatuwezi kuyandika yote ambayo MUNGU amekuwa akiyafanya huku mtaani/nje kupitia uwimbaji wako. MUNGU amegusa mioyo ya watu wengi sana kupitia hiyo karama aliyokupa. Endelea kuichochea.
@neemashirima1617
@neemashirima1617 Жыл бұрын
🥳🥳🥳🥳 Mungu azidi kukupa mafunuo Mtumishi wa Mungu kulifundisha kanisa kile Mungu anataka tuenende nacho🙏🏼🙏🏼 yaan ni ujumbe kwa kanisa na mtu mmoja mmoja anayetaka kumwona Mungu katika viwango vingine
@sebastianmwantuge5597
@sebastianmwantuge5597 Жыл бұрын
Sijashangaa kwa uzuri wa wimbo huu maana Mungu amekuinua,nyimbo zako zote ni nzuri na zina mafundisho. Mungu aendelee kukuinua.
@malifedhamachimu4882
@malifedhamachimu4882 Жыл бұрын
Mungu aendelee kukutumia mtu wa Mungu yaani unaimba rohoni ,,,ujumbe umekamilika kabisa wokofu ni utakatifu siyo kuhubiliana miujiza tuu Nadhani wamesikia...
@amonramothy6790
@amonramothy6790 Жыл бұрын
Najifunza na ninakua kiroho kupitia jumbe zitokanazo na Neno la Mungu.. Barikiwa sana mtumish wa Mungu..
@kamotajunior1681
@kamotajunior1681 Жыл бұрын
This is exactly what is happening in our churches today, wimbo huu una mafundisho ya kweli.....
@katarinasimon8647
@katarinasimon8647 2 ай бұрын
Nzuri sana jamani eeeh baba akubariki Mungu aah😅
@BenCheck-jx9lo
@BenCheck-jx9lo Жыл бұрын
Wewe ni mbaraka kutoka kwa Mungu. Mataifa yote yatasikia na kutambua Mungu yupo. Siku zote Nyimbo zako zinagusa na kupenya katika nyoyo za watu. Ubarikiwe sana.
@ireennanjela2993
@ireennanjela2993 Жыл бұрын
Huu wimbo umefundisha ubarikiwe mtumishi endelea kua kiroho acha roho aendelee kukuongoza ktk utumishi wako.
@damasmayanja2930
@damasmayanja2930 Жыл бұрын
Hii ni Injili, this is Gospel mpeni maua yake Mwasongwe
@pascazianhigula1900
@pascazianhigula1900 Жыл бұрын
Kwa neema ya Bwana hujawahi kukosea ,sifa na utukufu ni kwa Bwana nangoja official video ya UMENIPA HESHIMA 🔥🔥🔥
@TinahNgailo
@TinahNgailo 13 күн бұрын
Mung awe naw napenda san nyimbo zako hasw ile ya watoto yatima
@kumbukamwasanguti855
@kumbukamwasanguti855 Жыл бұрын
Kumbe Yesu alikuta Ibada zetu nyingi Feki...Daima nakukubali Ambwene, Mungu aendelee kukuinua!!
@glorymusa4869
@glorymusa4869 Жыл бұрын
I'm blessed Mungu aendelee kukutumia jinsi apendavyo yeye mtumishi🙌💅🙌
@michelmwamba5630
@michelmwamba5630 Жыл бұрын
Ubarikiwe na Mungu ! Nyimbo zako zimenibariki Sana! Toka DRCongo. Lubumbashi.
@NadsonAnthony
@NadsonAnthony 3 ай бұрын
Amen! Tunashukuru sana kwa habari njema (Good News) unazotupatia kupitia nyimbo Mtumishi Mungu akubariki sana 🙏🙏🙏
@rebeccakatasi2778
@rebeccakatasi2778 Жыл бұрын
Aksanti Sana kwa huu wimbo umenifunza kutokuhikumu ndugu zetu Bali tujihukumu wenyewe. Mungu aniwezeshe n'a akubariki pamoja n'a kwaya njima. Nawafata apa congo Kinshasa RDC
@rtlusungu
@rtlusungu Жыл бұрын
Sema Ambwene una madini sana.. Daaah, we endelea tu kuimba Kaka, sisi tunapona huku.. Songs straight from the throne of heaven.. Hiki kizazi kina bahati ya kuwa na mtu kama wewe.
@safindume5051
@safindume5051 Жыл бұрын
Kabisa
@selestinekaale7545
@selestinekaale7545 Жыл бұрын
Ni kweli kaka usemalo, Aisee! Halafu Tazama Hekima za BWANA, yeye kaka Ambwene anaona kawaida tu Aisee!😃😃
@willyke2251
@willyke2251 Жыл бұрын
Very true
@gilbertgodfrey6376
@gilbertgodfrey6376 Жыл бұрын
Kabisa huyu mwamba namkubali kinoma maana hamuigi mtu kuimba na anaimba kwa kumaanisha
@gilbertgodfrey6376
@gilbertgodfrey6376 Жыл бұрын
Yaani waimbaji wa siku hizi naona wamebaki wamili Ambwene na mchungaji abiudi wengine wote wanarapu na wananiudhi sana maana wanatoka nnje ya maadili ya mungu
@emanueldarema1751
@emanueldarema1751 Жыл бұрын
Mungu akubariki sana Ambwene Mwasongwe. Full song from the Scriptures. My favorite Tanzanian Gospel Artist.
@evansimsagaatkog1953
@evansimsagaatkog1953 Жыл бұрын
Mtumishi wimbo huu uko vizuri Sana Sana ebuwatu wausikilize ktk Roho Kuna Mambo makubwa ya kujifunza
@gloriaamase9764
@gloriaamase9764 Жыл бұрын
Ameen ni kweli kabisaa mtumishi wa Mungu hiyo ndo inatendeka kwa sasa mtu akisaidia mwenzake anapost kwa mtandao ndo dunia yote ijuwe alisaidia lakini si hivyo maandiko inasema unapotowa kwa mkono wa kulia mkono wa kushoto usijuwe inatufunza nini wakati unasaidia mwenzako mtu yeyote asijuwe ni Mungu pekeake anafaa kujuwa barikiwa sanaaa Mtumishi wa Mungu
@patranabwire4012
@patranabwire4012 Жыл бұрын
I love this man of God Bless u🇺🇬🇺🇬
@Jehovarohiband
@Jehovarohiband Жыл бұрын
Huyu Mtumshi anaimbia Mungu wakweli kabisa eee Mungu umuongoze asitoke kwenye mstari wako Kama wengine
@gracepetro5430
@gracepetro5430 Жыл бұрын
Yaani MUNGU atusaidie Sana watu sikuhizi wanahukumiana,pasipo kujiuliza kuwa hata tunao hukumiana hatujakamilika,,watu tunajipendelea,wenyewe hasa mtu ukiwa na fedha ndo utapendwa balaa ,ukiwa huna utazalauliwa Sana ,,God bless you
@prosperkileo7139
@prosperkileo7139 Жыл бұрын
AMEN AMEN AMEN UBARIKIWE NA KRISTO YESU ALIE HAI BINAFSI NIMEBARIKIWA NA KUJIFUNZA
@florentinafabian3537
@florentinafabian3537 Жыл бұрын
The music saasa; uwiiiiii this song 🙌🙌🙌🤭... life transforming to the church kabisa kabisa 😭🙌
@didacebigirimana7350
@didacebigirimana7350 Жыл бұрын
Nadondokaga machozi nikisikia nyimbo zako zina nigusa saana,unanisaidia saana Kwendelea na njia ya kwenda kwa Baba mbinguni,nakuombea saana kaka 🇧🇮🇺🇸🇹🇿
@barikimpomwa6539
@barikimpomwa6539 Жыл бұрын
Hii mwimbo nilivyo isikiliza nimeisikia nimeamua kuilipeat kila wakati kutokokana na uzima na uwezo wa Mungu ulioifunika,,Mungu akuongezee ujuzi na maarifa zaidi
@Jenipha-so9rk
@Jenipha-so9rk 2 ай бұрын
Ibada njema
@ConfusedMonarchButterfly-bp5dx
@ConfusedMonarchButterfly-bp5dx Ай бұрын
Amina ❤❤
@SamsonEzekiel-or9xc
@SamsonEzekiel-or9xc Ай бұрын
Halloo halloo hii imeenda safiiii oyoooo
@katekoeddah6606
@katekoeddah6606 Жыл бұрын
Mungu niondolee roho ya majivuno, wapendwa tumwabudu Mungu katika roho na kweli., Barikiwa sana kakaangu,. Mungu akutunze
@LuganoMwandoto-pf8zg
@LuganoMwandoto-pf8zg 8 ай бұрын
😀🔥Mungu akikupa kibari sehemu frani🔥 usinyamaze🔥🙌
@hyasintapastory4398
@hyasintapastory4398 Жыл бұрын
Naupenda sana huu wimbo
@mamakoku5123
@mamakoku5123 Жыл бұрын
uko kama mrisho mpoto kwenye muundo wa mashahiri lakin wewe uko kizazi zaidi , ubarikiwe sna Big Up
@anganilekalinga9574
@anganilekalinga9574 5 ай бұрын
MUNGU ni roho hukumu zake ni za rohoni ❤❤❤nampenda BWANA YESU ❤❤❤🎉
@b.jmwalupii7684
@b.jmwalupii7684 Жыл бұрын
Hongera kwa huu wimbo mzuri
@yusuphharamba7520
@yusuphharamba7520 Жыл бұрын
I feel so happy to see...how gospel is sang sooo well. . make straight the way of the LORD brother AMBWENE. Mungu akubariki.. Am proud.
@mamacaren1519
@mamacaren1519 Жыл бұрын
Kaka nabarikiwaga sana na nyimbo zako hakika unanigusa sana nakuelewa sana nazichambuaga mpaka napata maana Barikiwaaa
@stayupethan6216
@stayupethan6216 Жыл бұрын
Nyimbo zako ni za Baraka sana zinaponya na kutupa nguvu hakika Mungu amekufanya chombo cha ibada sifa utukufu na heshima vimrudie kristo Mungu azidi kukuongoza
@morrismuriithi6741
@morrismuriithi6741 Жыл бұрын
Powerful Message! "Inatupasa kumwabudu kwa Roho na Kweli. Anaye tafsiri lugha ya Moyo" Mungu akubariki sana Ambwene Mwasongwe.
@user-tk2lw3wu2u
@user-tk2lw3wu2u 2 ай бұрын
Glory to God ❤❤
@merymalachy1707
@merymalachy1707 Жыл бұрын
Asante kaka...kwa huu wimbo hakika una mafunzo, much love from kenya 🇰🇪
@VastineKahindo
@VastineKahindo 26 күн бұрын
Hi wimbo unanijenga sana
@MorganjustusK
@MorganjustusK Жыл бұрын
Wow! Jamani ndugu yangu Ambwene Mungu akubariki...Wewe unaimba Kaka ukweli kulingana na Neno lake Mwenyezi Mungu...Naposikiza nyimbo zako zanipa kunyenyekea na kubondeka mbele za Mungu...I say Kaka unaimba,,, Na huu ndio ukweli ambao kizazi hiki chaitaji..Baraka Mtu wa Mungu
@lewinalameck2643
@lewinalameck2643 Жыл бұрын
Waoooh,mtumishi unaimbaaa ubarikiwe
@TheKapungala
@TheKapungala Жыл бұрын
I just love how our Tanzanian brothers and sisters make music straight from the scriptures. More love form Nairobi!
@rogathesarwatt
@rogathesarwatt Жыл бұрын
All about Lugha Adhu ya Kiswahili
@paulwachenje861
@paulwachenje861 Жыл бұрын
That's exactly what I was heading to post but you represented the likes of us well
@barakahiluka4905
@barakahiluka4905 Жыл бұрын
Mungu akubaliki sana mtumishi👐
@danielnzali5609
@danielnzali5609 Жыл бұрын
Mungu akutunze mtumishi....🔥🔥
@dollnjosy3210
@dollnjosy3210 Жыл бұрын
🙏🙏❤️
@isayasementi2646
@isayasementi2646 Жыл бұрын
Ubarikiwe kaka AMBWENE hakika MUNGU katupa wewe zawadi watanzania
@stelaezekiel9858
@stelaezekiel9858 Жыл бұрын
Nenda na usitende dhambi tena. ukawe na moyo wa ibada unaotetemeka usikiapo neno la Mungu. Barikiwa sana;:;
@lexiennaturals8366
@lexiennaturals8366 Жыл бұрын
This guy his songs are in a different realm be blessed. Love from kenya
@alfredymgaya2520
@alfredymgaya2520 Жыл бұрын
🙏🙏🙏✍️mungu akutie nguvu zaidi
@linahanindo7363
@linahanindo7363 Жыл бұрын
True. Listened to this song after you recommended, leads one to repentance 🙏
@anithamushi7979
@anithamushi7979 Жыл бұрын
Glory to God.....very powerful massage....Mungu aendelee kukutumia kaka ..nyimbo zako zinamtukuza Mungu mioyoni mwetu na kutufundisha
@michaelmwanda1673
@michaelmwanda1673 Жыл бұрын
Mungu wa mbinguni akubali sana mtumish wa bwana kristo akutie nguvu
Ambwene Mwasongwe - Unikumbuke (Official Music Video)
7:56
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 900 М.
Ambwene Mwasongwe - Nimeachilia (Official Music Video)
7:17
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 990 М.
Василиса наняла личного массажиста 😂 #shorts
00:22
Денис Кукояка
Рет қаралды 10 МЛН
OMG😳 #tiktok #shorts #potapova_blog
00:58
Potapova_blog
Рет қаралды 4,3 МЛН
The day of the sea 🌊 🤣❤️ #demariki
00:22
Demariki
Рет қаралды 102 МЛН
Uso Wangu
9:52
Emmanuel Mgogo - Topic
Рет қаралды 42 М.
Emery kuhimba - Mwamba Wangu ( Official live recording video )
12:45
Annoint Amani - Msizike bado yuko hai ( official music video )
8:54
Annoint Amani
Рет қаралды 106 М.
OMBI LANGU BY AMBWENE MWASONGWE (OFFICIAL MUSIC VIDEO)
5:52
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 4 МЛН
Bony Mwaitege - Acha Nizaliwe (Official Music Video)
6:58
Bony Mwaitege Official
Рет қаралды 2,7 МЛН
KISHINDO CHA WAKOMA (OFFICIAL VIDEO) - NJIRO SDA CHURCH CHOIR
6:32
Njiro SDA Church
Рет қаралды 12 МЛН
Ambwene Mwasongwe - Tumekubalika na Mungu(Official Music Video)
7:17
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 536 М.
Bahati Bukuku - Picha ya Mama (Official Music Video)
8:21
Bahati Bukuku
Рет қаралды 1,6 МЛН
Қанат Ерлан - Сағынамын | Lyric Video
2:13
Қанат Ерлан
Рет қаралды 3,1 МЛН
Kobelek
4:11
6ELLUCCI - Topic
Рет қаралды 378 М.
IL’HAN - Pai-pai (lyric video) 2024
3:24
Ilhan Ihsanov
Рет қаралды 64 М.
Zattybek & ESKARA ЖАҢА ХИТ 2024
2:03
Ескара Бейбітов
Рет қаралды 143 М.
Ozoda - JAVOHIR ( Official Music Video )
6:37
Ozoda
Рет қаралды 9 МЛН
IL’HAN - Eski suret (official video) 2024
4:00
Ilhan Ihsanov
Рет қаралды 852 М.
Duman - Баяғыдай
3:24
Duman Marat
Рет қаралды 172 М.