Рет қаралды 26,529
Viongozi mbalimbali wa dini waliokuwa mstari wa mbele kwenye kutaka tume huru ya uchaguzi akiwemo Father Charles Kitima, Aksofu, Askofu wa Dayosisi ya Karagwe, Dk Benson Bagonza pamoja na Askofu wa Kanisa la Uamsho la Moravian, Emmaus Mwamakula wakizungumzia hatua ya Serikali ya kupeleka bungeni miswada inayolenga kufanya mabadiliko kwenye tume ya uchaguzi.
Viongozi hao wamezungumza leo Ijumaa, Novemba 10, 2023 nnje ya ukumbi wa bunge ambapo awali walishuhudia mishwada mitano iliyosomwa bungeni kwa mara ya kwanza.