No video

KIGOMA YA SASA SIO YA ZAMANI: MIKAKATI MIKUBWA YAWEKWA KUIMARISHA BANDARI ZA ZIWA TANGANYIKA

  Рет қаралды 9,115

Millard Ayo

Millard Ayo

Күн бұрын

MENEJA wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama amesema kuwa katika Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) inatekeleza miradi miwili ya uboreshaji wa miundombiu ya bandari ikiwemo ya kujenga gati kwenye eneo la Lagosi na kwamba utekelezaji wake umefikia asilimia 85.
Akizungumza mbele ya waaandishi wa habari, Salama amesema kuwa mradi huo ni wa miezi 24 na hivyo mkandari aliyepewa kazi ya ujenzi wa gati hiyo atatakiwa kukabidhi mradi Aprili 2020.Kwa hiyo utaona ni kwamba mwekelekeo wa mradi huo ni mzuri na utamalizika kwa wakati.
Amesema mbali ya ujenzi wa gati katia bandari hiyo pia kuna ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mizigo, jengo la abiria, nyumba ya mfanyakazi wa Bandari ambaye atakuwa anahudumia eneo hilo pamoja na ujenzi wa miundombinu mingine wezeshi ambayo itachangia kufanya shughuli za kibandari kuwa bora na za kiwango kinachohitajika.
Amefafanua wakati hayo yakiendelea katika Ziwa Tanganyika, pia watawezesha kumairika kwa mawasiliano ya kibiashara kati ya wenzao wa DRC na nchi nyingine ambazo ni jirani na Tanzania.Pia ujenzi wa miundombinu utapunguza gharama kwa wananchi ambao wanasafiri kupitia Ziwa Tanganyika.
Salama amesema pia kuna mradi mwingine mkubwa ambao unafanyika kwenye Bandari ya Kalya ambayo wao wanaiita Sibwesa ambapo ujenzi wa bandari kubwa tayari umekamilika kwa asilimia 100." Nasi TPA tumeshaweka mashine pale ya kuanza kutoa huduma tafsiri yake tunawaambia wana Kigoma ya kwamba sasa Sibwesa imeanza kutoka huduma na imekamilika na meli zinaweza kutia nanga pale.

Пікірлер: 8
@mayungavicent6104
@mayungavicent6104 4 жыл бұрын
Jamaa yuko vizuri sana kiutendaji,kigoma itabadilika sana,wampatie muda tu
@charlesjuma6279
@charlesjuma6279 4 жыл бұрын
Mtu wa kwanza ku view apewe tuzo yake
@selemanijilla5978
@selemanijilla5978 3 жыл бұрын
Kwa mafuta tumieni reli siyo Barbara zina haribika kwa mizigo mizito
@nasibugunda7927
@nasibugunda7927 4 жыл бұрын
Zito aache kubweka bweka tu Maendeleo hayalamizimishwi mawndeleo hufika kila sehemu kwa wakati
@rashidyahya6904
@rashidyahya6904 4 жыл бұрын
Kigoma in hitaji meli mpya ya abiria
@msafiriiddy3135
@msafiriiddy3135 4 жыл бұрын
kigoma shamba tu
@hussenmzaganya1081
@hussenmzaganya1081 4 жыл бұрын
kila mji ulianza kua shamba, halafu ulivyo na wivu nani kabishana na wewe kama kigoma ni shamba au sio shamba?
@donaldmgomba7571
@donaldmgomba7571 4 жыл бұрын
Mshamba hajielewi huyu ,hajui hata maana yashamba,
白天使选错惹黑天使生气。#天使 #小丑女
00:31
天使夫妇
Рет қаралды 14 МЛН
Zombie Boy Saved My Life 💚
00:29
Alan Chikin Chow
Рет қаралды 28 МЛН
Whoa
01:00
Justin Flom
Рет қаралды 41 МЛН
HII NDIO BANDARI YA PILI KWA UKUBWA  ZIWA TANGANYIKA..
6:29
Global TV Online
Рет қаралды 3,2 М.
Mohammad bin Salman: Prince With Two Faces
54:00
Show Me the World
Рет қаралды 5 МЛН
Congo, Thrill of the River | Deadliest Journeys
49:39
Best Documentary
Рет қаралды 4,9 МЛН
MVUA ZINAVYOLETA ADHA KIGOMA
6:40
Mwananchi Digital
Рет қаралды 1,7 М.
RAIS SAMIA AZINDUA NA KUKABIDHI NDEGE VITA NA MABASI KWA JWTZ
1:54
白天使选错惹黑天使生气。#天使 #小丑女
00:31
天使夫妇
Рет қаралды 14 МЛН