Mambo matano 5 yenye kuharibu Swaumu (Funga)

  Рет қаралды 1,349

Muslimu Tv

Muslimu Tv

3 жыл бұрын

Kufunga swaumu ni kutokula, kunywa na kutoshiriki kitendo cha ngono katika muda kati ya wakati wa fajr sadiq (adhana ya pili/alfajiri ya kweli; wakati wa mchana kunapokuwa na mwangaza kwenye upeo wa macho kabla ya kuchomoza jua) na kati ya kuchwa kwa jua.
Kufunga swaumu pia kunaitwa imsak. Maana ya Imsak ni kuiweka roho/nafsi mbali na inayoyatamani na kutoyafanya. Kinyume cha imsak ni iftar, yaani kufutari.
Amri ya Kidini ya Kufunga Swaumu
Kufunga swaumu ni moja ya nguzo tano za Uislamu. Wakati huo huo, ni moja ya alama kubwa za Uislamu. Imefaradhishwa (wajibu) katika mji wa Madinah, mwaka mmoja na nusu baada ya Hijra (Kuhama Makka kwenda Madinah) na siku ya tarehe 10 mwezi wa Shaban. Uwajibu wake umeanzishwa na Kitabu (Qur’an), Sunnah (mwenendo wa Mtume) na Ijma’ (makubaliano ya ummah/jumuia au ulama/wanazuoni wa Uislamu).
Katika Qur’an yanaelezwa yafuatayo:
Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyoandikiwa walio kuwa kabla yenu… (Qur'an, Al-Baqarah, 2:183)
Kufunga swaumu pia ni ibada ya kimwili kama wajibu sala ya faradhi. Sifa maarufu ya ibada hii ni kwamba inawaepusha mbali na maovu, na hilo linadhibiti matamanio ya ziada na kuihimiza nafsi. Katika hadith, inaelezwa hivi:
Kufunga swaumu ni ngao (inawakinga binadamu kutokana na matamanio na maovu). Aliyefunga hatakiwi kutamka maneno machafu kutokana na ujinga. Aliyefunga asiwajibu wanaotaka kupigana na kupambana naye kwa kusema tu: mimi nimefunga.’
Kwa kuwa kufunga swaumu kunawakinga wanaadamu dhidi ya kuinikia maovu, Mjumbe wa Allah (S.A.W.) amewashauri vijana, makapera kufunga swaumu ili kupunguza msongo wa matamanio ya ashiki. Pia ni ukweli unaokubalika kisayansi kwamba kufunga swaumu kunatuliza hisia za matamanio ya ashiki.
Mwezi wa Ramadhani unapoingia, kunakuwa na upungufu mkubwa wa matukio ya uhalifu yanayofanyika katika jumuia. Maovu hufifishwa hadi kiwango cha chini. Matokeo yake, matendo mema huongezeka. Kunakuwa na makaribishano kunjufu na upendo. Kusaidiana kwa pande mbili pamoja na mshikamano huongezeka. Mjumbe wa Allah (S.A.W.) anafafanua sababu ya athari ya kijamii iliyomo kwenye kufunga swaumu katika hadith ifuatayo:
Inapoingia Ramadhani, mwezi wa kufunga swaumu, milango ya Pepo hufunguliwa; milango ya Moto hufungwa na mashetani wote hupigwa pingu.
Thamani kubwa iliyomo katika kufunga swaumu mbele ya Allah inaelezewa katika hadith qudsi ifuatayo:
Matendo mema yote na ibada wanazozifanya wanadamu ni kwa ajili yao wenyewe (upo wasiwasi wa starehe na manufaa kwao). Hata hivyo, kufunga swaumu sio hivyo. Kufunga swaumu ni ibada inayofanywa kwa ajili ya ridhaa Yangu. Na Nitaitolea malipo.
Katika hadith qudsi nyingine, inaeleza:
Kwa kila tendo jema, kuna malipo yake mara kumi hadi mara mia saba. Hata hivyo. Malipo ya kufunga swaumu hayatolewi kwa kigezo hicho. Kwa kuwa ni kwa ajili Yangu. Ni Mimi Pekee nitayoilipa.
Kama inavyofahamika kutokana na sentensi hizo, licha ya kuwa kila jema na ibada kuna thawabu zake (malipo ya matendo mema yatakayohisabiwa siku ya qiyamah/siku ya kiama) zilizoambatishiwa kuanzia thawabu 10 hadi 700, kwa upande wa funga thawab zake hazihesabiki.
Na Allah hakuyaacha malipo yake yahesabiwe na malaika Wake bali Ameyaweka kwake Yeye Mwenyewe kuyalipa. Kwa sababu hii, Siku ya Kiama, waumini watakuta thawabu nyingi kutokana na swaumu zao ambazo hawakuzitarajia.
#RamadhaniyakwanzaMambomatanoyenyekuharibuSwaumuFunga #mawaidharamadhani #mamboma5yenyekuharibufunga #mamboyakujiepushawakatiwaramadhani
Mjumbe wa Allah (S.A.W.) amesisitiza suala hili kama ifuatavyo:
Zipo furaha mbili kwa mtu anayefunga: Ya kwanza ni wakati wa kufutari (anapofungua baada ya kuzama jua); ya pili ni furaha ya kufunga swaumu (malipo yake) atapokutana na Mola wake Mlezi.
Katika baadhi ya hadith, fadhila za juu na hadhi ya heshima wanayoipata wanaofunga inaelezewa kama ifuatavyo:
Upo mlango Peponi unaitwa Rayyan. Siku ya Kiama, wale waliofunga tu ndio wataoweza kuingia (Peponi) kupitia mlango huo. Hakuna mwingine atayeweza kuingia kupitia mlango huo. (Siku ya Kiama), kutanadiwa: Wako wapi waliofunga? Waliofunga simameni na ingieni. Baada ya kuingia, mlango huo unafungwa; kuanzia hapo, hakuna atayeweza kuingilia mlango huo.
Naapa kwa Allah kwamba harufu ya njaa ya kinywa kilichofunga inaridhisha zaidi kuliko harufu ya uturi, ni msafi zaidi na maridhia mbele ya Allah.
Dua ya watu wa aina tatu haitokataliwa:
Aliyefunga mpaka afutari (mlo unaoliwa baada ya kuchwa jua ili mtu kufutari)
Mtenda haki/mkuu wa dola mwadilifu
Aliyetendewa uovu/aliyedhulumiwa.
Maswali juu ya Uislamu

Пікірлер
Sheikh Othman Maalim - Misingi ya Kuchagua Mke Anayefaa Kuoa
1:02:51
FAIDA ZA KUFUNGA/SWAUM KISAYANSI  🌴 - FUNDI Dr. SULE 🗣
52:44
Saidy Januzaj
Рет қаралды 88 М.
One moment can change your life ✨🔄
00:32
A4
Рет қаралды 29 МЛН
Playing hide and seek with my dog 🐶
00:25
Zach King
Рет қаралды 28 МЛН
It’S So Fun To Wash My Son’S Hair! #funny #baby#cute  #funnybaby
00:14
Amazing Children Toys
Рет қаралды 8 МЛН
Clown takes blame for missing candy 🍬🤣 #shorts
00:49
Yoeslan
Рет қаралды 27 МЛН
UCHUNGU ANAOPATA MTU PINDI ANAPOFIKWA NA UMAUTI PART 2
55:29
Muslimu Tv
Рет қаралды 101 М.
ADHABU KWA MWENYE KUACHA SWALA
1:02:08
IQRAA TV
Рет қаралды 1,4 М.
KHUTBAH YA IJUMAAH - SHEIKH ALI ABUBAKAR
54:31
Al Haajar TV Kenya
Рет қаралды 1,1 М.
HIVI NDIVYO VITU 10 VINAVYO HARIBU SWAUMU YAKO SIKILIZA KWA MAKINI
9:39
SHUHADAA ONLINE TV
Рет қаралды 6 М.
KISA CHA BIBI MWENYE KUJIBU MASWALI KWA QUR AN
52:57
Muslimu Tv
Рет қаралды 2,6 М.
One moment can change your life ✨🔄
00:32
A4
Рет қаралды 29 МЛН