No video

DC MAGOTI ARUDI MSIKITI ULIOLAZA WATOTO 90+, ACHANGIA MIFUKO 300 YA CEMENT “MMETEKELEZA AGIZO HARAKA

  Рет қаралды 71,031

Millard Ayo

Millard Ayo

Ай бұрын

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama, ametoa mifuko 300 ya cement kwenye vituo viwili vinavyotoa mafundisho ya Dini ya Kiislamu ikiwemo kituo kilichopo Msikiti wa Masjid Salaf uliopo Kiluvya Madukani, hatua hii inakuja siku mbili tangu aagize kituo hicho kifungwe na kuwarejesha Watoto zaidi ya 90 kwa Wazazi wao hadi watakapojenga mabweni na kupewa kibali maalum cha kuendesha mafunzo hayo, hii ni baada ya kubaini Watoto hao wanalazwa katika eneo dogo Msikitini na wengine nje ya Msikiti huku mazingira wanayopikia chakula na yanayowazunguka yakiwa hatarishi na machafu.
DC Magoti ambaye amefika Msikitini hapo akiwa na Sheikh wa Mkoa wa Pwani Sheikh Khamis Mtupa, ametoa mifuko 150 ya cement kwenye Msikiti huo na mifuko mingine 150 kwenye Msikiti mwingine unaoitwa Masijid Abdulaziz Ashlak ambako nako walibaini Watoto wakiwa wanalala kwenye mazingira yasiyo rafiki na salama na akaagiza warejeshwe mwakao “Nimefurahi agizo limetekelezwa ndani ya saa 24, nimeamua kuchangia ujenzi na nitasaidia michakato yote ya hati ya kiwanja na usajil wa kituo”
Kiongozi wa kituo hicho, Sheikh Abdul Hamid amemshukuru DC Magoti kwa kuwachangia cement huku akimuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kwa ujumla kuwachangia pia kila mmoja kwa kile atakachojaaliwa ili wawezeshe kujengwa kwa Hostel ya ghorofa 5 na Watoto warejee kuendelea na masomo… namba za kuchangia ni Tigo Pesa 0719380268 (Jina Abdallah Samudu)

Пікірлер: 471
@charlesmugisha6529
@charlesmugisha6529 29 күн бұрын
Mimi ni mkristo lakini uyu shekh kiukweli yuko vizuri ni mtu mwenye eshima na mnyenyekevu nimempenda sana mwenyezi mungu ampe maisha marefu.🙏🙏🙏🙏
@issaadinaniissa6487
@issaadinaniissa6487 25 күн бұрын
Uislamu sahihi ndio huo unyenyekevu, masalafi ndio hao karibu sana ujifunze mengine mengi
@bakarisahede9532
@bakarisahede9532 25 күн бұрын
Charlesmugisha6529 Nikweli nduguyangu hatamimi kanihuzunisha sana huyu sheghe mpole mnyenyekevu duh
@Muadhin1
@Muadhin1 12 күн бұрын
anakukaribisha ukamtembelee
@victorterry227
@victorterry227 28 күн бұрын
Shukrani Miradi Ayo kwa kutusapoti sisi waislam katika hili insha-allah Allah akulipe na akujalie ya heri na akuepushe na yashari
@rashiditembo1574
@rashiditembo1574 Ай бұрын
Mwenyezi mungu akupe maisha marefu DC wangu,na akutangulie katika majukumu yako ya Kila siku.
@jojomdosi-ip4rg
@jojomdosi-ip4rg Ай бұрын
Kiongozi mwenyezimungu hakujalie hakupe maisha marefu hakupe hulizi wa kutosha kwa kutusitili Aameen ya rabb
@KONDOBANNAHMUSIC
@KONDOBANNAHMUSIC 24 күн бұрын
Huyu DC hapo ata akifa Leo ghafla PEPONI anaenda
@KONDOBANNAHMUSIC
@KONDOBANNAHMUSIC 24 күн бұрын
​@@jojomdosi-ip4rgkabisa yani sikutegemea aseeeee kama angerudi kwa staili hiyo huyu BANA mi namuombea aseeee ni mtu mwema
@sufianijuma5568
@sufianijuma5568 Ай бұрын
Kwel,Allah amesema kwel ktk Quruan ,Mnaweza mkachukia jambo likawa heri yenu na mnaweza mkapenda jambo likawa shari yenu,Allah tuzidishie subra Waislam na hekma na busara kwan aman kwetu ndo tulio usiwa na mtukufu wa daraja.Allah iongeze nchi yetu muongoze Dc Magot aijue haki na aifuate,Amyn Amyn Amyn.bila kusahau Mpe Hekima na Busara Rais wetu Samiya Suluhu Hassan❤Amyn Amyn Amyn
@YohanaThadeo-ki2qg
@YohanaThadeo-ki2qg 29 күн бұрын
Samia
@RamaahMtulivu
@RamaahMtulivu 18 күн бұрын
Wallah DC Allah akupe maisha malefu na akuonyeshe haki aamin. Sheykh Allah akulipe Kila kheiri liwe kwako kwa jitihada zako fidunia walikhera aamin.
@kilogreekachananawatuwasio4054
@kilogreekachananawatuwasio4054 Ай бұрын
Huyu sheikh muelevu sana msikilivu mungu Awabariki viongozi wote na sheikh wangu ❤❤❤
@Allybinamour
@Allybinamour Ай бұрын
Kwa hapa DC umekua kiongozi unaepaswa kua mfano wakuigwa. alhamdulillah kiongozi wewe allah akubarik. asante DC kwa kazi nzur mashallah
@christinewomanoffaith5479
@christinewomanoffaith5479 29 күн бұрын
SI mnatuita makafir,haya kafiri kawasaidia Kwa hekima ti
@Allybinamour
@Allybinamour 29 күн бұрын
@@christinewomanoffaith5479 kufanya wema hakuondoi dini ya mtu, na wala si makosa kumsifia kafiir anapofanya jambo la maslah kama hili. na huo ndio uadilifu.
@trophywilson7211
@trophywilson7211 27 күн бұрын
​@@AllybinamourNa Wewe kafiruna pia
@user-dq8qu5oy3u
@user-dq8qu5oy3u Ай бұрын
Tunaomba namba ya kutuma michango japo kidogo jambo la kheri Hilo,hongera MKUU WA Wilaya Kwa Moyo Mkuu
@fahadfaraj6474
@fahadfaraj6474 Ай бұрын
Namba c zimetajwa Skiza vizuri basi
@husna34562
@husna34562 Ай бұрын
Mashallah
@winfordmwangonda5375
@winfordmwangonda5375 29 күн бұрын
Hamna kidogo mbele ya kuchangia msikiti, chochote ulicho nacho ni kikubwa mno mbela ya Allah
@trophywilson7211
@trophywilson7211 27 күн бұрын
​@@winfordmwangonda5375siyo msikiti ni majengo
@masoudrashidmohammed4124
@masoudrashidmohammed4124 Ай бұрын
AL hamdulillah namshukuru Allah juzi niliandika comment yng nikasema simlaumu mkuu wa wilaya ktk hili ila nnao walaumu ni matajiri wa kiislamu wapo tyr kutoa mamilioni ya mapesa ktk mipira na baadhi ya mambo ya kipuuzi yasiokua na faida . Sasa kiongozi Magoti hapa umeqapiga pini kubwa sana sasa baada kiongozi wng kutoa cement 150 + 150 sehemu nyengine tutawaona wanaafiki matajiri sasaiv kujitokeza. Mungu akubariki Hon Magoti
@SuleimanKhdija
@SuleimanKhdija 28 күн бұрын
Mashallah Mungu akubariki ulipo towa hicho Mungu azidishe kingine Baada ya dhiki ni faraja Mungu atujaalie subra katik wakati mgumu huwezi juwa nilip litakacho fwata Allahul mustaan
@user-kz5en5tq2z
@user-kz5en5tq2z 7 күн бұрын
Mi ni mchungaji nawapongeza sana sheikh kwa unyenyekevu ambao umezaa mema hayo. Viongozi wa dini tujifunze mema, toka kwa mtu yoyote mwenye karama hizo. Mmbarikiwe sana Kisarawe na Dc wenu.
@ZuberJafar
@ZuberJafar Ай бұрын
Takibir takibir anaye mtaka DC aendre n moyo huuu weka laik nyingi kwenye komenti yangu alhu akibal mungu anasababu kufanya k2
@Official83640
@Official83640 Ай бұрын
Kuna watu walitafsir vibaya sana leo sura zao wataweka wapi Dc kawaumbua vibaya mno Alhamdulillah Allah afanye wepesi In'shaallah
@burhaanmamboleo3551
@burhaanmamboleo3551 26 күн бұрын
Na ni sura mbaya kweli...na hao hao uliowaita wametafsiri vibaya sauti zao ndy zimefanya huyo jamaa yako akajikosha.....huwezi sema mazingira yale ni mabovu kuliko mahala pa kulala nguruwe....sisi tumesoma shule mbovu vyoo vibovu tena za serikali hakuna aliezivamia usiku wala kuzifunga na hata leo shule za namna hiyo zipo...bado alichokifanya hakijafunika uvundo alioufanya ..
@epimackjohn461
@epimackjohn461 Ай бұрын
Mimi sijui kuongea kiingereza lakini kwa kitendo cha DC MAGOTI najaribu kukiongea nikisema "VERY GOOD DISRICT COMMISIONER MAGOTI " Kumbe ziara yake pale siku za nyuma Alisikitishwa na alichokiona akaona afanye jambo .
@salomewandya7257
@salomewandya7257 29 күн бұрын
😂😂😂😅
@chusseboywcb2808
@chusseboywcb2808 Ай бұрын
Mama Samia hili Jambo nilaheri sio mnasapiti mpira tu Jambo la mungu mnaacha nyuma mnasafirisha paka mashabiki naomba mlione nahili la mungu muweke akiba duniani na ahera💪💪💪💪💪
@GibsonNtamamilo
@GibsonNtamamilo Ай бұрын
Huyu Mkuu wa Wilaya nimemkubali mapema sana japo Mimi niko Kigoma. Big up DC Petro Magoti
@user-sv6zy3hc8o
@user-sv6zy3hc8o Ай бұрын
Kwaio ulijua ukiwa nae mkoa moja ndo utamjua vizuri au
@adambakari9276
@adambakari9276 Ай бұрын
Unajua kwann kafanya hvyo huyu kafungia madrasa na waislamu wamekuja juu hapo anajisafisha juz tena katangaza wauza mkaa na pikpik wakamatwe fain milion 1 na vijana wengi wa kisarawe ndo kaz yko
@EddahBure-te7ft
@EddahBure-te7ft Ай бұрын
Na mm nilitaka nishanga yaani kw Maneno yale yakuwaambia watoto waende shule wakasome wapate kuajiriwa kwa kweli ningeshangaa sana kuona uislam ungekaa kimya 😅​@@adambakari9276
@w4058
@w4058 28 күн бұрын
Tupatieni namba ya kuchangia
@hamidashaban1203
@hamidashaban1203 Ай бұрын
Allah akubariki DC magoti Allah azidi kukuongoza katika njia iliyonyooka na hiyo sadaka Yako iwe ni nyumba Yako yakuishi akhera.
@azzaalhabsi1505
@azzaalhabsi1505 29 күн бұрын
Tunashukuru sana mkuu wa wilaya kwa hicho ulicho toa.mungu akulipe kila lenye heri na wewe pamoja na familia yako awafanyie wepesi kwa kila jambo.ubarikiwe sana🙏
@user-uw5oh5yy5m
@user-uw5oh5yy5m Ай бұрын
Umeupiga mwingi sana DC kwa kuonesha mfano kwa viongozi wengine ,mungu akubariki sana!!Inshallah jengo litakamilika kwa uwezo wake ALLAH S.W .INNAH BAADA USRI YUSRA🎉🎉🎉
@ScopionScopion-zj9cd
@ScopionScopion-zj9cd Ай бұрын
mungu akubaliki sadaka hii itaish miaka na miaka hongera sana unafaa kuigwa
@LabiloWabikongo
@LabiloWabikongo Ай бұрын
mashaallah
@stevenmanase8162
@stevenmanase8162 Ай бұрын
Kesho tuu mnanza kuwaita makafili alaa kumbe kafili anaweza kuwa lulu hivi waisilamu wote leoa wanapompongeza
@MohamedAhmada-ie7ke
@MohamedAhmada-ie7ke Ай бұрын
​@@stevenmanase8162uyo kiongozi yupo apo kwa ajili ya wananchi
@ScopionScopion-zj9cd
@ScopionScopion-zj9cd Ай бұрын
kwaiy kwa sababu katoa sadaka Ndio ukafili wake umeisha ukafili haundolew Nasadak Na hata kafili akifanya jema anastahili kushukuliwa japokua ukafili wake upo pale pale mpaka asilim
@fettyrashid9042
@fettyrashid9042 29 күн бұрын
Allah akujaalie DC Magoti, Lakini pia Ustaadh alikuwa na hekima kwa clip ya kwanza majibu yalikuwa mazuri na pia alikwa msikivu sana Allah atamjaalia Ustaadh wetu❤
@saeedmagoda9651
@saeedmagoda9651 Ай бұрын
Mtangazaji Mungu akubariki kaka unajua kuriport hongera sana kwa taarifa yako
@MichaelKingazi-wm7xj
@MichaelKingazi-wm7xj 28 күн бұрын
Ni Dc mfanowa kuigwa, the best Dc.
@jeffmwambe7657
@jeffmwambe7657 28 күн бұрын
Asante sana DC huo ndo uongozi na utu maana rengo ni zuri ivyo tuna shukuru kwa saport yako.
@abuushakiraddausiy8666
@abuushakiraddausiy8666 Ай бұрын
Maaashaalllllah maashaallah maashaallah maashaallah maashaallah maashaallah maashaallah..........hongeraaa sannaaaa mungu akufanyie wepes....kwajuhudikuuubwaaa ulizofanya mkuu wa wiliyaa...
@HassanJaphari-rx7jy
@HassanJaphari-rx7jy Ай бұрын
MashaAllah. Hongera sana Dc Petro magoti kwa moyo wako mkunjufu nakuombea kwa Allah akusimamie katika majukumu yako ya kazi inshaAllah. Ameen
@stevenmanase8162
@stevenmanase8162 Ай бұрын
Watu walianza kumdhihaki mh petrol sisi wakristo hatuna baya kazi kazi kwenu sasa ona hata milioni16 mnashindwa kuchangishana mnaomba kwa rais mmekalia kuwa ita watu makafili tuu
@SwalahaHusseini
@SwalahaHusseini Ай бұрын
Maashaallah. Allah akupe zawasi ya kuingia katika uislamu na akufishe ukiwa katika imani sahihi .
@husseinkadawa2846
@husseinkadawa2846 Ай бұрын
Allahuakbar shekh Allah hatakuacha peke yako na malengo ulio weka yata timia tu kwa uwezo wake ndugu zangu waislam na wale wote tunao amini uwepo wa mungu tuchanga usidharau hela hata buku tuma kwa maana buku kwa watu milioni ni bilioni jambo linaenda nuia sadaka yako tuma huenda na wew ikawa ndo sababu ya kufunguliwa matatizo yako.
@shabanimbiaji
@shabanimbiaji 29 күн бұрын
SUBIRI NA WEWE MUDA SI MREFU ALLAH ATAKUPA MAKIPO YAKO,,,,SUBHANNALLAH,!!!!!
@allymwinyi970
@allymwinyi970 Ай бұрын
Ahsante sana Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. MUNGU akubariki. Tunakuombea MUNGU kwa wema ulioifanyia Madrasa hiyo. Tunaamini huku fanya lile zuio kwa utashi wako, ila kwa utekelezaji wa majukumu yako ya kuangalia maslahi ya baadae ya watoto hao. Tunamwomba MUNGU akuinue kupitia Raisi mwenye huruma kwa watu wa makundi, rangi na dini zote na na hata huruma kwa watu waakundi maalum. Mama yetu Dkt SAMIA SULUHU HASSAN. MUNGU anakupenda, wananchi wote wanakupenda. Kuna watu hawakuona Kam unaweza. Kwa Rehma na Huruma ya MUNGU amempa jicho Raisi wetu kukuteua na sisi tunaona. MUNGU akulinde na akulipe heri nyingi. Amin.
@SophiaAthumani-ri4lu
@SophiaAthumani-ri4lu Ай бұрын
Asante DC hakika umefanya vema kulichukulia jambo hilo kwa uzito,Sadaka yako ikawe kheri kwa watoto wetu.
@FghgRyy
@FghgRyy 2 күн бұрын
Takbiiiiiiiirrr ALLAHU AKBARU ALLAHU AKBARU ALLAHU AKBARU Walillah Llihamdu
@SalmaSamiry
@SalmaSamiry 29 күн бұрын
Mashaallah allahumma barik mwenyezi mungu awajaalie awape maisha marefu awaepushe na hasadi za walimwengu ameen ameen ameen yaa Allah 🙏
@user-ry8xf1no2s
@user-ry8xf1no2s Ай бұрын
Mashalahaa Alha akufanyiewepesi kwenye uongoziwako Mueshimiwa laisi wangu mpendwa Samia suluhuhasani ujawaikuniangusha una tupa viongozi makini sana awakulupuki na kupenda laisi wangu Samia
@maryamabdallah3140
@maryamabdallah3140 Ай бұрын
Siku zile nilijisikia vibaya lakini lengo lako lilikuwa jema kabisa...Mungu akutunze DC
@abdulmagido5444
@abdulmagido5444 Ай бұрын
Big up Doto Magoti Allah akuhifadhi
@ashiaabdul887
@ashiaabdul887 Ай бұрын
Masha Allah DC Allah akufanyie wepesi katika utendaji wako wa kazi .
@user-qw6wv4hf5c
@user-qw6wv4hf5c Ай бұрын
Mwenyezi mungu akujakie ds magoti Kwa moyo waupendo allah akulipe kheri ww na timu yako inshaallah
@chikujuma18
@chikujuma18 Ай бұрын
❤❤❤❤ mashallah mwenyezi mungu ampe maisha marefu na afya njema inshallah
@user-hy1bp7sp6z
@user-hy1bp7sp6z 17 күн бұрын
Mashaallah Allah haitupi Qura'an alishaahidi
@AbuujureyjKhaniy
@AbuujureyjKhaniy 28 күн бұрын
Usimjaji mtu kwa muonekan wake hakik Dc umekuwa mwema na umetend haki mungu akutangulie Shekh uwaz na ukweli wake mungu kamfungulia upande mwengine hakika ukweli ni baraka nyoote Allah akutangulie
@EmmaPonera
@EmmaPonera 9 күн бұрын
Hapo hoster itakuwa ya mfano Mungu atawaleta maajabu wafadhiri watamiminika maajabu yanakwenda kutendeka hapo
@abdulkaleemmbarak6670
@abdulkaleemmbarak6670 Ай бұрын
Mungu anatufundisha katika quran kua na subra katika kila Jambo. "Waeza chukia Jambo kumbe Lina kheir nawe na ukapenda Jambo kumbe Lina shari nawe.Awali wengi tuliona Shari kumbe mbeleni DC Magoti ameleta faida kwetu.Kaka Magoti mungu akupe umri mrefu na akufanyie wepesi katika maisha yako.Yaraby mpe furaha kama alivyo tufariji.
@abuuhafswa
@abuuhafswa Ай бұрын
ila kutoa siyo tatizo msinganganie sadaka mnazopewa tuu . angalia na dosari aliyoiweka kwenye dini . yapasa atuombe radhi
@EddahBure-te7ft
@EddahBure-te7ft Ай бұрын
​@@abuuhafswaDosari kubwa sana kwa kweli nilishangaa sana yale sio maneno yakuwaambia watoto, eti watoto wazuri mama samia anawapenda amewajengea shule nzuri zenye ubora ili muene mkasome muwe watumimishi kama hawa niliokuja nao so kungangania kulala hapa mahala hapafai, kwakwelu nilimshangaa sana ana maanisha nini kuwaambia vile watoto na kuwashushia lawama wazazi kua wamewatelekeza watoto wao wamewatupa kama hawana uchungu nao, yan imeniuma sana ivi unazani mm kama mzazi unakuta nimepeleka mtoto wangu hapo na naona video ya mazingira kama hio na maneno kama hayo alafu naambiwa mtoto anarudishwa nyumban unazani ntajiskiajee ?? Mwengine anaweza akagairi kabisa kumrudisha mtoto hapo atamtaftia sehem nyengine kbs na kuichukia dini, na kwa hao watoto walio rudishwa sizan kama watarudi kwa idadi sawa kama walivyoondoka wengi watabak makwao, mm ninachojua kama yeye kiongozi alipoona hilo tu angechukua maamuz ya kusaidia ujenzi watoto wakae mahal salam kam wanavyofanya makanisani ila kwasbb ameona ni waislam hawana wakuwasemea amejifanya yeye kama hajali kinachoendelea hapo wala hakina maana anawaambia watoto waende shule waende shule wakati watoto karibia wote hapo wanaenda shule na wanarud hapo kupata elimu ya dini ila yy akataka kufikisha ujumbe waonekane kana kwba waislam wamewarundika watoto hapo kama kuwakusanya ty kwa kwel. Iliniuma sana ile vd jinsi alivyoongea 😢
@user-ow7pl6tz2c
@user-ow7pl6tz2c Ай бұрын
nikweli alisema vibaya sana naamekosea sana waislam na hiyo sio lizaa yake itakua amepokea maagizo kutoka juu
@EddahBure-te7ft
@EddahBure-te7ft Ай бұрын
@@user-ow7pl6tz2c safi
@nzwibasson8479
@nzwibasson8479 Ай бұрын
Kuna ujinga unafanywa hapa. Kwa waisilamu wenye akili wameshaliona hili. Tuhimizane subira waisilamu. Tunakila sababu ya kulinda tunu ya uisilamu tuliyopewa na Allah. Waisilamu wote tunahitaji kuwa na jitihada ya kutafuta elimu ya dini haijalishi ni katika hali gani. Baadhi ya jamii elimu si kipaumbele chao.
@trophywilson7211
@trophywilson7211 27 күн бұрын
mmh Dini Bila Elimu Dunia Ni bure
@GdFf-ik2eo
@GdFf-ik2eo Ай бұрын
Ma sha allah Tunashukuru kwa kusema alhamdulilahi
@zainabwage4658
@zainabwage4658 Ай бұрын
Mungu akuzidishie
@zaituniNkupa
@zaituniNkupa 29 күн бұрын
Hongera mkuu wa wilaya umefanya jambo jema mno. Mungu akubaruki
@user-xv7mo8tw7c
@user-xv7mo8tw7c 29 күн бұрын
Masha Allah tunahtaj viongoz kama wey mungu akupe afya
@jamalnaheka
@jamalnaheka 28 күн бұрын
mh.magoti Allah akupe afya njema sana kazi nzuri.
@davidkawesa3594
@davidkawesa3594 26 күн бұрын
Mlikuwa mnamsema unafiki tu
@femidayahaya4882
@femidayahaya4882 Ай бұрын
Mheshimiwa Petro Magoti ubarikiwe sana. Mungu azidi kukufungulia na akujaalie afya njema.
@khalfanabeid5998
@khalfanabeid5998 Ай бұрын
Allah ampe maisha marefu na anyanyue uchumi wa nchi yetu kupitia hili. Amin.
@SalmanMughal-lq5lt
@SalmanMughal-lq5lt Ай бұрын
MashaAllah.mkuuu.wawilaya.Allah.akupemwisho.mwema.naimani.mola.wetu.anaweza
@fahamimiraji2338
@fahamimiraji2338 10 күн бұрын
Allah alifanyie wepesi inshaallah
@issarashid7707
@issarashid7707 Ай бұрын
Mungu akusimamie katika kazi zako ..Kwa hakika huo ndio mfano mzur
@hassanmussa7664
@hassanmussa7664 Ай бұрын
Anajikosha tena.....waache mihemko.....ukuu wa wilaya una mambo mengi ya kufanya....especially kusimamia sera
@isayakihongile4921
@isayakihongile4921 29 күн бұрын
Sera ni pamoja na watoto siyo barabara na maji tu
@WardaDonyi
@WardaDonyi Ай бұрын
Hakika DC Magoti were ni kiongozi bora sana. ALLAH akubariki ulipotoa
@SophiRamadhani
@SophiRamadhani 29 күн бұрын
Mama msikivu na mtendaji. Mwenyezi Mungu amuongoze kwa hili liwe jepesi Insha Allah
@EmmaPonera
@EmmaPonera 9 күн бұрын
Huyu shekh mnyenyekevu sana anaipenda sana dini yake
@mgongolwajoseph6901
@mgongolwajoseph6901 7 күн бұрын
Wsisilamu ni wanyenyekevu sana na mh magoti ni mnyenyekevu
@RahimaMct-ik8mr
@RahimaMct-ik8mr Ай бұрын
Allahu akbar DC mungu Allah akuhifadhi❤❤❤
@mwanajumaomahundumla6504
@mwanajumaomahundumla6504 Ай бұрын
Kitu cha maana sana na cha muhimu barikiwa DC maana niliwaza sana ni bora watoto au vijana kujua DIN kuliko kuwa mtaani au kuwa waharifu
@allyjumakukulo4972
@allyjumakukulo4972 Ай бұрын
Masha Allah allah akuongoze na akufanyie wepes upate neema ya uislam
@user-qn3cf2bg4u
@user-qn3cf2bg4u Ай бұрын
asantesana mkuuwa wilaya munguakujaliye kwaupendowako akuogezeumrimrefu akuhfadhiwewe na familiyayako
@mayaniphilipo9256
@mayaniphilipo9256 Ай бұрын
Hongera Sana Mheshimiwa Nimependa Ulivyorejea Mwanzo Ulinishangaza Kwa Lugha Zako Ila Hakuna Aliyekamilika Allah Atusamehe, Atuongoze Na Atufanyie Wepesi Kwenye Harakati Zetu BIG UP DC
@lukumanisharifu
@lukumanisharifu Ай бұрын
Safi sana DC huo ndio uungwana mungu akupe Imani sabiti
@MariamAlly-hk7io
@MariamAlly-hk7io 5 күн бұрын
Naada dhiki faraja Innamaal usri yusra Allahu akbar
@fatimahants1526
@fatimahants1526 Ай бұрын
Hongera mheshimiwa kwa moyo wa kutowa msaada
@BIGBOSS-hl3bu
@BIGBOSS-hl3bu Ай бұрын
Hongera sana MH magoti wewe ni mfano wa kuigwa ❤❤❤
@zenasalum2231
@zenasalum2231 Ай бұрын
Kama kuna mtu alienda kuchongea ili kumshusha huyo shekh sasa kampandisha Allahu Akbar
@ibnkhaldoun9694
@ibnkhaldoun9694 Ай бұрын
@ YAONEKANA WALITAKA KUWATIKISA WAISLAM,LAKINI KWA HEKIMA ZA MUFTI NA WELEDI WA VIONGOZI WAMELITIBU KI AINA YAKE.KONGOLE KWA WOTE WALIOELEWA TATIZO LIKO WAPI NA KULISHUGHULIKIA KWA NJIA BORA NA YA KISTARABU KULIKO VILE WAJINGA WALIVYOTAKA KULETA TAHARUKI.
@fedmiradaf3141
@fedmiradaf3141 Ай бұрын
Hakuna kumchongea ni kweli mazingira hayakuwa rafiki kwa watoto
@NaziaMudi
@NaziaMudi Ай бұрын
Wanafiqi saana awa baada yakuaambia watoto kwamba elim ya dini aina maana wasome wawe madaktari na viongozi wakubwa serikalini leo tena 😅😅😅😅😅😅😅😅😅😅😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢😢 innalillahi wainna ilayhi raj'uun allah awape ufaham wakuitambua hakki
@adilhabib8988
@adilhabib8988 27 күн бұрын
Maa shaa allah
@twayasinilukokelwa625
@twayasinilukokelwa625 28 күн бұрын
Tatumai huyu DC kama namkubuka ni ex-pugu secondary school ujamaa 1 anaelewa changamoto zinazowakumbaa wanafnz WA bweni,mi nimepata pale fm6
@eliezasamwel4891
@eliezasamwel4891 Ай бұрын
Baadhi ya watanzania ni watu wa ajabu sana Kuna wanao mpongeza leo Mh.DC lakini mwanzoni walimponda na kusema anataka kuleta udini sijui anamkosea Mungu hebu acheni kuwa na unafiki ivoo😮
@kivatirokitojo657
@kivatirokitojo657 29 күн бұрын
❤magoti umefanya kitu cha akili kubwa, nilikulaumu kidogo sio sana ila hapa ndio nimeona kua wewe ni kiongozi wewe ni kiongozi wa kutatua changamoto
@Anza_tz
@Anza_tz Ай бұрын
Hii inaitwa wajibisha alafu fundisha kwa hekima safi sana mkuu wa wilaya ni Jambo jema Sana la kuigwa na kufuatwa
@abbaskhamis3407
@abbaskhamis3407 Ай бұрын
anapuliza siyo tumeshamulelewa hana nia nzuri kabisa ana maneno machafu sana
@user-gc3ec9wx6z
@user-gc3ec9wx6z Ай бұрын
Ss kwa nn useme ivo
@dimosomkoba356
@dimosomkoba356 Ай бұрын
Huyo bwana inaonekana alimezeshwa vitu kwahiyo akaenda na maamuzi yake toka kule aliko toka wala mwanzo hakuenda kwa kutaka kujua na kutatua changamoto, kama unakumbuka akasema angewaweka lumande, sasa ameshajua aliteleza kwa maamuzi yake kwahiyo akaja na mbinu mbadala ya kujaribu kusawazisha!! ZINGATIA NENO KAMATI YA AMANI.
@user-xk7vy4gb6g
@user-xk7vy4gb6g Ай бұрын
​@@dimosomkoba356Naam
@RajabuMarinda
@RajabuMarinda 17 күн бұрын
bahat yake kajirud kwa njia iyo, angesababisha mpasuko wa udini hapo , alafu eti anasem mam kajenga shule analipa mishahara vizur , somen , yani anamaanisha kabisa kwa sis hatuna elimu, ya sekyula zaidi ya dini, jibu siyo kweli tumambiwa tutafute elimu hata kam ikiwa umbali wa China twende tukasome, watot wanapaswa kupewa elu ya kumjua Mungu wao na dunia yao, ili wawe viongoz bola wenye kumuogopa Muumba wao na uyo dc wakae nae kwa makin san ana uchembe flan ivi ndani yake
@alihabib2270
@alihabib2270 Ай бұрын
SAFI SANA DC MAGOTI, HAKIKA WEWE NI KIONGOZI MUADILIFU NA MUWAJIBIKAJI. MWENYEZI MUNGU AKULINDE NA AKUONGOZE KATIKA MAJIKUMU YAKO YA KUIJENGA JAMII.
@jamilmwinge3695
@jamilmwinge3695 26 күн бұрын
Mungu ni mwema wakati ukitimia kila kitu kitakamilika no jambo la heri.
@shabanimbiaji
@shabanimbiaji 29 күн бұрын
SUBIRI NA WEWE MUDA SI MREFU ALLAH ATAKUPA MAKIPO YAKO,,,,SUBHANNALLAH
@gmelectronics1997
@gmelectronics1997 22 күн бұрын
Taqabal Minah wa aminkum JAMIYAHTUL muslimunah..kila apangalo mungu hua lina kheri kubwa
@nasrasalumu7005
@nasrasalumu7005 28 күн бұрын
DC wewe ni mfano wakuigwa kabisa mungu akuongoze hivyo hivyo kiongozi wangu mkuu wa wilaya safi kabisa na shekhe mungu akulipe kwa hekma wewe muelewa na msikivu na wewe mungu akuongoze hivyo hivyo na akujaalie mwisho mwema inshallah
@mpefu_4936
@mpefu_4936 Ай бұрын
Watanzania tuache kuwa tunalaumu vituo atalishi juzi mlisema anapinga hiyo dini Leo mnasifia Ina maana hayo mazingira mliyapenda
@AbdillahMngoya-zj5or
@AbdillahMngoya-zj5or Күн бұрын
me nashangaa ile juzi shekh alikuwa peke yake kwenye kujibu maswali ila saiv DC kaleta cement mashekhe wamekuwa wengi duuuuh
@abuusuhayl7830
@abuusuhayl7830 Ай бұрын
Mashaa Allah..wale walio kejeli na kutoa maneno ya kifedhuli wamefedheheka wao
@hemedahmed3094
@hemedahmed3094 Ай бұрын
مَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَنْ يَعْمُرُوا مَسَاجِدَ اللَّهِ شَاهِدِينَ عَلَىٰ أَنْفُسِهِمْ بِالْكُفْرِ ۚ أُولَٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ وَفِي النَّارِ هُمْ خَالِدُونَ إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَاجِدَ اللَّهِ مَنْ آمَنَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَأَقَامَ الصَّلَاةَ وَآتَى الزَّكَاةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا اللَّهَ ۖ فَعَسَىٰ أُولَٰئِكَ أَنْ يَكُونُوا مِنَ الْمُهْتَدِينَ
@HABIBHASSAN-wf5mr
@HABIBHASSAN-wf5mr 20 күн бұрын
Mwanzo nilitaka kumlaumu MH Magoti LAKINI NI mtu MZURI sana
@yasirsaid8464
@yasirsaid8464 27 күн бұрын
MAA SHAA ALLAH ALLAH Awabariki wote
@user-hq5mo3dx7l
@user-hq5mo3dx7l Ай бұрын
Mungu akujalie sana kuona tatizo na kulitatua sio kuhukumu haijawahi tokea hili ungeeishia tu sehemu
@LovelyOmbreSky-pu4jt
@LovelyOmbreSky-pu4jt Ай бұрын
Asante sana mkuu huu ndiyo uwongozi mungu akulipe
@user-qn3cf2bg4u
@user-qn3cf2bg4u Ай бұрын
masha allah kajitahifi mkuwamkowa.naselekari yetuwendwa
@abdulkarimabdallah9536
@abdulkarimabdallah9536 29 күн бұрын
Allah akulinde ktk uongoz wko mku wa wilaya yakisarawe wewe nikiongoz wakuigwa ktk uongoz
@HashimSalim-qj7zn
@HashimSalim-qj7zn Ай бұрын
NATAMANI NIWE NA PESA HUU UJENZI NIUJENGE MM MAANA NDIO VITU VYA KUTANGULIZA HIVI MBELE YA ALLAH
@KAIPAAA3211
@KAIPAAA3211 Ай бұрын
Mungu akubariki mkuu wa willaya
@hanifamziray277
@hanifamziray277 Ай бұрын
Allah akubariki ujenzi utausha kwa uwezo wa wake
@HanifaOman-oo4pl
@HanifaOman-oo4pl Ай бұрын
Maashaallah. Allah akutoe kwenyegiza akuoete kwenyemwanga yaraby. Mjaalie huyo baba atukiewitowako. Amyn
@GdFf-ik2eo
@GdFf-ik2eo Ай бұрын
Mkuu tunashukuru Mungu akubariki
@fetychina3969
@fetychina3969 29 күн бұрын
Mungu ambariki amazing alipo pungunguza
@JumaJuma-i2g
@JumaJuma-i2g Ай бұрын
hapo safi hongera mkuu wa wilaya
@ancytarimo1103
@ancytarimo1103 Ай бұрын
Hakika huyu Shehe ni mnyenyekevu sana . Mwenyezi Mungu atakuinua kwa hilo.
@Shafikimanga7
@Shafikimanga7 Ай бұрын
Huu ndio uongozi. Unasimamia Sheria na kutoa usaidizi. Hongera DC Magoti
@SirahShabani
@SirahShabani 25 күн бұрын
Mashaallah ❤
@fatumasaid9882
@fatumasaid9882 Ай бұрын
Mashalaah mashalaaah peter magot kwa hilo umengusaaa
👨‍🔧📐
00:43
Kan Andrey
Рет қаралды 7 МЛН
Алексей Щербаков разнес ВДВшников
00:47
The Explainer | Jimi Wanjigi explains why 'Ruto must go'
28:27
Citizen TV Kenya
Рет қаралды 15 М.
DC MAGOTI APOKELEWA KISHUJAA KILUVYA/WATU WAFURIKA
3:36
JEHOVA JIRE TV TANZANIA
Рет қаралды 1 М.
👨‍🔧📐
00:43
Kan Andrey
Рет қаралды 7 МЛН