Рет қаралды 225
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Peter Serukamba amewataka Wazazi na walezi Mkoani Iringa kujitokeza Kwa wingi kuwapeleka watoto wenye umri wa mwaka 0 mpaka miaka 5 ili kupima hali ya udumavu na kutambua ni eneo lipi lina changamoto zaidi ili kukabiliana na kutokomeza changamoto hiyo
Mhe Serukamba ameyasemwa hayo leo Juni 10 ,2024 ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema ili kuhakikisha changamoto ya udumavu inamalizika, Mkoa umeanzisha kampeni ya siku nne kwa lengo la kutathimini na kujua maeneo yanayokabiliwa zaidi na changamoto ya udumavu ili nguvu ya ziada iwekezwe kuweza kuukabili udumavu.
Kwa hatua nyingine Mhe Serukamba ameeleza kuwa mpaka sasa kiwango cha udumavu Mkoani Iringa ni kikubwa huku ikishika namba moja nchini kwa asilimia 56.9
kwa sensa iliyofanyikia 2022 ambapo kati ya Watoto 56 - 57 kati ya 100 wana udumavu.
Hata hivyo Mhe Serukamba ameongezea kwa kusema kuwa Serikali ya Mkoa wa Iringa imeagiza kila Halmashauri kutenga kiasi cha shilingi elfu 1000 kwa kila mtoto mashuleni lengo likiwa ni kutokomeza udumavu.