Рет қаралды 271
Magonjwa ya kuku ni maradhi yanayoathiri afya ya kuku na kusumbua wafugaji wengi wa kuku, hasa wafugaji wadogowadogo na kupelekea hasara kubwa kwa wafugaji. Kuku kama walivyo viumbehai wengine, hupatwa na magonjwa mbalimbali hivyo basi ni jukumu la kila mfugaji kutatua tatizo linapotokea ambalo hujumuisha afya ya kuku wake.
Video hii inaelezea baadhi ya magonjwa ya kuku yanayosababishwa na virusi, dalili za magonjwa hayo na baadhi ya njia za kupunguza au kujilinda na magonjwa hayo