HOTUBA YA RAIS DKT. MAGUFULI HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI MRADI WA UMEME WA RUFIJI

  Рет қаралды 16,133

Ikulu Tanzania

Ikulu Tanzania

5 жыл бұрын

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri Mhe. Dkt. Mustafa Madbouly tarehe 12 Desemba, 2018 wameshuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji utakaotekelezwa kwa muda wa miezi 42 kuanzia sasa.
Mkataba huo umetiwa saini kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka na wawakilishi wa kampuni za ujenzi kutoka Misri ambao ni Mwenyekiti wa kampuni ya Arab Contractors Bw. Mohamed Mohsen Salaheldin na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Elsewedy Bw. Ahmed Sadek Elsewedy.
Hafla ya utiaji saini mkataba huo imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Bashiru Ally Kakurwa, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi, Mawaziri na Naibu Mawaziri wa Tanzania na Misri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa, Wabunge, viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa Dini, viongozi wa vyama vya siasa, Wakuu wa Wilaya na viongozi wa taasisi mbalimbali za Serikali.
Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo, Mhe. Rais Magufuli amesema ujenzi wa mradi huo utakaozalisha megawatts 2,115 za umeme utagharimu shilingi Trilioni 6.558, fedha ambazo zinatolewa na Serikali ya Tanzania na katika kipindi cha miaka zaidi ya 60 ya uhai wake mradi huu utaiwezesha Tanzania kupata umeme mwingi, wa uhakika na wa gharama nafuu kwa ajili ya matumizi ya majumbani na biashara ikiwemo viwanda.
“Kwa hivi sasa nchi yetu ina megawatts 1,560 tu za umeme, mradi huu pekee yake utazalisha megawatts 2,115. Uzuri ni kwamba umeme unaozalishwa kwa kutumia maji ni nafuu sana (shilingi 36/- tu kwa uniti moja) ikilinganishwa na umeme wa vyanzo vingine (mfano umeme wa mafuta unaofikia shilingi 446/- kwa uniti moja)” ametoa mfano Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa mradi huu unatarajiwa kuleta manufaa mengine kama vile kuimarisha uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya mradi, mifugo ikiwemo wanyamapori kupata maji ya kutosha, kilimo cha umwagiliaji, kuvutia utalii, uvuvi na kukuza ujenzi wa viwanda, tofauti na madai ya baadhi ya watu wanaodai kuwa utaharibu mazingira.
“Eneo lote la mradi huu ni sawa na asilimia 1.8 hadi 2 tu ya pori zima la hifadhi ya akiba ya Selous, kuwepo kwa mradi huu kutasaidia watu wengi kupika kwa kutumia umeme badala ya kuni na mkaa ambao takwimu zinaonesha umekuwa ukisababisha kukatwa kwa hekta 583 za miti kila siku. Tuna imani kubwa ukikamilika wananchi wengi wataachana na matumizi ya kuni na mkaa na badala yake kutumia umeme utakaopatikana kwa bei nafuu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono juhudi za Serikali kutekeleza mradi huu na amewataka wanaotumiwa na mabeberu kupiga juhudi hizi waache kwa kuwa mradi huu unatekelezwa kwa manufaa ya Watanzania wote bila kubagua itikadi ya siasa, dini ama kabila la mtu.
Pia amewashukuru viongozi wa Dini waliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo na kuomba dua njema kwa mradi na Taifa, pamoja na viongozi wengine wote kwa kutambua umuhimu wa mradi huu mkubwa.
Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Waziri Mkuu wa Misri Mhe. Dkt. Mustafa Madbouly kwa ujio wake hapa nchini na amemuomba amfikishie salama za shukrani kwa Rais wa Misri Mhe. Abdel Fattah el-Sisi kwa uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Misri na ameahidi kuuendeleza na kuukuza uhusiano huu.
Waziri Mkuu wa Misri Mhe. Dkt. Mustafa Madbouly amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano mzuri wa Tanzania na Misri ulioasisiwa na viongozi wa Mataifa haya Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Gamal Abdel Nasser, na ameahidi kuwa pamoja na kutekeleza mradi huu Misri itaendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mengine ya biashara na uwekezaji pamoja na kuunga mkono juhudi mbalimbali za kuwaletea Watanzania maendeleo.
Nao viongozi mbalimbali waliopata fursa ya kutoa salamu katika tukio hilo wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa jitihada kubwa anazozifanya katika uongozi wake ikiwemo kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, kuhakikisha nchi ina amani, kulinda hadhi ya nchi na kuhakikisha nchi inajenga misingi ya kujitegemea na wameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi hizo kwa manufaa ya Taifa.

Пікірлер: 49
@victustemba
@victustemba 5 жыл бұрын
Uwaga nikimsikiliza Raisi wangu, moyo wangu unayoyoma kwa furaha,Mungu akubariki sana my Hero. Kuna siku watanzania wote tutakuelewa.
@christianremnantsda5304
@christianremnantsda5304 5 жыл бұрын
Vzr sana rais wangu wa nguvu, MUNGU akuinue zaidi,
@gumzootv425
@gumzootv425 5 жыл бұрын
Duh, sir Magu ukimtizama macho yake anaonekana halali kwa ajili ya waTanzania safi sana hiyo ndo nguvu ya kura yangu ya mwaka 2015
@valeryluoga5948
@valeryluoga5948 4 жыл бұрын
Tanzania itajengwa na sisi wenyewe, hongera kwa watanzania na serikali yetu kwa maamuzi muhimu
@samuelmtasha9272
@samuelmtasha9272 5 жыл бұрын
Mungu bariki Tanzania 🇹🇿 Mungu mbariki Rais wetu Magufuli, katika jina la Yesu AMEN 🙏
@dicksonmatulile1523
@dicksonmatulile1523 3 жыл бұрын
A man of the people
@benjaminpallangyo4545
@benjaminpallangyo4545 5 жыл бұрын
one of the strongest speech. viva JPM
@mateikihoi8125
@mateikihoi8125 5 жыл бұрын
Watashindana hawatashinda Magufuli ndiye rais tuliyekuwa tunakuhitaji kwa wakati huu
@sillasmartin108
@sillasmartin108 5 жыл бұрын
nakupenda rais wangu
@mramtakujasambaaguy6681
@mramtakujasambaaguy6681 5 жыл бұрын
appreciation to you presidaa
@gospelsmusic2555
@gospelsmusic2555 5 жыл бұрын
God bless you my President🙏
@zankuipujini3973
@zankuipujini3973 5 жыл бұрын
Muheshimiwa Raisi Dr. Jon Pombe Magufuli, hakika umefanya lamaana sana, kiukweli sasa tunaelekea kwenye Industrial Revolution sababu ili uweze ku invest kwenye viwanda lazima miundombinu iwe mizuri. Na miundo mbinu yenywe ni uwepo wa umeme wakutosha. Hongera sana
@mateikihoi8125
@mateikihoi8125 5 жыл бұрын
Congratulations Mr prez dar
@awadhirajabu7754
@awadhirajabu7754 5 жыл бұрын
Ila Wasiwasi Wangu Kama Mtanzania Upo Kwa Wanyama Mana Apo Kutakua Na Watu Wengi Vipi Wanyama Wataishi Kwa Fulaa Kama Zamani Hau Watapata Tabu Sana Kwa Kuwindwa Mana Kutakua Na Muingiliano Wawatu Wengi Je Kiongozi Wetu Ukiondoka Madalakani Hao Wanyama Waishi Salama
@leonardmaganja9535
@leonardmaganja9535 5 жыл бұрын
Jamani ninakoshwa sana na Rais wangu mpendwa na mtenda miujiza Mungu akimtumia kutenda mema kwa Taifa letu. Ongera sana Rais MAGUFULI
@hasnuumakame9219
@hasnuumakame9219 5 жыл бұрын
Hongera sana Mr President, mimi niko Egypt kimasomo ila nashuhudia ukweli unaousema hawa jamaa wa Misri katika fani hiyo ujenzi (uhandisi) ni watu dhamana na wapigaji kazi wa uhakika, hawana ubabaishaji na wahandisi wa viwango vya kimataifa
@awadhirajabu7754
@awadhirajabu7754 5 жыл бұрын
Uyu Ndo Kiongozi Wawatu Wote Waisio Tanzania Anaipenda Nchi Na Watu Wake Achagui Mtu Wa Kumpa Sifa Yeye Mtu Yoyote Anaestairi Sifa Atamsfu Awezi Kumpa Sifa Asiestairi Sifa
@benjjlifetechnologie435
@benjjlifetechnologie435 4 жыл бұрын
like dat
@gabrielmathew740
@gabrielmathew740 3 жыл бұрын
Nailudia 2021
@swediharuna24
@swediharuna24 5 жыл бұрын
Mega watt 2000 good jpm
@hafidhusulemani8277
@hafidhusulemani8277 5 жыл бұрын
Huwa najihisi nikohuru pindininapomsikia huyukidume anavyozungumza napenda anavyojiamini anatufanya kujiamini watanzaniawote kiujumla ongelasana muheshimiwa rahisi wangu mpenda Jon pombe magufuri
@amiryhamza1984
@amiryhamza1984 3 жыл бұрын
mzee hakika wewe nimzarendo namba1 tanzania
@shabanimwema7334
@shabanimwema7334 5 жыл бұрын
Daaa wanyama wana umuhimu bt kipi bora mama anejifungua hsptl hauna umeme au wanyama plus ma mbuga mengi
@aridiyahya8049
@aridiyahya8049 5 жыл бұрын
Kuanzia 2013 nilijua kuwa wewe ni Raisi wangu. Wacha tu upondwe maana hata Yesu alirushiwa mawe.
@nyanda427
@nyanda427 5 жыл бұрын
🇹🇿🇹🇿🇹🇿
@michaelmathew8309
@michaelmathew8309 5 жыл бұрын
JPM mfano kwa kila mtanzania
@shindanopapaya2084
@shindanopapaya2084 5 жыл бұрын
shikamoo JPM na awamu ya 5 kwa ujumla
@nkuba_tz258
@nkuba_tz258 5 жыл бұрын
vizur PREZDAA
@mnzavachris5423
@mnzavachris5423 5 жыл бұрын
hmm
@shijamoshida496
@shijamoshida496 5 жыл бұрын
100%
@sudiyahya9276
@sudiyahya9276 5 жыл бұрын
Wewe unae taka chokochoko zauraisi, nakuuliza je? Unahakili nauthubutu kama wa raisi wetu ,SIR DR JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI?
@f.a6043
@f.a6043 5 жыл бұрын
🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
@amapiaanocityintz6454
@amapiaanocityintz6454 3 жыл бұрын
JPM furaha yangu ni kukuona upo serious
@shabanmkenga3154
@shabanmkenga3154 5 жыл бұрын
🇹🇿
@paulshamba1746
@paulshamba1746 5 жыл бұрын
mimi sioni kama kuna umuhimu wa kufanya uchaguz 2020 aendelee tu jpm
@nobertbamugimba9204
@nobertbamugimba9204 5 жыл бұрын
Rais JPM ni wa pekee,nakupenda Rais wangu
@josephmlela9757
@josephmlela9757 5 жыл бұрын
Tunamkarbisha saaana tz
@mnzavachris5423
@mnzavachris5423 5 жыл бұрын
nani?!
@natafutamatatizo4382
@natafutamatatizo4382 5 жыл бұрын
MAGUFULI USITUDANGANYE, NANI HAJUI KAMA PESA WAMEKUKOPESHA PESA WA EGYPTIAN, NA HAO HAO UMEWAPA CONTRACT, YAANI WAPATE KAZI WAO NAFAIDA IWE YAO. HALAFU TUKUUNGE MKONA KWA MADENI WAKATI WEWE TUTAKULIOA MPAKA KUFA. UNATUDHULUMU POMBE NA WACHA KUTUDANGANYA.!!
@yasinkihupi3211
@yasinkihupi3211 5 жыл бұрын
Una akili lakini au huwa mnajiskiaga ku comment tu???
@natafutamatatizo4382
@natafutamatatizo4382 5 жыл бұрын
@@yasinkihupi3211 NILIJUA LITATOKEA SHOGA KUNIJIBU.😘😘😘 I LOVE YADIN
@evancempotwa6360
@evancempotwa6360 5 жыл бұрын
Amekopa zinapolipwa si zinalipwa na watanzania!?
@sirfabiano767
@sirfabiano767 5 жыл бұрын
Una ushaidi wa kutosha, ila sikulaamu xana make uwezo wako wa kufikili ndo umeishia hapo
@hamisisonga4357
@hamisisonga4357 5 жыл бұрын
Ali Simai ohoooo unayumba shoga wewe
RAIS DKT. SAMIA AKIWAAPISHA VIONGOZI WATEULE IKULU DAR ES SALAAM
59:08
A little girl was shy at her first ballet lesson #shorts
00:35
Fabiosa Animated
Рет қаралды 6 МЛН
Llegó al techo 😱
00:37
Juan De Dios Pantoja
Рет қаралды 50 МЛН
Red❤️+Green💚=
00:38
ISSEI / いっせい
Рет қаралды 79 МЛН
Hotuba ya uzinduzi wa Bunge la 11 dodoma Nov 20,2015
1:38:02
Ikulu Tanzania
Рет қаралды 146 М.
#LIVE: RAIS DKT. MAGUFULI AKIZUNGUMZA NA  WANANCHI MBALIMBALI .
24:52
Ikulu Tanzania
Рет қаралды 18 М.
RAIS MAGUFULI ALIVYOKWENDA BENKI KUU BILA KUWATAARIFU
8:03
Millard Ayo
Рет қаралды 1,9 МЛН
MAGUFULI:NILIPOTAKA KUJENGA TRENI YA UMEME INAWEZEKANA  HAWAKUNIAMINI''
7:39
RAIS DKT. SAMIA AKISHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA
1:07:10
Ikulu Tanzania
Рет қаралды 8 М.
A little girl was shy at her first ballet lesson #shorts
00:35
Fabiosa Animated
Рет қаралды 6 МЛН