Рет қаралды 2,859
Kumekuwepo na njia mbalimbali za kutibu kuku, zikiwemo za asili na zisizokuwa za asili. Moja wapo ya tiba rahisi ya asili kwa kuku ni kwa kutumia shubiri mwitu maarufu kama Aloe Vera. Mmea ambao umekuwa ukisifika kwa kutibu magonjwa mbalimbali kwa binadamu, wanyama na ndege.Tafiti zilizofanyika kwa kutmia mmea huu kutibu ugonjwa wa Coccidiosis ambao unamadhara makubwa kwa wafugaji wa kuku zinaonesha kuwa mti huu unaweza kutumiwa kama mbadala wa dawa za viwandani. Maji maji ya mmea huu yana uwezo wa kutibu magonjwa na kuponyesha majeraha yanayotokana na maambukizi ya magonjwa pamoja na kupandisha kinga ya kuku kwa asilimia kubwa dhidi ya maonjwa mbalimbali. Tazama video hii kuona ni magonjwa gani yanatibiwa na aloe vera na matumizi sahihi ya mmea huu.