CHALAMILA AWA MBOGO SAKATA LA WAFANYABIASHARA KARIAKOO, ATAKA MAJINA 891 YAFUTWE

  Рет қаралды 6,470

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

27 күн бұрын

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Albert Chalamila ameagiza kuondolewa majina 891 ya wafanyabiashara yaliyowekwa kwenye mtandao wa Shirika la Masoko Kariakoo mpaka pale vyombo vya dola vitakapojiridhisha na majina hayo.
Hatua hiyo inakuja baada ya wafanyabiashara zaidi ya 800 waliokuwepo sokoni hapo kabla ya soko kuungua Julai 2021 kuandamana jana Alhamisi, Julai 11, 2024 kwenda Ofisi za CCM Lumumba kupinga kutorejeshwa.
Katika orodha hiyo, wafanyabiashara 891 kati ya 1,861 ndio walioelezwa kuwa na vigezo vya kurejea. Uamuzi huo uliwafanya kujitokeza katika viwanja vya Mnazi Moja kuhakikiwa na baada ya kutoridhishwa ndio wakaandamana.
Chalamila ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Julai 12, 2024, alipozungima na uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo katika Ofisi ya Shirika la Masoko Magogoni.

Пікірлер: 14
@binsherbal6089
@binsherbal6089 21 күн бұрын
Hebu nyoosha maneno, Rais amelipa!!!??? Hapo hapo unasema ni Kodi zetu walalahoi!!!??? Amelipa Rais au tumelipa sisi? Hii kauli inakera sana, Kila kitu Rais kafanya Rais kafanya Rais anatoa wapi pesa? Mbona mambo yakiharibika hamsemi kama Rais kaharibu? Kila kitu ni Uchawa tu siku hizi.
@hamidabarraball3162
@hamidabarraball3162 21 күн бұрын
Yaani kila kiongozi akitoa hutuba lazima amtaje rais zaidi ya mara kumi, inatia aibu sana, tunaona nchi za wenzetu raisi hasifiwi kiasi hicho
@hudhaifamsafiri8731
@hudhaifamsafiri8731 21 күн бұрын
Kwan wakuu wetu hawawezi kufanya kazi bila kumuusisha Raisi
@user-hi8le2vb7z
@user-hi8le2vb7z 21 күн бұрын
leo ajastua leo😊
@gmdigitostore8550
@gmdigitostore8550 21 күн бұрын
Hapo safi. Kibano hicho.
@GeorgeSikazwe-mm7nn
@GeorgeSikazwe-mm7nn 21 күн бұрын
😂 hii nchi bhn..serikali nd inalipa ww
@evamacha4861
@evamacha4861 21 күн бұрын
Mkuu wa mkoa nadhani unakumbuka soko la.mbagala zakgiem ulituuza sana kwa kutudanganya kuwa ukiona kuna mafisadi lakini ulitudanganya soko la zakhiem uliweka wafanyabiashara wapya badala ya wale waliopisha soko kujengwa.ulifanya dhambi kubwa sana bado tunalia machozi ya damu na mungu pekee ndio natafuta machozi yetu.
@maimunaathumani9121
@maimunaathumani9121 21 күн бұрын
Kweli mkuu wengine pale kariakoo walisishana familia zima sisi twende wapi
@mbwanakiting7180
@mbwanakiting7180 21 күн бұрын
Tuliambiwa pesa katoa maamaa na serikalli sasa shirika limeweka mtaji gani?
@faustinluambano2958
@faustinluambano2958 21 күн бұрын
Huyu naye.
@user-tn7ic2ky3i
@user-tn7ic2ky3i 21 күн бұрын
Aneye lipa ni Samiya ao ni serikali acha uchawa
@user-xk7vy4gb6g
@user-xk7vy4gb6g 21 күн бұрын
Soko la ccm hilo
@hebronmwamwaja7660
@hebronmwamwaja7660 21 күн бұрын
Siyo ameripa tumeripa acheni ayo mambo ya uchawa tumeripa
Best KFC Homemade For My Son #cooking #shorts
00:58
BANKII
Рет қаралды 73 МЛН
SIRI YA MANABII KUMILIKI UTAJIRI IMEFICHUKA
8:19
Wasafi Media
Рет қаралды 17 М.