Рет қаралды 246,383
Kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale ametofautiana hadharani na mwenyekiti wa baraza la magavana Isaac Rutto alipomtaka awajibike kuhusiana na hela ambazo kaunti yake ya Bomet ilipewa kabla ya kudai hela zaidi katika kampeni ya pesa mashinani, mbele ya Naibu wa Rais William Ruto mjini Narok. Hii ni mara ya pili kwa naibu wa rais kupata kuhudhuria mkutano wenye viongozi wa mrengo wa jubilee wanaotofautiana naye wanaopigia debe uchaguzi wa maoni. Pia naibu wa rais amedai kuwa kampeni za pesa mashinani na 'Okoa Kenya' hazina nia ya kuwaokoa wakenya ila ni za kupigia debe kiongozi wa Cord Raila Odinga.