SABABU ZA MISUGUANO KATIKA KARISMATIKI KATOLIKI | KATEKESI MTANDAONI - EPSODE 5

  Рет қаралды 4,480

Kwaya ya Familia Takatifu St. Joseph Cathedral DSM

Kwaya ya Familia Takatifu St. Joseph Cathedral DSM

4 жыл бұрын

Karismatiki Katoliki ni mwamko mmojawapo katika Kanisa Katoliki ambao unakazia suala la uwazi zaidi kwa Uwepo na Nguvu za Roho Mtakatifu na Karama zake; mabadiliko ya kiroho ya mtu binafsi na Kanisa zima kwa ujumla.
KUZALIWA KWA UPYAISHO WA KIKARISMATIKI KATOLIKI
Mara nyingi watu wananiuliza kama nilishawahi kuchoka kuhadithia kilichotokea katika Wikiendi ya Dukweni. Kamwe sijawahi kuchoka, kwa sababu ni hadithi ya kimapenzi - hadithi ya jibu la kipekee na la neema la Mungu kwa maombi ya watu fulani wa kawaida sana.
Katika kipindi cha masika cha mwaka 1966, maprofesa wawili wa chuo cha Dukweni walikuwa WAKIOMBA, WAKITAFUTA NA KUBISHA. Walikuwa wamejiahidi kuomba kila siku kwa miminiko kuu la Roho Mtakatifu katika maisha yao wakitumia Sikwensia ya Pentekoste. Katikati ya kipindi hiki cha maombi, marafiki zao kadhaa waliwapa vitabu viwili: Msalaba na Upanga (The Cross and the Switchblade) na Wananena kwa Lugha Nyingine (They Speak With Other Tongues). Vitabu vyote vinaelezea uzoefu wa Ubatizo katika Roho Mtakatifu. Hawa maprofesa wakatambua kuwa Ubatizo katika Roho Mtakatifu ndio hasa waliokuwa wakiutafuta.
Januari 1967, Wakatoliki wanne kutoka Dukweni walihudhuria kwa mara ya kwanza mkutano wa sala wa Kikarismatiki wa mchanganyiko wa madhehebu - mkutano wa Chapel Hill - nyumbani kwa bi Flo Dodge, Mpresbiteri aliyejazwa Roho Mtakatifu. Jambo la kuvutia zaidi, miezi michache kabla Wakatoliki hawa hawajaja, Bwana Alimuongoza bi Flo kusoma Isaya 48 ambapo Anatangaza kwamba Yu karibu kutenda ‘jambo jipya’. Kwa hakika, Mungu Alikuwa Yu karibu kutenda jambo jipya miongoni mwa Wakatoliki kama matokeo ya mkutano wa sala. Wale watu kutoka Dukweni walivutiwa na kile walichokishuhudia kule. Tarehe 20 Januari, wawili miongoni mwao wakarudi tena. Wakapokea Ubatizo katika Roho Mtakatifu na kuanza kudhihirisha vipawa vya kikarismatiki. Wakarudi nyumbani kuomba na wale wengine wawili ambao hawakuhudhuria usiku ule.
Kipindi hiki nilikuwa ni mwanachama wa kikundi cha kusoma Maandiko cha Chi Rho kilichokuwa kikikutana pale chuoni Dukweni. Wawili kati ya hawa maprofesa walikuwa ni wasimamizi wa kikundi hiki, na ingawa hawakutuambia moja kwa moja juu ya uzoefu wao wa Kikarismatiki, wale waliowajua vizuri walitambua wana mwako wa furaha mpya. Tulikuwa tunapanga mafungo yetu ya Februari na maprofesa wakapendekeza mada mpya: “Roho Mtakatifu.” Katika maandalizi kwa ajili ya mafungo, walituambia tuombe kwa mategemeo/matarajio, tusome kitabu cha Msalaba na Upanga, na tusome sura nne za kwanza za kitabu cha Matendo ya Mitume.
VENI CREATOR SPIRITUS, “NJOO ROHO MUUMBAJI”
Siku chache kabla ya mafungo, nilipiga magoti chumbani kwangu na kuomba,”Bwana, naamini nimekwisha kumpokea Roho Wako katika Ubatizo na Kipaimara. Lakini kama inawezekana kwa Roho Wako kutenda kazi zaidi maishani mwangu kuliko ambavyo amekuwa hadi sasa, NAMHITAJI!” Jibu kuu na la ajabu la maombi yangu lilikuwa li karibu kuja.
Tarehe 17 Februari watu 25 tuliondoka chuoni kwenda katika nyumba ya mafungo ya The Ark and The Dove (Safina na Njiwa) iliyokuwa nje kidogo ya jiji. Tulipokuwa tukikusanyika katika kila kipindi, maprofesa wetu walituambia tuimbe kama maombi tenzi ya zamani Veni Creator Spiritus, “Njoo Roho Muumbaji”. Ijumaa usiku kulikuwa na tafakari kwa Mama Maria. Kisha tukawa na Huduma ya Kitubio. Katika Injili ya Yohana tulisoma kwamba Roho Mtakatifu Atakapokuja Ataushuhudia Ulimwengu kwa habari ya dhambi. Hicho ndicho kilichotokea miongoni mwetu wakati tukitubu katika Sakramenti ya Upatanisho.
Jumamosi mshiriki mmoja wa kikundi cha sala cha Chapel Hill alikuja kuzungumza juu ya Matendo ya Mitume sura ya pili. Tulichoambiwa ni kwamba alikuwa ni rafiki wa Kiprotestanti wa maprofesa wetu. Ingawa uwasilishaji wake ulikuwa ni rahisi, ulijawa na nguvu za kiroho. Alizungumzia kujisalimisha kwa Yesu kama Bwana na Mkuu. Alimwelezea Roho Mtakatifu kama Nafsi Anayemtia nguvu kila siku. Huyu alikuwa mtu ambaye kwa hakika alionekana kumjua Yesu kwa undani na binafsi! Alijua nguvu za Roho Mtakatifu kama Mitume walivyojua. Nilijua nilitaka kile ambacho mtu huyu alikuwa nacho na niliandika katika notisi zangu, “Yesu, Uwe halisi kwangu.”
Katika majadiliano baada ya mafundisho yake, David Mangan akapendekeza kwamba tufunge mafungo yetu kwa kupyaisha Kipaimara chetu…kwamba sisi, kama vijana wakubwa, tuseme ‘ndiyo’ binafsi kwa Roho Mtakatifu. Niliunganisha mkono wangu na wake na kusema, “hata kama hakuna mwingine anayetaka kufanya hivi, ninafanya.” Kisha nilichana karatasi na kuandika, “Nataka muujiza!”, na kuibandika katika ubao wa matangazo.
SOMA ZAIDI
www.jamiiforums.com/threads/n...

Пікірлер: 14
@paulhando6286
@paulhando6286 Жыл бұрын
Fanya reference kongamano LA Pentecost Dodoma lililoshirikisha wachungaji wa kilokole kama in sahihi kupoteza waamini kwa wao kuwa njia panda
@masseepesa7539
@masseepesa7539 2 жыл бұрын
Asante sana Baba, na ubarikiwe sana. Waumini wanachanganywa sana na hii Karismatiki, ambayo hata mafundisho yako yanadidimiza na kuleta confusion juu ya mafundisho ya Masakramenti
@EmanuelMakalla-wu1zu
@EmanuelMakalla-wu1zu 21 күн бұрын
Yeyote anayepinga karismatiki akiwa kijana jua ni muasherati na akiwa mzee jua huyo mchawi sana
@deogratiasrwechungura3451
@deogratiasrwechungura3451 2 жыл бұрын
Asante Baba kwa ufafanuzi mzuri wa kueleweka Ila ushauri wangu ni nyinyi viongozi wetu wenye thamana katika hili kuwa karibu sana na vikundi hivi maana inapokosekena maeneo mengi wahusika wanajikita katika karismatiki ya wenzetu na kupoteza muelekeo wa Kikatoliki na hivyo kuweka alam za kujiuliza nyingi
@theogeorge3773
@theogeorge3773 22 сағат бұрын
Mungu asaidie kila mmoja afanye lile limpendezao Mungu
@eternalword1843
@eternalword1843 4 жыл бұрын
Safi sana. Asante kwa ufafanuzi mzuri.
@josephphares5334
@josephphares5334 4 жыл бұрын
Asante Baba kwa ufafanuzi huu mzuri
@Suzy-p3b
@Suzy-p3b 14 сағат бұрын
Thank u
@user-gd4eg4dp5m
@user-gd4eg4dp5m
👏
@felisterligwa
@felisterligwa 4 жыл бұрын
Amina
@damianlucas8502
@damianlucas8502 3 жыл бұрын
Hongera fr
@meshackmtewele718
@meshackmtewele718 2 жыл бұрын
🙏🙏
@simonnjovu586
@simonnjovu586 Жыл бұрын
Kongamano la Dodoma halikuwa na tatizo kubwa kwa jinsi inavyoelezwa na wapinga Karismatiki Katoliki. Kama alivyosema padre hapa, ni kutokuelewa tu.
CHANZO NA UHALALI WA KARISMATIKI KATIKA KANISA KATOLIKI - KATEKESI MTANDAONI | EPSODE 3
15:06
Kwaya ya Familia Takatifu St. Joseph Cathedral DSM
Рет қаралды 11 М.
KUNENA KWA LUGHA NI NINI? | KATEKESI MTANDAONI | EPSODE 06
6:04
Kwaya ya Familia Takatifu St. Joseph Cathedral DSM
Рет қаралды 2 М.
Alex hid in the closet #shorts
00:14
Mihdens
Рет қаралды 18 МЛН
Ouch.. 🤕
00:30
Celine & Michiel
Рет қаралды 26 МЛН
Schoolboy - Часть 2
00:12
⚡️КАН АНДРЕЙ⚡️
Рет қаралды 5 МЛН
BABA ASKOFU NA KARISMATIKI KATOLIKI JIMBO LA NJOMBE
7:43
Mahubiri Karismatiki Katoliki Njombe Tv
Рет қаралды 8 М.
HISTORIA YA MONSINYORI MBIKU KUZALIWA MPAKA MAUTI/ALIKUWA MUISLAMU
8:37
Baba  Askofu Mkuu Renatus Nkwande na Askofu Eusebius Nzigilwa Wakiwasili  Parokia ya Kiseke.
2:08
Archdiocese of Mwanza - Jimbo Kuu la Mwanza
Рет қаралды 2,7 М.
80 Year Olds Share Advice for Younger Self
12:22
Sprouht
Рет қаралды 1,7 МЛН
Kwaya ya Mt. Gaspar del Bufalo - Twaimba sifa za Bwana
4:32
KMG TEGETA
Рет қаралды 399
Alex hid in the closet #shorts
00:14
Mihdens
Рет қаралды 18 МЛН