Рет қаралды 202
Kumheshimu au kuwa na heshima kwa mweza wako si UTUMWA au ishara ya kunyanyasika kama wengi tunavyodhani.
Kwa kutambua umuhimu wa heshima, katika kujenga mahusiano bora yasiyo na migogoro isiyo ya lazima , mhusika anastahili kufanya tendo hili kwa moyo wake wote huku akimwomba Mungu kibali kwa mwenza wake kufunguliwa ufahamu na kuelewa umuhimu huu.
Wanawake wengi hasa waliotutangulia wameijua kuitumia silaha hii muhimu na kuitumia vema katika kudumisha mahusiano yao.
Kumbuka , kamwe mafahari wawili hawaishi zizi moja.
Mungu akubariki unapoendelea kujifunza na kutafakari kwa kina.
SHALOM SHALOM