Ambwene Mwasongwe - Picha ya Pili (Official Music Video)

  Рет қаралды 191,900

Ambwene Mwasongwe

Ambwene Mwasongwe

Күн бұрын

Ambwene Mwasongwe presents the Official Music Video For "Picha Ya Pili"
Stream/Download: orcd.co/pichayapili
PICHA YA PILI
Ni wimbo unaokutaka uanze kuiona picha ambayo huwezi kuiona kikawaida, Picha hii wengi wetu hatunayo, na kwa kuikosa tumefanya maamuzi mengi bila kufikiria na kwa sababu hiyo tumeongeza maumivu makali kwa wenzetu hasa wenye hali tofauti na sisi.
Mwanadamu ni kiumbe mwenye akili na mara zote amekuwa akijitahidi sana kuficha hali yake halisi ya maisha, ndio maana akitoka nyumbani, huoga, hupaka mafuta, hutabasamu, na ukimuangalia na kumsikia kwa picha ya kwanza unaweza danganyika ukadhani kafanikiwa sana, ana furaha, kapendeza na mambo yake ni mazuri.
Lakini akibaki peke yake mahali hakuna mtu anamuona hali yake halisi huwa wazi na hana cha kuficha, huko hulia sana, huugua sana, hulalamika sana, na huko ndiko anakosononeka na kupata vidonda vya tumbo, sukari, presha na msongo wa mawazo. Huko huchakata kila neno, kila tendo, kila lugha ya mwili uliyomwonyesha na hutengeneza maana ya kila tukio.
Hivyo kila unapokutana naye na kutenda jambo lolote mfikirie kwa picha hii ya pili, na jaribu kuvaa viatu vyake kwamba ungekuwa wewe ungepokeaje maneno, matendo, zawadi, na tukio ambalo wewe umefanya kwa mwenzako.
UNAWEZA toa zawadi kwa yatima, wajane, maskini, vichaa, walemavu ukafurahi ukadhani umefanya jambo jema sana,( ni kweli umefanya vyema) Lakini je! umeitafakari njia uliyotumia kutenda hayo? je! ingetumika kwako ungefurahi? au nawe ungeenda mahali pa peke yako na kulia, kuugua na kusononeka?
Jaribu kufikiri umepoteza mume wako, au wazazi wako, au kiungo chako cha mwili, Au hali yako ya maisha, kisha wanakusaidia watu kwa michango na fedha, nguo, chakula nk lakini wanakusimamisha mbele ya kadamnasi au kamera kukupa na wanakupost kila mtu aone uyatima wako, ujane, hali yako, ulemavu wako! Unahisi ukikaa peke yako utaona muujiza, fahari, bahati au utaona wametonesha kidonda cha maumivu? maana hukupenda kuwa na hali hiyo, hivyo msaada ni matokeo ya hali yako, ukiwasilishwa vibaya hauwi baraka unakuwa maumivu.
NINAKUSIHI KWA HURUMA YA YESU KRISTO UPOKEE WIMBO HUU, CHUKUA HATUA KWA AJILI YA MUNGU WASAIDIE WASIOJIWEZA, YATIMA, WAJANE, WALEMAVU NA MASKINI BILA KAMERA, MATANGAZO, NA USHABIKI MAANA HUJUI KESHO ITATOKEA KWA NANI.
Unafanya vyema kusaidia ila fanya vizuri zaidi kwa kuzingatia heshima ya unayempa kama mtu wa Mungu na wewe kama unampa Mungu.
Watch All Music Videos by Ambwene Mwasongwe: • Ambwene Mwasongwe All ...
Follow Ambwene Mwasongwe
Instagram: / ambwenemwasongwe_
Subscribe to Ambwene: / @ambweneobadiamwasongwe
Digital Branding & Marketing By:
Black Ozen Entertainment Limited: / blackozenentertainment...
JICHO LA PILI (lyrics)
Verse 1
Yahitaji macho ya moyo, kuona picha ya pili.
Yahitaji sikio la ndani, kusikia sauti ya moyo.
Nimeona chozi likitiririka, kwenye uso unaocheka.
Nimesikia sauti ya kuugua, katikati ya kigelegele.
Nimeona watu wakienda, kuwaona wahitaji, ila wamebeba kamera uuuh! kuuonyesha ulimwengu.
Yatima nao wajane, mbele ya kamera, hushukuru kwa kutabasamu.
Ila wakibaki peke yao na Mungu hulia kwa kuugua.
Sababu ya uyatima, sababu ya ujane, ni kama twadhalilishwa,. HAWAJUI size ya kiatu hiki namna kinavyobana, Hawajui twaumia.
Chorus 1
Ni Yesu tu, Ni Yesu, Anayeletaga faraja ya moyo kwa aliyeumizwa na kuvunjwa vunjwa bila matangazo... (wewe Yesu u mwema kwetu yooh!..)
Ni Yesu tu ,ni Yesu anayetoaga neno la faraja la moyo, liwe hadharani au la sirini wala haliumizi.
(Ni wewe ufanyaje kwa kutufikiria utu wetu)
Ni yesuuu tu ni Yesu anayetoaga Neno la Faraja Liwe hadharani au la sirini wala Haliumizi
Verse 2
Nilimwona mama analia, mtoto wake kawa teja, anavuja mate mtaani, wenzake wanamcheka.
Wanapiga picha naye wanafanya self wanapost wanacheka.
Wanainjoi wanatafuta views hawajui maumivu ya mzazi.
Kicha kwa mwenzako anachekesha sana, akiwa kwako anauma.
Mlemavu kwa jirani anaburudisha, akiwa kwako anauma.
Niliona wazazi wanalia eeeh! malezi yamewashinda, wamejitahidi sana kusema, watoto hawasikii.
Wanasikia mtaani wanasemwa vibaya, bado hawakati tamaa.
Hata kama ni mwizi, hata kama malaya, ni mtoto wangu hakati tamaa.
Chorus 2
Ni Yesu tu, Ni Yesu asiyewatupa tusiowajali, tunaowasema tuliowachoka na kuwadharau. (eeheee)
Ni Yesu tu Ni Yesu anayeletaga jibu la maswali kwa waliochoka, wenye utata na waliokwama (eeeheee!)
Ni Yesu tu Ni Yesu anayeletaga jibu la maisha kwa waliochoka, wenye maswali, na wenye utata. (Bwana nakuombaaa)
Verse 3
Naomba wakumbuke, tuliowachoka, tunaowasema, tunaowadharau. Bwana warehemu ni watoto na utusamehe.
Samehe makosa Yetu samehe raha yetu, tumefurahiii tukadhani tumefanya kwa ajili yao kumbe kwa ajili yetu.
Samehe Bwana kuwatangaza wao bila kujali utu.
Ni Yesuuuu Ni Yesuuu Ni Yesuuu oooh! Ni Yesuuuu Ni Yesuuu, Ni Yesuuuu, Ni Yesuuuu uuu
#AmbweneMwasongwe #PichaYaPili

Пікірлер: 932
@pastadandan3569
@pastadandan3569 Жыл бұрын
Tanzania Kuna waimbaji alafu Kuna ambwene mwasongwe huyu jamaa Huwa haimbi yeye vile ukimsikiliza Kuna malaika Huwa anaimba ndani yake sio ambwene kabisa 🔥🔥🔥🔥
@hossalemanuel1968
@hossalemanuel1968 Жыл бұрын
Amen
@janethmollel406
@janethmollel406 Жыл бұрын
Hakika uneusema ukweli mpe mtu sifa zake akiwa hai. I really understand this Man of God.❤️❤️❤️❤️❤️🙏🏻
@lilianlyatuu5442
@lilianlyatuu5442 Жыл бұрын
Fantastic Mteule wa Mwakozi.
@frankfrancis6965
@frankfrancis6965 Жыл бұрын
Ni Yesu tyu asiyewatupa tusiowajali,tunaowasema na kuwadharau,,,,ni Yesu tyu anayeletaga jibu la maswali Kwa wanaochoka ,wenye utata na waliokwama,,,,,🎉🎉🎉🎉🎉🎉🎉🎉kazihii ni njema ni darasahuru,,,mwalimu ni Yesu mwenyewe!!!!!!!Barikiwasana ,,,,NI YESU TYU@Frank mganga
@neemamabinza4208
@neemamabinza4208 Жыл бұрын
Hakika
@HighzackMichael
@HighzackMichael Жыл бұрын
✓ kama mziki wa injili ungekuwa unawawakilishi bungeni basi ambweni mwasongwe angewakilisha vizuri sana waimbaji wa injili.kwanza nyimbo zake zina upako,halafu kila dini inaweza kusikiliza nyimbo zake.simama na Yesu milele ambwene
@tanunewstz
@tanunewstz Жыл бұрын
Tunaoishi maisha ya Ambwene tujuane 🎉
@nurumwangoka5924
@nurumwangoka5924 Жыл бұрын
Kama hujawahi kuwa mjane ama yatima huwezi kuelewa ila Mfano me ni mjane mwaka wa 10 huuu changamoto nilizopitia ni #YESU tuuu amenivusha,,,,,#YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU 🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾 Asante Ambwene kwa wimbo mzuri na MUNGU wa mbinguni akubariki
@halizonihongoli4686
@halizonihongoli4686 Жыл бұрын
Ambwene mtu mzito Kichaa wa mwenzako anachekesha akiwa kwako anauma sana
@peterernest
@peterernest Жыл бұрын
Tumeenda kwenye ulimwengu ambao furaha binafsi ni muhimu kuliko utu WA wenzetu, kicheko chetu ni Bora kuliko machozi ya wenzetu, japokua havituongezei chochote ila tumechagua hivyo bila kujali wengine wanaumia kiasi gani. Ni huzuni sana kua tumetoa pasipo kuiongeza hazina yetu mbinguni Bali tumeongeza uchungu mioyoni mwa wahitaji
@edsonedmond6919
@edsonedmond6919 Жыл бұрын
Picha ya pili ni wimbo ambao Roho mtakatifu anataka watu wajifunze na wagunduwe kwamba bado tuna nafasi yakujirekebisha , maana tunazani tunafanya kwaajili ya kusaidia watu ambao wana uwitaji, bali tunafanya kwaajili ya kuonesha ulimwengu kuwa tunawasaidia watu . Mungu akutumie na akupe miaka mingi ya kuishi Mtumishi wa Mungu ambwene mwasongwe
@marykyusa8212
@marykyusa8212 Жыл бұрын
😭😭😭😭😭ombi langu kwa Mungu akulinde tu.unanfanya nikumbuke kuomba Mungu kla wakat.Mungu akuongeze zaid kwaajl ya watu wake waliotayar na wale ambao bado hawako tayar.Mungu akukumbuke daima.
@rachelgiliard4014
@rachelgiliard4014 Жыл бұрын
Hakika ni Yesu tu ndiye anaetoaga faraja ya moyo, barikiwa mtumishi.
@lymsannouncement2321
@lymsannouncement2321 2 ай бұрын
😢😢😢 huu wimbo umekua neno la faraja kwenye kipindi kigumu sana na jibu tosha sana kwenye maswali magumu tuliokua tunamuliza Mungu katika dhoruba tuliokua tunapita Mimi na familia yangu.
@erickchaula5084
@erickchaula5084 Жыл бұрын
Naweza kusema wewe ambwene huimbi bali unahubili tena mahubili ya ambayo hata makanisani hatuyasikii God bless you man of God
@mrmartinipaul2464
@mrmartinipaul2464 7 сағат бұрын
Mungu akubariki sana ila naomba tena,, tuwekee KZfaq ile nyimbo ya HAKUNA WA KUFANANA NAYE
@danielkyando4085
@danielkyando4085 Жыл бұрын
😭😭 🙇🙇nafurahi na kuogopa Mungu anapozungumza.
@christinephilip5043
@christinephilip5043 Жыл бұрын
😔😔😭
@user-vj7fx4bh2t
@user-vj7fx4bh2t 8 ай бұрын
Kusikiliza Huu wimbo Mmoja,Ni masomo Ambayo Mtu Angeweza Kuyapata Kwenye Vitabu 100 ❤
@ephraimkyando6744
@ephraimkyando6744 Жыл бұрын
Wimbo huu umenitoa machozi.... Yesu aturehemu kwa popote tulipomcheka yeyote kwa kujua au kutojua kutokana na udhaifu wake . Ahsante Yesu kwa msamaha. Tusimcheke tena yeyote au kumbeza kwa kasoro yake . Yesu bado anaweza kumuinua. Amina.
@ephrahimmasiko9873
@ephrahimmasiko9873 Жыл бұрын
Wamemchoma moto na Picha ya Pili kwangu hizi si nyimbo ni Sauti ya Mungu kwa wanadamu. Abwene ni akiba ya Mungu kwa kizazi hiki.
@MariaFilibert-wf3om
@MariaFilibert-wf3om Жыл бұрын
Kabisa
@komandowayesu3642
@komandowayesu3642 Жыл бұрын
mafuta.mafuta. kaka mkubwa wimbo ni mzuri mno🔥🔥🔥🙏🙏🙏
@DaudSulle-oe9nm
@DaudSulle-oe9nm 9 ай бұрын
Ambwene ubarikiwe sana.. huwa nabarikiwa sana na nyimbo zako.. 🙏🙏🙏🙏
@mhogomchungu7882
@mhogomchungu7882 Жыл бұрын
Nimeshasema nikienda mbinguni nisipokukuta…nitaandamana mpaka wakusamehe na ww uje mbinguni…unatubariki sana 😢😢😢
@shamirasongati3906
@shamirasongati3906 Жыл бұрын
Kichaa kwa mwenzako anachekesha sana,akiwa kwako anauma,mlemavu kwa jirani anaburudisha,akiwa kwako anauma😥😥 YESU atusaidie,,Mungu amekuweka na azidi kukuweka hai kwa ajili yetu mtumishi AMBWENE MWASONGWE utuhudumie watu tuliovunjika moyo🧘‍♀️🧘‍♀️🧘‍♀️
@DativaVedasto
@DativaVedasto Жыл бұрын
yaani nimesikiliza huu wimbo simalizi asante yesu usiyenichoka
@rudinyumbani
@rudinyumbani Жыл бұрын
Bwana Yesu atusaidie kwakweli,tupone katika hili 😭
@KidonyWambassa-rz8kq
@KidonyWambassa-rz8kq Жыл бұрын
Kuna gospel za akina rose mhando AF kuna gospel ya ambwene Anahitaji watu wenye uelewa mkubwa Wa kimungu kumuelewa! Barikiwa sana
@georgeburchard4872
@georgeburchard4872 Жыл бұрын
🤝🤝🤝
@AyubuPeter-fu5qo
@AyubuPeter-fu5qo Жыл бұрын
Mungu akubaliki ambwene Mimi nikisikiliza nyimbo zako waga nakuona umebaki pekee mwimbaji unae baliki moyo wangu
@johntaalumamadembo358
@johntaalumamadembo358 Жыл бұрын
Halleluyah Halleluyah, lisifiwe jina la Bwana kwa ufunuo huu mpya... Ila machozi yametiririka moyoni🙇🙇 Ila ni Yesu tu ni Yesu anayeletaga jibu la maswali kwa walio choka...😥😥😥
@michaelgerrard6862
@michaelgerrard6862 Жыл бұрын
MUNGU aendelee kukuinua kwa viwango vya juuu,tunaendelea kumtukuza Mungu kwa talanta yako
@salmamacha9434
@salmamacha9434 Жыл бұрын
Toka siku ya Kwanza nimeanza kumsikiliza Ambwene sijawah kuchoka wala kukinahi kumsikiliza,nilitambulishwa nyimbo zake na kijana mmoja tulikua tukiuza duka moja la nguo kinondoni studio miaka 13 iliyopita kwakweli nilibarikiwa sana na ninaendelea kubarikiwa sasa,Mungu amtunze na kuendelea kumbariki mtumishi wa Mungu Ambwene.
@KenethKilemile
@KenethKilemile 6 ай бұрын
Umeokoka?
@aalescokipangula9191
@aalescokipangula9191 Жыл бұрын
ubarikiwe kwa ufariji wako
@cosmaselias187
@cosmaselias187 Жыл бұрын
Daaah! Jamaa ujumbe umeufiksha vzur sanaaaaa! Waimbaji wengine wajfunze kwako kwamba njia ya kufikisha ujumbe co mpaka ucheze adi nguo ya ndani iyonekane!! AMINAAA
@adeshenericobatinoluho3755
@adeshenericobatinoluho3755 Жыл бұрын
Kuna Roho ndani ya huyu Bwana...Haimbi kwa akili yake ya kawaida yake na kipaji chake cha kawaida..
@yusuphmukama9958
@yusuphmukama9958 Жыл бұрын
Chochote tunachofanya kiwe kwa utukufu na kutangaza jina la Mungu na siyo kwaajili ya sisi kuonekana machoni pa watu. Mungu tusaidie sana kufanya yaliyo mapenzi yako.
@elijahrangi4370
@elijahrangi4370 Жыл бұрын
Amen and amen
@salmamacha9434
@salmamacha9434 Жыл бұрын
Ninaponywa kwa nyimbo za mtumishi Wa Mungu Ambwene nimepitia mengi mno yanayo uchosha moyo wangu ila kwakua ninae Mungu naendelea mbele mpaka pale atakaponiita japo kuna wakati nafikia kukata tamaa naona kifo ndio suluisho ila mtumishi Wa Mungu amenifanya nijirudi nakumtazamia Mungu wangu
@mlwaletyson2042
@mlwaletyson2042 Жыл бұрын
Mungu akusaidie uwe jasiri katika yote unayopitia ndugu
@jekoniarobben5307
@jekoniarobben5307 Жыл бұрын
Polee usife moyo tumaini la mwisho ni kristo
@tigerchristmas5491
@tigerchristmas5491 11 ай бұрын
Endelea kumtumiania Yesu mauti ikuepuke kbla ya muda mpendwa
@barakaedom3828
@barakaedom3828 Жыл бұрын
Ambwene Ambwene Ambwene... Nimekuita mara tatu... Unaubariki Moyo Wangu
@balozimkini5587
@balozimkini5587 Жыл бұрын
Jamaniii Mungu wa Mbinguni akutunze sanaaa,, wimbo mzuri sanaaa,,, nimebarikiwaaa,,, mwalimu wangu unastahili pongezi
@ruthlameck1450
@ruthlameck1450 Жыл бұрын
Mungu turehemu tulijua tunafanya kwa ajili Yao,kumbe Ni kwa ajili yetu.. turehemu 😭😭🙇😭😭🙏
@agnesyjoseph3906
@agnesyjoseph3906 Жыл бұрын
Hakika Ni Yesu tu anayeletaga faraja ya moyo🙏🙏, watu wengi wanakusaidia kwa lengo la kuonekana Wala si mguso wa kweli Wana malengo yao
@wa-mbeyaTv4725
@wa-mbeyaTv4725 Жыл бұрын
Nmeusikilizaa huu kwa hisia na cjakuchoka🙏🙏🙏
@ladislausmwaya2616
@ladislausmwaya2616 Жыл бұрын
daaaah kwa kweli mtumishi wa mungu ambwene mwasongwe, nyimbo zako zote huwa zinanifariji Sana , na huwa sichoki kuzisikiliza, mungu akubariki Sana na aendelee kukufunulia nyimbo nyingi zaid
@jescaakyoo2989
@jescaakyoo2989 Жыл бұрын
MUNGU akutunze daima kakaang,,azidi kukutumia kwenye izi nyakati za mwishisho ,,nmejfunza mengi kwenye nyimbo zako
@shalomchaula4420
@shalomchaula4420 Жыл бұрын
Bro ambwene iko madhabua kubwa Sana ndani yako kuhusu huduma hii na unatugikia wengi Sana yani wimbo mzima Kila mtu anajimegea kipande chake na wengi wetu tumekuwa kiimani na kupata nguvu sababu ya huduma yako ,.....lipo kundi kubwa Sana nyuma yako kaka Mungu aendele kukutumia Kwa hesabu na majira yote ambayo ameyaamuru chini ya jua.
@marystellaevarist5873
@marystellaevarist5873 Жыл бұрын
Mungu azid kuinua huduma yako mtumishi wa Mungu....unanibariki kwa kila wimbo
@happynesssamwel2917
@happynesssamwel2917 Жыл бұрын
Ambwe kaka Mungu akubariki sana sana Sieliwi ninalia nini baada kusikiza huu wimbo
@MiliiamSigara
@MiliiamSigara 9 күн бұрын
Nikwel ni YESU pekeyak 🙏🙏
@user-be8iv8hl5r
@user-be8iv8hl5r 2 күн бұрын
ni kweli kabisa ni Yesu tu
@johnmgaya2280
@johnmgaya2280 Жыл бұрын
Jamani like zenu kama tuko pamoja kumbariki mtumishi huyu katika huduma ya uimbaji
@AgnesHillary-js4hd
@AgnesHillary-js4hd Жыл бұрын
Mremavu kwa jirani anachekesha Ila ikiwa kwako anauma...mungu tusaidie
@ezrakayagambe5926
@ezrakayagambe5926 Жыл бұрын
Mungu Ameweka Neema kubwa sana Ndani Yako unafanyika baraka katika kizazi hiki Mungu Akutunze mtumishi Ili uendelee kufanyika Baraka 🙏🙏🙏
@alexmalangalila8340
@alexmalangalila8340 Жыл бұрын
Niliwahi kujikuta nawaaminisha WATU kuwa ambwene ni msanii wa muziki wa injili ambaye anamvuto ktk kuimba kwake kozi ya voko pia stori sing kwa kumlinganisha na manguli kwenye bongo ladha baada ya kuzingatia wimbo wake wa Ninamkumbuka mama mm1...mbk sasa hali hiyo naiyona sasa chukua 🌹🌹🌹yako mapema sana tusidaiane
@fridolinribatiro4064
@fridolinribatiro4064 Жыл бұрын
Amina. nimebalikiwa na wimbo huu kutoka nchini Burundi.
@neemajulius8017
@neemajulius8017 Жыл бұрын
Jamn usiombe ukawa yatima jman uyatima unauma mwee!ila ashkuliwe Mungu alie baba wa yatima anatufarij tusio na wazazi🙏!wimbo umenibarik san Mungu akubarik mtumishi na azidi kukuinua kwenye huduma yako
@gustaphmapunda3299
@gustaphmapunda3299 Жыл бұрын
I can feel your feeling, uyatima haufai
@muhimajames8111
@muhimajames8111 Жыл бұрын
Ni Yesu tu, anaye toa nano la faraja bila matangazo🤗🙌🙏💕❤
@danielsiwale4051
@danielsiwale4051 Жыл бұрын
hakika ni Yesu tu anayetoaga neno la falaja ambalo halumizi Mungu akubaliki kwa wimbo wa falaja
@neemasamwel8968
@neemasamwel8968 Жыл бұрын
Kaka ambwene Mungu azidi kukutumia huu ujumbe ulioimba naùsikia kwa mara ya pili mara ya kwanza kwa mchungaji wangu mara ya pili ni kwako kwa njia hii ya uimbaji niseme tu Mungu awabariki nyote kuna somo kubwa nimepata kutoka kwenu kiukweli ah ee Mungu uturehemu 🥲
@roidaregani6337
@roidaregani6337 Жыл бұрын
Ongoza hatua Zangu kuputia wimbo huu nimekuta machozi yananitoka
@user-uu1nx8lj7f
@user-uu1nx8lj7f 6 ай бұрын
Wimbo unaujmbe mzuri San, ubarikiwe SANA
@emmanuelsamwel741
@emmanuelsamwel741 Жыл бұрын
Huu wimbo umejaa message kubwa sana , kumbe kila unamuona kichekesho au hafai macho ya pili ni maumivu wanayapitia😢😢
@BeatriceKivuyo-df7gv
@BeatriceKivuyo-df7gv Жыл бұрын
Wimbo umenitoa machozi,, Mungu tunaomba neema ya kufanya kwa ajili yao na si kwa kujionyesha
@McTabasam-is1de
@McTabasam-is1de 9 ай бұрын
Kaka ambwene mungu azidi kukutunza kwaajili yangu na watu wengine ambao wanaona ibada ambayo unaifanya kupitia uimbaji
@nkungujackson7092
@nkungujackson7092 Жыл бұрын
Nyimbo zako zinaishi hiyo haina kupinga jaribu kufutilia albam ya kwanza Hadi ya mwisho hakuna nyimbo ya ovyo hata mmoja 🙌🙌🙌😭😭
@EverlynKenneth
@EverlynKenneth 9 ай бұрын
MUNGU AMTUNZE MTUMISHI WAKE❤😢
@user-gc4on8hh4r
@user-gc4on8hh4r Жыл бұрын
Kaka mafuta haya nilianza kuyaona tangu wakat wa majaribu ni mtaji, umekuwa wa pekee na mfano Kwa waimbaji wa gospel, Siri Yako naifahamu ni maombi na unyenyekevu barikiwa Sana.
@everlynkilimba3963
@everlynkilimba3963 Жыл бұрын
Powerful ,
@powerofgospelbandtz196
@powerofgospelbandtz196 Жыл бұрын
Atal kaka MUNGU hakutumie zaidi ya hapoulipo nyimbo imebeba ujumbe 🔥🔥🔥
@daudiisack8252
@daudiisack8252 Жыл бұрын
Barikiwa rafiki yangu Ambwene Mwasongwe wewe ni mbarikiwa aisee..
@benardmbuuko6801
@benardmbuuko6801 Жыл бұрын
Mungu akubariki kaka ambwene.itakuwa nadra kweli kujipata kwenye upande wa haki kwenye hukumu hii .lakini twaweza kuungama na kusamehewa kwake yesu..
@samuelmlapwa7858
@samuelmlapwa7858 Жыл бұрын
Utukufu kwa Bwana na Ubarikiwe na Bwana mtumishi
@robertthadeo
@robertthadeo Жыл бұрын
Hakika Mungu anakupelekaga mbali kukupa jumbe zenye tafakari ya ndani sana, wimbo umeugusa moyo wangu sana😢😢
@sophiashabani5361
@sophiashabani5361 9 ай бұрын
Mwimbo wa baraka sana hakika ni yesu tu
@sayunimrocky8445
@sayunimrocky8445 Жыл бұрын
Ukisikia mahubiri kwa nyimbo ndiyo haya, Mungu akuweke kaka kuna kipindi nilikpita sikujuanitatokaje lkn nilipokua nakusikiliza nilijikuta nafarijika nakujiona ni mtu mwenye thamani sana, kama ule Mungu aliniamini alijua hili naliweza nakweli nimeliweza na nimepita slm. Keep it up my brother na Mungu akupe hitaji la moyo wako.
@bethstanford9840
@bethstanford9840 Жыл бұрын
Kwa kwel huyu kaka Mungu amtunze Sana uwa anagusa Sana moyo wangu ,nilifiwa mm na mchumba wangu na nikawa Sina mwelekeo mwez wa pili msiba mwez huohuo akatoa nyimbo nimeachilia kiukwel ni Yesu tu
@rehemafungo3705
@rehemafungo3705 23 күн бұрын
Mungu azidi kukuinua zaidi ya apo shetani asipate nafasi ya kukuangusha
@youngvocal6946
@youngvocal6946 Жыл бұрын
Barikiwa sana baba ambwene picha ya pili
@giftyboakye-boateng2323
@giftyboakye-boateng2323 Жыл бұрын
I do not understand the lyrics of this song, as a matter of fact I heard this song from my Tanzanian friend… but my spirit resonated with it. Indeed our spirit attest that we are children of God. Would a subtitle version of English for this song
@user-cr8bf2rd3k
@user-cr8bf2rd3k Жыл бұрын
Hata nikiwa n magumu gan nikisikiliza nymbo zako napata faraka mungu akuinue zaid 4:08
@samuelbahatifranck7028
@samuelbahatifranck7028 Жыл бұрын
WIMBO HUU UMEJAA NA MAFUNDISHO MAKUBWA SANA, MAN OF GOD AMBWENE MUNGU AMEKULETA DUNIANI KWA INJILI NA MOYO WAKO UNAJAA MAPENDO YA KIMUNGU KUPITIYA MANANO MAKALI YA UFUNUO AMBAYO UMEPEWA NA ROHO MTAKATIFU. MUNGU AKUONGEZE ZAIDI
@user-vf8mc7dy5y
@user-vf8mc7dy5y Жыл бұрын
🎉🎉🎉mimi nakupa maua yako mapema ❤❤ ubarikiwe sana
@amigoshamisi126
@amigoshamisi126 Жыл бұрын
Mungu akuzishia ubunifu Saidi.
@ElizabethLugono
@ElizabethLugono Жыл бұрын
Ninabarikiwa sana sana na wimbo huu halafu kuna siku ulikuwa singida kkkt wakati unaimba nilipata ishara maombi yangu kwa Mungu akutunze na akutendee shauku na kiu ya moyo wako
@annabashasha1409
@annabashasha1409 Жыл бұрын
😭😭Kila nikisikia wimbo huu machozi yananitoka tuuu,, Mungu akutendee mema Ambwene
@etooferooz3086
@etooferooz3086 Жыл бұрын
asante sana kwako ndugu ambwene mwasongwe kwa nyimbo hizi,ila kumbuka ndugu yangu ulimwengu huu kwa sasa hunafikia kikomo,sasa hakikisha kipaji hikichako hiki ni mungu mwenyewe tu ndo anakuongoza,na husikichanganye na kavumu za ulimwengu huu,husijekua mwalimu na mwinjilisti kwa wengine alafu hukakosa kuhiingia kwenye mbingu mpya na yerusalemu mpya ambayo bwana wangu yesu kristo,anao wa wekea wale walioshindania ziki kuu,na waliofia imani ya mitume wa bwana wangu yesu kristo mungu aliehai,na mungu akubariki sana amina.
@mwlhalimoja.ekingunza1819
@mwlhalimoja.ekingunza1819 Жыл бұрын
Tanzania kuna waimbaji wengi sana ila kwangu mimi hakuna aliyewahi kukupita Ambwene. Wewe ndiyo chaguo langu la kwanza siku zote miaka 20+ kwa sasa. Uishi milele na Bwana Yesu aikuze Karama yako maana hujawahi badilika kutafuta pesa bali huisema kweli ambayo wengi imewashinda. Live long Mtumwa wa Yesu Kristo.
@georgeburchard4872
@georgeburchard4872 Жыл бұрын
Nakuunga mkono! Hakika upo sahihi Sana!
@johnsonbubinza4646
@johnsonbubinza4646 Жыл бұрын
uyu mzee wa nimeachilia si aliteswa kule na mke wake sasa anakuja kuwapa msaada wahitaji uku yupo na camera. ila Ambwene naomba utoe wimbo wa pamoja na akina mwakalinga boaz dr ipyana nawakubali sana nyie
@magdalenamsengi2016
@magdalenamsengi2016 Жыл бұрын
Very powerful message. Mungu atusaidie tunajisahau sana kwenye mambo kama haya. Umebarikiwa Mtumishi wa Mungu na asante kwa ujumbe huu🙌🔥🔥🔥
@andrewjohn-rm9xt
@andrewjohn-rm9xt Жыл бұрын
Naamini sikumoja nitakua kama Ambwene nitaimba na yeye wimbo mmoja 🙏🔥🔥🔥
@atupakyselwesya5853
@atupakyselwesya5853 Жыл бұрын
Hajawahi kosea kuimba tangu nianze kumfuatilia mungu azidi kukuongoza zaidi na zaidi
@samsonmtalege4858
@samsonmtalege4858 Жыл бұрын
Ukiusikiliza huu wimbo vizuri lazima machozi yakutoke, barikiwa Sana mtumishi A. Mwasongwe
@naomipanja5768
@naomipanja5768 Жыл бұрын
Ni YESU tu anaye toa faraja ya kweli😔😌😔😌☺️😊.. nampenda YESU wangu😊😚😘☺️🥰
@elvismalonga7427
@elvismalonga7427 Жыл бұрын
Tuko tuna subiri sana nyimbo, zegine piya
@stevenmwandelile9819
@stevenmwandelile9819 Жыл бұрын
Namkubali sana
@ImpressiveFacts
@ImpressiveFacts Жыл бұрын
Mungu akubariki sana mtumishi kwa ujumbe huu mzuri
@paulinajemson2719
@paulinajemson2719 Жыл бұрын
Huu wimbo eeh Mungu 😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭
@deborahmakisha
@deborahmakisha Жыл бұрын
Barikiwa mtumishi kwa uimbaji mzuri wa kuganga mioyo. Mungu akuinue viwango kwa viwango, viwango viwango..... Amen
@ibwesilvano8493
@ibwesilvano8493 Жыл бұрын
Be blessed🙏🙏
@Obeidkazimili
@Obeidkazimili Жыл бұрын
Kama unataka nyimbo zenye ujumbe wa sasa ni hizi hapa
@nacybrian
@nacybrian Жыл бұрын
So touching song mnaotoa misaada na macamera muwe mnaangalia huyo mtu anataka hizo camera au anahitaji faraja Kuna muda Hana namna ..... Yesu awabadirishen Kwa dam yake ahsante kaka ambwene ni kweli Kuna muda unaona tabasam la mtu kumbe moyoni ana mengi anayapitia
@witnesskilale3361
@witnesskilale3361 Жыл бұрын
Asante Mungu kwa kumtumia ambwene mwasongwe kutufariji,kututia moyo,kutufundisha neno la mungu,kutufundisha namna ya utoaji wa sadaka .Mungu Asante kwa ajili yake .umenibariki na kunifuta machozi mara nyingi eeeeeeh Mungu asante
@joycemwafungo4673
@joycemwafungo4673 Жыл бұрын
Ooooh my God. where did you came from with song. Its really life we had. oooh Mungu asante kwa ujumbe huu.
@georgeburchard4872
@georgeburchard4872 Жыл бұрын
Hivi jamani mna hakika huyu Bwana Ambwene ni binadamu wa kawaida? Mbona nishaanza kupata mashaka! Huu uwezo sio wa kawaida kabisa!
@LisahAlly-nd5st
@LisahAlly-nd5st Жыл бұрын
😁😁😁
@donathalinus5538
@donathalinus5538 4 ай бұрын
Inatosha bwana, aksante Ambwene kwa ujumbe mzuri Mungu akuweke maisha marefu
@MossesGidagui
@MossesGidagui 13 күн бұрын
Mimi namuona mungu ndani ya ambwene
@blaunclecleaning9492
@blaunclecleaning9492 9 ай бұрын
Strong msg man of God
@Witnessvlog
@Witnessvlog Жыл бұрын
Huyu ndiye Ambwene tunaemjua. Asante sana Mtumishi kwa wimbo mzuri unaogusa. Hakika tunachakujifunza. Salaam kutoka Denmark
@afamatv4848
@afamatv4848 Жыл бұрын
witness Kwanza naomba namba yako. Nakuonaga tu KZfaq
@Officialpiejotv
@Officialpiejotv Жыл бұрын
​@@afamatv4848 kaka na wewe skwizi hupokei cm Yangu, cjui kwanini yaani 😢😢 P4 hapa.
Ambwene Mwasongwe - Nimeachilia (Official Music Video)
7:17
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 1 МЛН
AMBWENE MWASONGWE - NITAAMBATANA (official music video)
7:48
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 393 М.
Inside Out 2: Who is the strongest? Joy vs Envy vs Anger #shorts #animation
00:22
БАБУШКИН КОМПОТ В СОЛО
00:23
⚡️КАН АНДРЕЙ⚡️
Рет қаралды 17 МЛН
Gym belt !! 😂😂  @kauermtt
00:10
Tibo InShape
Рет қаралды 17 МЛН
Ambwene Mwasongwe - Nifundishe Kuomba (Official Music Video)
7:15
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 220 М.
Bony Mwaitege - MWALIMU (Official Music Video)
6:34
Bony Mwaitege Official
Рет қаралды 57 М.
Uongezeke Yesu | Boaz Danken
11:40
Lucas Kaaya
Рет қаралды 2,3 МЛН
AMBWENE MWASONGWE - ALIKUTA IBADA (OFFICIAL MUSIC VIDEO)
8:07
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 1,2 МЛН
The Best Of Christopher Mwahangila Songs 2021
1:35:00
CHRISTOPHER MWAHANGILA Official
Рет қаралды 8 МЛН
Sadraddin - Taxi | Official Music Video
3:10
SADRADDIN
Рет қаралды 811 М.
Serik Ibragimov ft IL'HAN - Жарығым (official video) 2024
3:08
Serik Ibragimov
Рет қаралды 187 М.
akimmmich (feat. Turar) - UMYTTYŃ BA?| official lyric video
2:54
Taxi
3:06
Sadraddin - Topic
Рет қаралды 219 М.
Әбдіжаппар Әлқожа - Ұмыт деме
3:58
Әбдіжаппар Әлқожа
Рет қаралды 1,2 МЛН
지민 (Jimin) 'Who' Official MV
3:28
HYBE LABELS
Рет қаралды 28 МЛН