AMBWENE MWASONGWE - ALIKUTA IBADA (OFFICIAL MUSIC VIDEO)

  Рет қаралды 1,283,799

Ambwene Mwasongwe

Ambwene Mwasongwe

2 жыл бұрын

Ambwene Mwasongwe presents the music video for "Alikuta Ibada"
Wimbo huu ni maalumu Kwa ajili ya kulikumbusha kanisa la Bwana kuwa tumefikia Hali ileile ya Mafarisayo na Masadukayo ya unafiki.....
Nakukumbusha tunapaswa kumwabudu Bwana kwa roho na kweli.....
Tuondoe na kuyaacha mambo mengi ya mwili tuliyoyaingiza kanisani, turudi kwanza msalabani Kisha tuendelee na safari....
Mungu akubariki utayeuona huu wimbo na nisaidie kuwatumia link na wengine ili ujumbe umfikie kila MKRISTO
Watch All Music Videos by Ambwene Mwasongwe: • Ambwene Mwasongwe All ...
Follow Ambwene Mwasongwe
Instagram: / ambwenemwasongwe_
Subscribe to Ambwene Mwasongwe: / @ambweneobadiamwasongwe
Digital Branding & Marketing By:
Black Ozen Entertainment Limited: / blackozenentertainment...
Alikuta Ibada - Ambwene Mwasongwe (Lyrics)
Alikuta ibada zinaendelea
Ila zina tatizo
Alikuta maombi yanafanyika
Ila yana kasoro
Alikuta mifungo inaendelea
Ila ina dosari
Akakuta sadaka zinatolewa
Ila zina makandokando mengi
Akashangaa mwili umetawala
Badala ya Roho!
Akawafundisha ibada za Rohoni
Jinsi zitakiwavyo
Muombapo msiombe sala ndefu
Ili watu wawasifu
Mtoapo msitoe kwa matangazo
Ili watu wawaone
Mfungapo msijionyeshe
Ili watu wawasifu
Ila baba yenu aliye sirini
Yeye atawajazi
Mungu ni roho
Na wote wamwabuduo
Imewapasa kumwabudu
Kwa roho na kweli
Yeye huona kile ambacho jicho haliwezi kuona
Yeye hushika kile ambacho mkono hauwezi kukishika
Yeye hutafsiri lugha ya moyo hata mdomo usiposema
(Kwake hakuna siri)
Akawakemea Viongozi wa dini
Na washika sheria
Waandishi na mafarisayo
Na masadukayo
Hawakutaka-Walikasirika
Wakaleta vitabu
Kwa mamlaka ya nani wafanya haya?
Wapate kumshitaki
Wakadhani kiroho ni shule
Ili wamfedheheshe
Akawatazama akawapima
Walikuwa weupe
Wakamletea mwanamke mzinzi
Aliyefumaniwa
Wakataka wasikie neno lake
Atakavyomuhukumu
Akainama akachora chini
Akaandika majina yao
Ardhi ikageuka "video touch"
Wote wakakimbia
Mzee wa kanisa alipojiona
Akilewa na wake za watu
Shemasi kaona aibavyo sadaka
Naye akakimbia
Wanakwaya wakaona wanavyosengenyana
Na kupiga majungu
Yesu alipoinuka
Wote wamekimbia
Akasema na mimi sikuhukumu
Nenda usitende dhambi tena!
Ole mafarisayo na masadukayo
Mwaosha vikombe kwa nje
Ila ndani ni vichafu
Mwapaka makaburi chokaa
Ndani yake ni mifupa
Mwawabebesha watu mizigo
Ninui hambebi
Ole!
Mwawatungia wengine sheria ninyi hamzifuati!
Ey!
Akalikaribia kapu la sadaka
Aone wanachotoa
Ghafla akamwona mwanamke mjane
Anatoa kichache
Akasema huyu ametoa vingi
Kuliko ninyi nyote
Maana kwa Mungu wingi sio idadi
Ni ukamilifu wa jambo
Wengi mmetoa kwa mbwembwe
Vimeonekana vingi
Ila mlivyobakisha nyumbani ni vingi
Sio kama mwanamke huyu
Akaona wanagawana chenji ibadani
Akakasirika
Wanauza vitu kama mnada hekaluni
Mahali pa ibada
Akachukua fimbo akawachapa
Akapinduapindua
Nyumba yangu itakuwa ya sala
Sio nyumba ya biashara
Uko wapi moyo wa ibada?
Uko wapi moyo wa kicho!?
Ule moyo wa kutetemeka
Tusikiapo neno la Bwana
Mambo haya Je yamo kanisani leo basi tujiulize
Akija yule mwenye kanisa
Je hatatuchapa?
Mungu ni Roho
Na wote wamwabuduo
Imewapasa kumwabudu kwa roho na kweli
Maana yeye huona kile ambacho jicho
Haliwezi kuona
Yeye hushika kile ambacho mkono
Hauwezi kukishika
Yeye hutafsiri lugha ya moyo hata mdomo usiposema
Tunatakiwa tumwabudu Bwana
Tusichonge sanamu
Tuangalie tusije kujiabudu wenyewe
Pamoja na vitu vyetu
Tukicheza ili watu watuone
Tumejiabudu wenyewe
Tukiimba ili watu watufurahie
Tumetwaa utukufu
Tukigeuka nyuma na kutafuta maoni ya watu
Tumejichuuza wenyewe
Hicho ndicho kilichomponza lusifa
Alitaka asifiwe
ooh!
#AmbweneMwasongwe #AlikutaIbada

Пікірлер: 1 600
@nakilingwembele9504
@nakilingwembele9504 9 ай бұрын
Jaman tunapoandka jina Mungu tusianzie na herufi ndogo,anza na herufi kubwa maana ndo Mungu aliyehai,ukiandika kwa herufu ndogo c Mungu aliyehai
@user-cr4eu4zc6u
@user-cr4eu4zc6u 2 ай бұрын
Mungu nijalie kuyafany mapenzi Yako wewe uonae moyoni mwangu😭😭😭😭
@SupajrChagaa
@SupajrChagaa 3 ай бұрын
Huu wimbo kila nikikaa niangalie TV lazima nianze na huu wimbo najiona kama nahubiriwa na mtume Paulo,ambwene Mungu wa mbinguni azid kukutumia uendelee kuomba kirohoo
@japhetmichael7608
@japhetmichael7608 2 жыл бұрын
Kaka Mungu akubariki waimbaji wa Tanzania nadhani wajifunze kwako miaka mingi upo unamtukuza Mungu lakini hauchoshi my brother Yesu akubariki Sana
@user-fv9tu2pe8s
@user-fv9tu2pe8s 4 ай бұрын
Endelea kutumikia KUSUDI LA MUNGU kwa kicho. BWANA YESU anaona utumishi wako
@pasteurelizabethruzoviyo3978
@pasteurelizabethruzoviyo3978 2 жыл бұрын
mungu akubaliki ambwene mwasongwe mimi wakati nime anza kusikia nyimbozako nili amuwa kuokoka kwa sasa niko bishop wakanisa inchi burundi🇧🇮
@israelmbedule3897
@israelmbedule3897 Жыл бұрын
Barikiwa sana
@ziadaambanjaula8900
@ziadaambanjaula8900 Жыл бұрын
Du umeokoka aya ubalikiwe
@elizabethleonard1809
@elizabethleonard1809 Жыл бұрын
Glory be to God 🙏
@cizajean-marie7223
@cizajean-marie7223 Жыл бұрын
Wahisemwo neza ncuti y'umusaraba
@wafabian8116
@wafabian8116 Жыл бұрын
God is great hallelujah
@citovunjabeilimitedcompany4455
@citovunjabeilimitedcompany4455 2 жыл бұрын
Naomba jina lako kamili nikutumie muchango mdogo imekuwa muda ume nibariki sana
@ambweneobadiamwasongwe
@ambweneobadiamwasongwe 2 жыл бұрын
Mungu akubariki Sana 0767619931 au 0713619931 Ambwene Mwasongwe
@VastineKahindo
@VastineKahindo Ай бұрын
Hi wimbo unanijenga sana
@Ijusthavequestions
@Ijusthavequestions Жыл бұрын
True worshipers will worship in Spirit and Truth.
@JanethMgeni-cr4wl
@JanethMgeni-cr4wl 2 ай бұрын
Ubarikiwe mtumishi wa munngu kwa ujumbe wa mungu kwa mataifa naamini wengi tumefunguliwa ubarikiwe sana
@christinamwangoc4779
@christinamwangoc4779 2 жыл бұрын
Namshukuru MUNGU kwa ajiliyako kwamaana katikati ya mabadiliko ya dunia Sayansi na tecnolojia lkn bado nakupata kakaangu unaemwimbia MUNGU ktk roho na kweli, MUNGU AKUTUNZE !
@nellykobadi8142
@nellykobadi8142 Жыл бұрын
Uko wapi moyo wa ibada, moyo kutetemeka aiseeeh Mungu nipe moyo wa ibada nikuabudu katika roho na kweli
@rebeccan2321
@rebeccan2321 3 ай бұрын
Uko wapi wa moyo wa Ibada ,ee Mungu wangu nanyenyekea kwako nope Moyo wa Ibada nikuabudu ktk Roho na kweli.❤
@REHEMAMGENI
@REHEMAMGENI 2 ай бұрын
Amen ambwene
@lazarozebedayo4948
@lazarozebedayo4948 2 ай бұрын
Amen wimbo mzuri Sana unaponya moyo
@mackrinaerenesto6402
@mackrinaerenesto6402 Жыл бұрын
Amina baba ubalikiwe San nabarkiwa San na nyimbo zako na haipit sku nimeskilza nakpenda san maana nyimbo zako nazielewa sana 🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽❤️❤️❤️❤️❤️
@robertwaichigo2553
@robertwaichigo2553 2 жыл бұрын
Huu ni zaidi wa Wimbo. Ujumbe wa Yesu Kristu.
@ZaiElias
@ZaiElias 2 ай бұрын
Amina🎉🎉❤
@letisiabaritazari7606
@letisiabaritazari7606 Ай бұрын
Wimbo muzuli Sana mungu akubaliki
@franksentiyongo8803
@franksentiyongo8803 Жыл бұрын
Ninapo sikiriza wimbo huu najifunz kitu mungu akubark ambwene mwasongwe ukyala utufighwe fihjo kangi fihjo
@jannethjohn747
@jannethjohn747 Жыл бұрын
Kaka Ambwene wewe endelea hivyohivyo kumsikiliza Mungu ktk huduma yako, hubiri kupitia uimbaji, tulio wengi chanzo cha kuokoka ni kupitia uimbaji, achana nao hao wanaoifuata dunia, wewe mtumikie Mungu kikamilifu
@SamsonEzekiel-or9xc
@SamsonEzekiel-or9xc 2 ай бұрын
Halloo halloo hii imeenda safiiii oyoooo
@Bryson883
@Bryson883 9 ай бұрын
Huu Wimbo ni Mawaidha, huu wimba ni mahubiri, huu wimbo ni Ibada, huu wimbo ni Misa takatifu...ubarikiwe sana Mtumishi wa Mungu...endelea kutimiza jukumu la Mungu kukuleta Duniani🙏
@leticiamakoye4871
@leticiamakoye4871 4 күн бұрын
Wasaidieni wake zenu wavae kibibilia
@mariampatrick3479
@mariampatrick3479 2 жыл бұрын
Hakika mwenyez MUNGU amekubarik kipaji MUNGU aendelee kukutumia
@martinchambai5460
@martinchambai5460 Жыл бұрын
Wimbo mzuri sana. Picha pia iko vizuri sana. Mungu aibariki huduma yako
@katarinasimon8647
@katarinasimon8647 3 ай бұрын
Nzuri sana jamani eeeh baba akubariki Mungu aah😅
@farajaemanuel1992
@farajaemanuel1992 2 жыл бұрын
Tenashara wa kizazi hiki. Yesu angekuchagua kuwa tenashara kaka,, Coz angeutazama moyo wa Utumishi ndani Yako.
@AnnaMasangula-h5e
@AnnaMasangula-h5e Ай бұрын
Mungu nisaidie mengi yanautesa moyo wangu, from now nimeachilia
@brendakinenekejo8464
@brendakinenekejo8464 Жыл бұрын
Nmejikuta nanena kwa lugha barikiwa mtumishi wa bwana
@lucywilson5875
@lucywilson5875 2 жыл бұрын
Hizi ndizo nyimbo tunazohitaji kusikiliza. Barikiwa Ambwene
@mzurikwaorevocatus2972
@mzurikwaorevocatus2972 2 жыл бұрын
Kwel yan
@givasmwananzumi5941
@givasmwananzumi5941 Жыл бұрын
@@mzurikwaorevocatus2972 kabisaaa hi nyimbo nzuri xn
@argentinachottah5962
@argentinachottah5962 Жыл бұрын
Ambwene Ambwene Ambwene Mwasongwe MUNGU BABA WA MBINGUNI AKUBARIKI SANA
@yulemwinjilisti
@yulemwinjilisti Жыл бұрын
Mandiko mwanzo mwisho.just how it should be.
@jamesbavo
@jamesbavo 2 жыл бұрын
Namshukuru Mungu kwa kutupatia zawadi hapa Tanzania 🇹🇿 ambayo ni #Ambwene_Mwasongwe na #Boaz_Danken kiukweli nyie watu mna Mungu ninaemuabudu mimi na mnaongozwa na Roho wa kweli
@nancygilliad2883
@nancygilliad2883 Жыл бұрын
Wimbo huu unanibariki sana san haya ndio mambo yapo leo makanisan Mungu atusaidie kweli,ubarikiwe Ambwene
@damianmwombeki5879
@damianmwombeki5879 2 жыл бұрын
Tuponye vijana wa sasa Mtumishi na MUNGU atusaidie
@rosadinahjoseph9137
@rosadinahjoseph9137 Жыл бұрын
Wimbo huu hunifanya ni barikiwee sanaa .... Mungu akutunzeee mtumishi
@magrethmkongwee8512
@magrethmkongwee8512 2 жыл бұрын
Katika watumishi wa Mungu tuliobaki nao Tz wanaoimba katika roho na kweli! Barikiwa saana Mtumishi! Unaponya saana mioyo ya wengi!
@mzurikwaorevocatus2972
@mzurikwaorevocatus2972 2 жыл бұрын
N kwel
@jeanettekikonde987
@jeanettekikonde987 2 жыл бұрын
Kwel kabisa nyimbo zake. Pamoja na mavazi yake inapendeza Sana ubarikiwe sana maombi ni silaa tosha
@sarahnyamwendo2118
@sarahnyamwendo2118 Жыл бұрын
Nyimbo niipendayo kila sku lazma niiskize Mungu akubariki sana kweny huduma
@ozanasylvester3663
@ozanasylvester3663 2 жыл бұрын
Ee Mwenyezi Mungu tunaomba utusaidie masikio ya Rohoni tunapo hubiriwa mafundisho kama haya kwa nyimbo tusiyapuuze bali yakalete mabadiliko ndani ya mioyo yetu.Amina
@johnmgaya2280
@johnmgaya2280 Жыл бұрын
Nataka like zenu kama huna kinyongo na mwenzio ( moyo mweupe)
@moseskipawua9548
@moseskipawua9548 Ай бұрын
😢😢😢😢😢😢😢😢😢
@milkajm4762
@milkajm4762 2 жыл бұрын
😭😭😭😭 Mungu tusaidie kurudi katika Neno na tuishi katika Roho.
@neemasanga5998
@neemasanga5998 Жыл бұрын
Akawaafundisha ibada za rohon jinc zitakiwavyo
@nasramtuluma3949
@nasramtuluma3949 Жыл бұрын
Nasikiliza huku nasisimka...asante kwa msg nzur
@ConfusedMonarchButterfly-bp5dx
@ConfusedMonarchButterfly-bp5dx 2 ай бұрын
Amina ❤❤
@eliufoosimonchuri4160
@eliufoosimonchuri4160 2 жыл бұрын
Mtumishi wa Bwana ubarikiwe. Tumepata ujumbe toka Yohana 4:24 kwa njia ya nyimbo. Kiukweli huwa unaimba theologia, tunapona kwa nyimbo zako. juzi mwana wa Azali, leo tena ujumbe huu muhimu.Mungu atusaidie tuabudu katika roho na kweli 🙏🙏🙏
@emmasanga4279
@emmasanga4279 2 жыл бұрын
Ubarikiwe sana Kaka endeleaa mbele .
@giftasifiwe
@giftasifiwe Жыл бұрын
Hii nyimbo imenikumbusha mwaaka 1984.kanisani.turivyofundishwa.
@daudicherehanis
@daudicherehanis Жыл бұрын
mungu akuzidishe katika huduma yako
@michaelmwanda1673
@michaelmwanda1673 2 жыл бұрын
Mungu wa mbinguni akubali sana mtumish wa bwana kristo akutie nguvu
@vedastomtasha
@vedastomtasha 2 жыл бұрын
Hakika wew ni mwamna imara daaaa nyimbo nmeikuta TikTok daa nmeifata ujumbe mzito sana najivunia kua na wew tz
@daynesnyoni2715
@daynesnyoni2715 2 жыл бұрын
Kuna vile hii nyimbo inatuonesha bible ni kitabu kizuri sana, kitachotufanya tukutane na watu walioshi maisha kama yetu , ILa walikuja kubadirika na kuwa watu wema sana, mungu akubariki na kukutunza sana kaka ambwene, akuweke ili kupitia wewe wengi kati yetu tumrudie mungu🤲 na kuijua kweli🙏.
@vickynduku4753
@vickynduku4753 2 жыл бұрын
Ambwene mwasongwe is underated his music is beyond international level ...God bless you MoG ...my favorite artist
@guershombenoit7156
@guershombenoit7156 2 жыл бұрын
Mungu Aku bariki muimbadji wa Mungu bwana
@montteyfloki3953
@montteyfloki3953 2 жыл бұрын
Hii nyimbo inatosha kukuweka kwenye uwepo wa roho mtakatifu
@damasmayanja2930
@damasmayanja2930 Жыл бұрын
Hii ni Injili, this is Gospel mpeni maua yake Mwasongwe
@user-tk2lw3wu2u
@user-tk2lw3wu2u 3 ай бұрын
Glory to God ❤❤
@ezekielenock4650
@ezekielenock4650 Жыл бұрын
Asante sanaa kwa kunikumbusha Ibabda ya Moyoni Mtumishi
@kelvinkijo7500
@kelvinkijo7500 2 жыл бұрын
Amen sana ubunifu mkubwa mtumishi wa BWANA, zidi kubarikiwa!
@joellumala3206
@joellumala3206 2 жыл бұрын
Our own Ambwene,. Kanisa letu la Tanzania lina baraka sana kuwa na mtu wa aina yako,. Umebarikiwa ulikumbushe kanisa na watu wa Mungu kuhusu maisha halisi ya Rohoni kabisa kabisa,.😌
@neemakitano5894
@neemakitano5894 2 жыл бұрын
Kaka Ambwenee nabarikiwa Sana nanyimbo zako. MUNGU akubariki sanaaaa sanaaaa 🙌🙌🙌🙌
@josephinemwambe3385
@josephinemwambe3385 Жыл бұрын
Huu wimbo umasema yanayotendeka kwa makanisa siku hizi Mtumishi wa mungu kakangu Ambwena kwa kweli nyimbo zako za nitia nguvu sana.. Wimbo mtaamu mno..Barikiwa sana South Africa 🇿🇦 Cape Town tunabarikiwa Ujumbe ufikia watoto wetu nchini Kenya 🇰🇪
@geitandelwa299
@geitandelwa299 Жыл бұрын
Ameni tuna Mambo MENGI Ila Sio ya MUNGU
@prosperkileo7139
@prosperkileo7139 2 жыл бұрын
AMEN AMEN AMEN UBARIKIWE NA KRISTO YESU ALIE HAI BINAFSI NIMEBARIKIWA NA KUJIFUNZA
@beatricemwasunda5027
@beatricemwasunda5027 2 жыл бұрын
Jehovah aonaye Sirini braza azodi kukuweka makumbusho kwa ajili ya UTUKUFU WAKE...Ahsante nimepokea ujumbe wangu
@ebenezerdayan3797
@ebenezerdayan3797 2 жыл бұрын
Duh!!!kuna wakati Daudi akiona kile Mungu amekiweka ndani yako anafarijika sana huko mbinguni na anatabasamu akijua kapata pacha aliyebaki hapa duniani. Ninampenda Mungu kwa ajili yako Ambwene🙏🙏🙏
@maggishillah4847
@maggishillah4847 2 жыл бұрын
Kabisaa yaani... It's a Powerful Song!
@juliananicodemus2746
@juliananicodemus2746 2 жыл бұрын
Wimbo mzuri mungu akubariki sna kaka Ambwene
@Jenipha-so9rk
@Jenipha-so9rk 3 ай бұрын
Ibada njema
@evansimsagaatkog1953
@evansimsagaatkog1953 2 жыл бұрын
Mtumishi wimbo huu uko vizuri Sana Sana ebuwatu wausikilize ktk Roho Kuna Mambo makubwa ya kujifunza
@ireennanjela2993
@ireennanjela2993 2 жыл бұрын
Huu wimbo umefundisha ubarikiwe mtumishi endelea kua kiroho acha roho aendelee kukuongoza ktk utumishi wako.
@ConfusedMonarchButterfly-bp5dx
@ConfusedMonarchButterfly-bp5dx 2 ай бұрын
Amen
@kamotajunior1681
@kamotajunior1681 2 жыл бұрын
This is exactly what is happening in our churches today, wimbo huu una mafundisho ya kweli.....
@vumiliajumanne8217
@vumiliajumanne8217 Жыл бұрын
Mungu akubaliki nyimbo zako zinanibariki
@isayasementi2646
@isayasementi2646 Жыл бұрын
Ubarikiwe kaka AMBWENE hakika MUNGU katupa wewe zawadi watanzania
@sebastianmwantuge5597
@sebastianmwantuge5597 Жыл бұрын
Sijashangaa kwa uzuri wa wimbo huu maana Mungu amekuinua,nyimbo zako zote ni nzuri na zina mafundisho. Mungu aendelee kukuinua.
@hyasintapastory4398
@hyasintapastory4398 Жыл бұрын
Naupenda sana huu wimbo
@mamacaren1519
@mamacaren1519 Жыл бұрын
Kaka nabarikiwaga sana na nyimbo zako hakika unanigusa sana nakuelewa sana nazichambuaga mpaka napata maana Barikiwaaa
@godlivingurassa5752
@godlivingurassa5752 2 жыл бұрын
Sina la zaidi ya UBARIKIWE
@pardonmwalyego9947
@pardonmwalyego9947 2 жыл бұрын
Kwa nyimbo zako tunamtukuza Mungu....live long life in music!! Stay blessed.
@faithikenda
@faithikenda 2 жыл бұрын
Natamani sasa Mungu akupe neema ya kuanza kufundisha na semina, seems you have more and we need to hear more!! Una hazina kubwa moyoni mwako .. Ikimpendeza Mungu akupe namna nyingine ya kutufikishia kwa wingi. Stay blessed
@danielmwenda3710
@danielmwenda3710 2 жыл бұрын
Mwimbaji.bora.kwangu.mpaka.dunia.itanduke.mungu.akubaliki.mtumishi.wamungu
@didacebigirimana7350
@didacebigirimana7350 2 жыл бұрын
Nadondokaga machozi nikisikia nyimbo zako zina nigusa saana,unanisaidia saana Kwendelea na njia ya kwenda kwa Baba mbinguni,nakuombea saana kaka 🇧🇮🇺🇸🇹🇿
@Jehovarohiband
@Jehovarohiband Жыл бұрын
Huyu Mtumshi anaimbia Mungu wakweli kabisa eee Mungu umuongoze asitoke kwenye mstari wako Kama wengine
@b.jmwalupii7684
@b.jmwalupii7684 Жыл бұрын
Hongera kwa huu wimbo mzuri
@Gwa-Kayaga
@Gwa-Kayaga Ай бұрын
Hapa comment za wakenya ni chache na sababu ni za kiroho,,, hongera sana mtu wa rohoni kaka🎉
@ReineDorDiamant
@ReineDorDiamant 2 жыл бұрын
Uko wapi moyo wakanisa😭😭😭😭😭😭😭😭😭yeye awona tusipo biona😭😭😭😭Mungu atusamehe🙏😭😭👆
@Jenipha-so9rk
@Jenipha-so9rk 3 ай бұрын
Ibada
@LuganoMwandoto-pf8zg
@LuganoMwandoto-pf8zg 9 ай бұрын
😀🔥Mungu akikupa kibari sehemu frani🔥 usinyamaze🔥🙌
@esperancenyabenda8386
@esperancenyabenda8386 2 жыл бұрын
Kwaweri wewe mumbaji tunakupenda afilica niwewe unagoza kwakuimba ukiwa rohoni tena kwanyekevu burundi tunapona kwanyimbo zako🤗🤗 🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮
@Gwa-Kayaga
@Gwa-Kayaga Ай бұрын
Hakika watu wa Burundi mko rohoni Sana,,,chuma hunoa chuma ndivyo mtu anoavyo uso wa rafiki yake,
@Gwa-Kayaga
@Gwa-Kayaga Ай бұрын
Ni maombi yangu kwenu, nchi yenu iwe na amani na utulivu Neema ya Mungu iwe juu ya anga la nchi yenu pia kama ilivyo Tanzania😢
@soniamuvyeyi
@soniamuvyeyi 2 жыл бұрын
Wawouuuuuh,unajuwa kweli ,Mungu akupanuliye mipaka.
@patranabwire4012
@patranabwire4012 2 жыл бұрын
I love this man of God Bless u🇺🇬🇺🇬
@TheKapungala
@TheKapungala 2 жыл бұрын
I just love how our Tanzanian brothers and sisters make music straight from the scriptures. More love form Nairobi!
@rogathesarwatt
@rogathesarwatt 2 жыл бұрын
All about Lugha Adhu ya Kiswahili
@paulwachenje861
@paulwachenje861 2 жыл бұрын
That's exactly what I was heading to post but you represented the likes of us well
@barakahiluka4905
@barakahiluka4905 2 жыл бұрын
Mungu akubaliki sana mtumishi👐
@danielnzali5609
@danielnzali5609 2 жыл бұрын
Mungu akutunze mtumishi....🔥🔥
@dollnjosy3210
@dollnjosy3210 2 жыл бұрын
🙏🙏❤️
@jacksonenock5231
@jacksonenock5231 2 жыл бұрын
Hakika huu wimbo Roho wa Mungu alikuongonza kuuandika barikiwa kwa injili safi ya wimbo.
@malifedhamachimu4882
@malifedhamachimu4882 2 жыл бұрын
Mungu aendelee kukutumia mtu wa Mungu yaani unaimba rohoni ,,,ujumbe umekamilika kabisa wokofu ni utakatifu siyo kuhubiliana miujiza tuu Nadhani wamesikia...
@glorymusa4869
@glorymusa4869 2 жыл бұрын
I'm blessed Mungu aendelee kukutumia jinsi apendavyo yeye mtumishi🙌💅🙌
@harunramadhan1652
@harunramadhan1652 Жыл бұрын
MUNGU mwema akujazi mtumishi wake
@egenmaster93
@egenmaster93 2 жыл бұрын
Neither a worshiper nor a praiser! Just a preacher!
@brigitafelix2421
@brigitafelix2421 2 жыл бұрын
Nimebarikiwa sana na ujumbe wa neno la Mungu kupitia wimbo huu hakika nimtukuza Mungu
@canciasnyabiondo7434
@canciasnyabiondo7434 4 ай бұрын
I just bumped into your songs,,, this one's is on another level
@rtlusungu
@rtlusungu 2 жыл бұрын
Sema Ambwene una madini sana.. Daaah, we endelea tu kuimba Kaka, sisi tunapona huku.. Songs straight from the throne of heaven.. Hiki kizazi kina bahati ya kuwa na mtu kama wewe.
@safindume5051
@safindume5051 2 жыл бұрын
Kabisa
@selestinekaale7545
@selestinekaale7545 2 жыл бұрын
Ni kweli kaka usemalo, Aisee! Halafu Tazama Hekima za BWANA, yeye kaka Ambwene anaona kawaida tu Aisee!😃😃
@willyke2251
@willyke2251 2 жыл бұрын
Very true
@gilbertgodfrey6376
@gilbertgodfrey6376 2 жыл бұрын
Kabisa huyu mwamba namkubali kinoma maana hamuigi mtu kuimba na anaimba kwa kumaanisha
@gilbertgodfrey6376
@gilbertgodfrey6376 2 жыл бұрын
Yaani waimbaji wa siku hizi naona wamebaki wamili Ambwene na mchungaji abiudi wengine wote wanarapu na wananiudhi sana maana wanatoka nnje ya maadili ya mungu
@veronicawilson4263
@veronicawilson4263 2 жыл бұрын
Hakika MUNGU azidi kukubariki nyimbo zako zinanibariki San nikiwa 🇮🇶
@trizasamuel8555
@trizasamuel8555 2 жыл бұрын
Umeupiga mwingi mtumishi umegusa kila Eneooo Mungu nisaidieeee
@mussafredy5165
@mussafredy5165 2 жыл бұрын
Man of God. Kyala akutule
@gracepetro5430
@gracepetro5430 2 жыл бұрын
Yaani MUNGU atusaidie Sana watu sikuhizi wanahukumiana,pasipo kujiuliza kuwa hata tunao hukumiana hatujakamilika,,watu tunajipendelea,wenyewe hasa mtu ukiwa na fedha ndo utapendwa balaa ,ukiwa huna utazalauliwa Sana ,,God bless you
@datanya_tz8181
@datanya_tz8181 Жыл бұрын
Mimi nahisi mungu alishusha waimbaji wa injili kwa ajili ya watu wavivu wa kusoma bibilia mungu alijua kuna viumbe vikisoma bibilia vinasinzia ndo akashusha waimbaji
@pascazianhigula1900
@pascazianhigula1900 2 жыл бұрын
Kwa neema ya Bwana hujawahi kukosea ,sifa na utukufu ni kwa Bwana nangoja official video ya UMENIPA HESHIMA 🔥🔥🔥
@exaverymakoye6026
@exaverymakoye6026 Жыл бұрын
Nimependesana hii nyimbo
@kizungutheophile1005
@kizungutheophile1005 Жыл бұрын
inatupasa tutembele musingi wa Yesu Kristo
Ambwene Mwasongwe - Nimeachilia (Official Music Video)
7:17
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 1 МЛН
Ambwene Mwasongwe - Unikumbuke (Official Music Video)
7:56
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 910 М.
Slow motion boy #shorts by Tsuriki Show
00:14
Tsuriki Show
Рет қаралды 9 МЛН
路飞太过分了,自己游泳。#海贼王#路飞
00:28
路飞与唐舞桐
Рет қаралды 35 МЛН
Inasikitisha: Kilichomkuta Ambwene Mwasongwe Unaweza Kutokwa Machozi
11:29
Mwabukusi Atoa Hotuba Nzito Baada ya Kuapishwa, 'Tuwe Wamoja'
19:11
Uso Wangu
9:52
Emmanuel Mgogo - Topic
Рет қаралды 80 М.
AMBWENE MWASONGWE - NITAAMBATANA (official music video)
7:48
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 393 М.
MISULI YA IMANI BY AMBWENE MWASONGWE (Official Music Video)
8:06
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 1,2 МЛН
OMBI LANGU BY AMBWENE MWASONGWE (OFFICIAL MUSIC VIDEO)
5:52
Ambwene Mwasongwe
Рет қаралды 4,1 МЛН
Ufunuo Choir  - Usisahau ( Live Performance )
9:33
UFUNUO CHOIR
Рет қаралды 4,9 МЛН
Serik Ibragimov ft IL'HAN - Жарығым (official video) 2024
3:08
Serik Ibragimov
Рет қаралды 201 М.
Жандос ҚАРЖАУБАЙ - Ауылымды сағындым (official video) 2024
4:25
Taxi
3:06
Sadraddin - Topic
Рет қаралды 226 М.
Aq Koilek
2:51
Algyt - Topic
Рет қаралды 141 М.
Stray Kids "Chk Chk Boom" M/V
3:26
JYP Entertainment
Рет қаралды 64 МЛН