Рет қаралды 149,404
AZAM TV YAWA YA KWANZA KULIFIKIA ZIWA NGOSI: Moja kati ya vivutio vikubwa vya utalii mkoani Mbeya ni Ziwa Ngosi. Hili ni ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika linalotokana na mlipuko wa Volacano. Miongoni mwa maajabu ya ziwa hili ni maji yake kubadilika rangi.
Ziwa hili linapatikana katika hifadhi ya misitu ya Poroto iliyoko wilayani Rugwe, takriban kilometa 30 kutoka Mbeya Mjini.
Azam TV kimekuwa ni chombo cha kwanza kufika katika ziwa hilo, ambapo kikosi chake kimechanja mbuga na kuupasua msitu huo hadi kulifikia Ziwa hilo na kukutana na wahifadhi wa Ziwa hilo katika Hifadhi asilia ya Milima Rungwe.
Wahifadhi hao wameeleza chanzo na asili ya jina la ziwa hilo. Wameeleza chimbuko na kuwataja watu waliolivumbua. Yaani simulizi kamili ya kutokea kwake iko hapa.
Pia hiki kama kivutio cha utalii kimelinufaisha vipi taifa hadi sasa?
Tazama Makala hii inayosimuliwa na Salim Mhando.