Рет қаралды 2,658
HYDROPONIC ni sayansi/sanaa ya kuotesha mimea kwa kutumia maji bila kuhusisha matumizi ya udongo kabisa, isipokuwa mimea inaoteshwa katika chombo maalum ‘tray” ambacho kipo katika hali ya usafi na kina matundu ya kiasi ili kusaidia maji yasituame wakati wa kumwagilizia pia virutubisho maalum (Hydroponic Nutrients) ili kuongeza uzito.Njia hii inazalisha malisho ya mifugo kwa gharama nafuu zaidi na kwa muda mfupi.
Uandaaji wa chakula aina ya hydroponics
Mimea inaoteshwa katika chombo maalum ‘tray” ambacho kipo katika hali ya usafi na kina matundu ya kiasi ili kusaidia maji yasituame wakati wa kumwagilizia. Katika utengenezaji wa chakula hiki, mbegu za nafaka kama vile Shairi, Ngano, Mchele, Mahindi, Uele, Ulezi na Mtama zinafaa. Ili kuotesha mbegu zako kwa utaratibu huu utahitaji vifaa vifuatavyo:
1. Tray ya plastiki au alminium yenye matundu ( umbo mstatili ni bora zaidi)
2. Sprayer (chupa ya kunyunyizia maji)
3. Mbegu za nafaka (chagua mbegu ambazo hazijatobolewa na wadudu)
4. Chombo cha kulowekea mbegu (Unaweza kutumia ndoo yeyote)
5. Chujio la plastiki ( Kama hauna unaweza kutumia kitambaa kisafi)
6. Virutubisho (nutrients): wengine hutumia buster za mazao (hakikisha haina madhara kwa mifugo).