No video

Kwa masikitiko Askofu Kilaini atoa homilia kumzika Padre Asterius/ "Niliona mwili wake nikashindwa"

  Рет қаралды 18,802

Radio Mbiu

Radio Mbiu

11 ай бұрын

Makuhani na wakristo wa Kanisa Katoliki wametakiwa kutafakari Fumbo la kifo na ufufuko wake Bwana wetu Yesu Kristo kwa matendo na maisha wanayoyaishi hapa duniani ili kuwa mfano wa kuigwa .
Askofu Method Kilaini, Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Bukoba ameyasema hayo Agosti 21wakati akiadhimisha Ibada ya Misa Takatifu ya kumuanga na kumuombea Marehemu Padre ASTERIUS MUTEGEKI aliyefariki kwa ajali ya pikipiki, ambaye alikuwa akifanya utume wake katika Parokia ya Ishozi Jimbo Katoliki la Bukoba, misa iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni -Rubya Jimbo Katoliki la Bukoba.
Askofu Kilaini amewataka Makuhani na wakristo kutafakari kwa kina kuhusiana na fumbo la kifo cha Yesu kristu na ufuko wake kwa kuonyesha uhalisia wa maisha yao kwa vitendo na kuitazama mienendo yao ili wawe mfano wa kuigwa huku wakitenda haki hata kama itawagharimu uhai wao ili kumwakilishwa yesu msulubiwa kwa kuachana na dhambi .
Hata hivyo amelitaka kanisa kushikamana kwa pamoja katika kipindi hiki kigumu kumuombea mpendwa wao Padre Asterius aliyefariki Ijumaa ,Agosti 13 2023 kwa ajali ya pikipiki ili Mungu mwenye Huruma ampokee mbinguni kwani bwana alitoa na ametwaa .
Akimuelezea Padre sterius Askofu Kilaini amesema kuwa marehemu Padre Asterius kote alipokwend katika maisha ya Seminari alikua anafanya vizuri na kijana ambaye aliundwa tangu akiwa mdogo na ambaye alikuwa ni mchapakazi, makini,mpenda watu, mwajibakaji,mwenye karama ya uongozi, mwenye furaha na ambaye alifanya kazi nzuri katika kanisa.
“Tunawashukuru wazazi kwa kumtoa kijana huyu na kutukabidhi kanisa awe wa kwetu na mwaka 2014 tukamchukua tukamlea na kumuunda ili aje afanye kazi ya Bwana. Tulimpitisha sehemu mbali mbali Kemondo, Ntungamo, Kipalapala Tabora na kote alipokwenda alifanya vizuri saa, sababu aliundwa vizuri tangu yupo mdogo’’ Alielezea Askofu Kilaini.
“Tarehe 25 January 2022 Baba Askofu Rwoma alimwekea mikono akawa Shemaji, ambayo ni hatua kubwa sana ukishaivuka ni vigumu sana kurudi nyuma, hapakuwa na wasiwasi sababu kijana alikua anapendeza kwa matendo yake. Na tarehe 2 July mwaka jana 2022 mimi mwenyewe nilimuwekea mikono akawa kuhani wa Bwana milele kwa mfano wa Melkisedeki umewekewa mikono, umeteuliwa umeitwa kwa sababu ulijitoa kwa Bwana” Kwahuzuni aliongeza Askofu Kilaini katika homilia yake
Aidha Askofu Kilaini amaemuelezea Marehemu Padre Asterius Mutegeki kwa kazi yake nzuri aliyoifanya katika kanisa, na usema wakati akiwa Shemasi alifanya kazi katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo akiwa ni mlezi wa vijana na wanafunzi wa Shule za Secondari (Chaplain), Baada ya kupadrishwa alipangiwa Utume katika Parokia ya Ngarama kusimamia Shule ya Msingi na Sekondari kwa lengo la kulea na kufanya kazi ya kitume katika Shule hiyo na baadaye kupangiwa Utume katika Shule ya Sekondari ya Ishozi kwa kusimamia katika Upande wa fedha, mali na uongozi na alisimamia vyema maendeleo.”
“Alishika wadhifa wa ukuhani kwa moyo wake wote, Tulimuweka pale Ihungo nyumba ya malezi pale kwaajili ya vijana wafanyakazi kwa shule za Sekondari na kwaajili ya vijana.
Askofu Kilaini alihitimisha kwa kusema kuwa Nilipofika mjini nilikuta mwili ulikuwa katika gari, nilipofunua na kumuona alikuwa ni Asterius yule yule anafanana kama amelala na tabasamu lake, nilijaribu kuongoza sala nikashindwa, nilikumbuka mengi sana nakumbuka wakati wa Jubilei yangu ya miaka 50 yeye ndiye alikuwa mshenga ambaye alikuwa karibu nami katika Vijilia, niliporusha ile picha Maaskofu wote walisikitika na kupiga simu kutoa pole na maaskofu wote wametuma ujumbe na kutoa pole sababu sio kitu cha kawaida” Alihitimisha Askofu Kilaini katika homilia yake.
Ikumbukwe kuwa Pade Asterius Mutegeki alizaliwa 28/12/1990 katika Kijiji cha Manyazi visiwa vya Bumbile vilivyopo Wilaya ya Muleba Jimboni Bukoba,Alibatizwa 23 December 1993 Parokia ya Bumbile na mbatizaji akiwa ni Padre Marceli Kaberwa ambaye ni Paroko msaidizi wa Parokia ya Mafumbo , Alipokea Sakramenti ya Kipaimara mwaka 1999 kutoka kwa Askofu Nestory Timanywa.
www.radiombiu.co.tz
#RmSautiYaFaraja

Пікірлер: 29
@rozkiwale912
@rozkiwale912 11 ай бұрын
Mungu amjalie pumziko la milele Amina .poleni sana kweli kabisa inauma sana jamani
@sudialihemed8656
@sudialihemed8656 11 ай бұрын
mtihani
@evanceruyumbu6347
@evanceruyumbu6347 11 ай бұрын
Apumzike kwa amani padre wetu.
@kaizilegjoseph46
@kaizilegjoseph46 9 ай бұрын
Pumzika kwa aman
@user-wy6ur1we3r
@user-wy6ur1we3r 11 ай бұрын
Ee Mwenyezi Mungu mpe pumziko la milele Padre Asterius Mutegeki. Amina.
@evodirudo4813
@evodirudo4813 11 ай бұрын
Raha ya Milele umpe Ee Bwana na mwanga wa Milele umwangazie Apumzike Kwa amani Amina, R.i.p
@abajenezasolange6811
@abajenezasolange6811 11 ай бұрын
Father RIP.
@winnieavit5985
@winnieavit5985 11 ай бұрын
😢😢😢 Apumzike kwa Amani 🕯️
@eliasmhagama4978
@eliasmhagama4978 11 ай бұрын
Rest in eternal peace Fr Asterius. BWANA YESU akupokee katika Ufalme wake huko Mbinguni
@AkwilinaMtafa-fu5de
@AkwilinaMtafa-fu5de 11 ай бұрын
Everything e mwenyezi mungu uiweke roho yake Mahali pema peponi
@starehe123
@starehe123 11 ай бұрын
Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani. Pole kwa kanisa zima.
@user-wo1gv1lf3n
@user-wo1gv1lf3n 11 ай бұрын
Raha ya milele umpe ee bwana apumzike Kwa amani. Pole sana Baba askofu
@frederickbaijukya4773
@frederickbaijukya4773 11 ай бұрын
Gone too soon. R I P Fr. Asterius.
@veronicaalfred235
@veronicaalfred235 11 ай бұрын
Pumzika kwa Amani Padri Esterius, MUNGU aipokee roho yako akurehem na kukusamehe makosa yako Amina, yote haya ni kwa mapenzi yake yeye
@RugemaliraRenatus-rf6yv
@RugemaliraRenatus-rf6yv 11 ай бұрын
Apumzike kwa amani mbinguni,Amina
@gilbertkalanda9354
@gilbertkalanda9354 11 ай бұрын
So young , R.I.P Fr. Asterius
@muajiribrahimuAllyMwombeki
@muajiribrahimuAllyMwombeki 11 ай бұрын
pumzika kwa amani
@rwekazamugasha6448
@rwekazamugasha6448 11 ай бұрын
R.I.P Padri
@maryrubunga6504
@maryrubunga6504 11 ай бұрын
Pumzika kwa Amani.Raha ya milele ampe we bwana Na mwanga Wa milele umwangazie
@user-gn4fu8dv6h
@user-gn4fu8dv6h 5 ай бұрын
By calling God a liar and saying that he withhold good form his subjects, SATAN questioned Jehovah s, right to rule Genesis 3:2-5,, Jehovah will use his Son, the Rules of the Messanci kingdom, to end all human suffering and death,undo it's effects.1john 3:8 ❤❤😮
@user-xo4gl3we1t
@user-xo4gl3we1t 11 ай бұрын
ee Mungu mpokee mwanao Mpendwa Asterius mutegeki Umulaze mahali pema. jamani Kwa kweli Nimeumia sana Ameacha pengo kaka yangu
@JudithMtegeki-nv8db
@JudithMtegeki-nv8db 11 ай бұрын
🙏
@jenyyusuph4973
@jenyyusuph4973 11 ай бұрын
Alikua anaumwa😢😢?
@MiriamAbdallah
@MiriamAbdallah 11 ай бұрын
Raha ya milele umpe ee BWANA na MWANGA wa milele umwangazie, poleni wazazi, kanisa na waimini wote
@user-hb1iw9uj3x
@user-hb1iw9uj3x 11 ай бұрын
Ni njia ya kila nafsi, eee muumba tuepushe na moto wa milele
@user-iu3pt6jq9i
@user-iu3pt6jq9i 9 ай бұрын
Baba pumzika kwa amani ww ni kuhani hata milele tutakukumbuka kwa sala
@milley7185
@milley7185 11 ай бұрын
mmemtafunaaa
@verdianabanabi2205
@verdianabanabi2205 11 ай бұрын
Kivipi?
@victoriarwerengera4831
@victoriarwerengera4831 11 ай бұрын
Eleza kinagaubaga
Советы на всё лето 4 @postworkllc
00:23
История одного вокалиста
Рет қаралды 4,7 МЛН
Amazing weight loss transformation !! 😱😱
00:24
Tibo InShape
Рет қаралды 67 МЛН
ASKOFU LAGWEN AWASILISHA ZAWADI ZA WAKATOLIKI JIMBO LA MBULU KWA RAIS SAMIA
11:02
KANISA KATOLIKI TANZANIA TEC
Рет қаралды 7 М.
MEDIA VATICAN ILIVYORIPOTI A-Z MSIMAMO WA MAASKOFU TEC KUHUSU UWEKEZAJI BANDARINI
14:04
KANISA KATOLIKI TANZANIA TEC
Рет қаралды 109 М.