Makala fupi ya Historia ya Padre Joseph Babu- Muasisi wa Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro

  Рет қаралды 8,322

Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro

Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro

Жыл бұрын

Ilipofika mwaka 1972, kwa Uweza wa Roho Mtakatifu, Jimbo la Arusha lilifanya Maamuzi mawili ya kihistoria na yenye Utukufu wa Mungu. Uamuzi wa kwanza, aliyekuwa Mkuu wa Jimbo Katoliki Arusha, Mhashamu Baba Askofu Denis Durning, alitoa kibali cha kuanzishwa kwa Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro. Pili, Uongozi wa Jimbo hili lililotajwa ulimteua Padre Joseph Babu kuwa Paroko wa kwanza na Mwanzilishi wa Parokia hiyo mpya ya Roho Mtakatifu Ngarenaro. Matunda ya Mbegu bora iliyopandwa na Padre Babu, ndani ya miaka 50 ya uhai wa Parokia hii ya Roho Mt. Ngarenaro yamemuenzi Yesu Kristo kwa huduma za Kiroho, afya na Elimu, sio tu kwa waumini pekee, bali pia kwa jamii nzima ya Tanzania. Utukufu huu uliopitia mikono ya Padre Babu, umeipa heshima kubwa Parokia hii, Jimbo kuu Katoliki Arusha na Taifa letu kwa ujumla.
Ni katika kuzingatia yote haya, kwa kumuenzi Padre Joseph Babu, Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro ikishirikiana na Jimbo Kuu Katoliki Arusha, wameamua kuweka tarehe 05 Mwezi wa Pili kila mwaka kuwa siku maalumu ya kumbukumbu ya Padre Babu itakayojulikana kwa jina la Siku ya Padre Joseph Babu ( Father Babu Day). Lengo kuu la siku hii ni kuenzi Utume wa Padre Joseph Babu na Mchango mkubwa alioufanya kwenye Parokia ya Roho mtakatifu Ngarenaro pamoja na Jimbo Kuu Katoliki Arusha kwa ujumla.
Mapadre, Kamati tendaji na waamini wote wa Parokia hii wameamua pia kuandaa Makala hii yenye kuakisi kazi na majitoleo ya Padre Joseph Babu ambaye ndiye mwasisi wa Parokia yetu. Ni ukweli usiopingika kuwa Maisha ya Padre Joseph Babu yaligusa, yanaendelea kugusa na yataendelea kugusa kila moja wetu kwa namna moja au nyingine; lakini pia kila mmoja wetu anafahamu jina la Padre Joseph Babu (Father Babu) ni watu wachache, hasa hasa vijana ambao hawafahamu kwa undani Padre Babu hususan Utume na mchango wake kwa Kanisa na jamii yetu kwa ujumla.
Ni kwa mantiki hiyo Parokia yetu imeamua kuandaa Makala hii fupi ili kubainisha historia ya Parokia hii pamoja na mchango wa kiimani, elimu na afya uliofanywa na Padre Joseph Babu. Ni wajibu wa kila mwanaparokia/Mwaamini kukikumbusha kila kizazi historia yake.
Mapadre, Kamati tendaji na Waamini wote wa Parokia hii wanafarijika sana kuandaa makala hii ili vijana na Wamini wetu wote waweze kuona na kujifunza Maisha na Karama ambazo Mungu alimjalia Padre Joseph Babu.
Sherehe ya kumbukumbu inayotarajiwa kufanyika tarehe 05 mwezi wa pili kila mwaka itafungua ukurasa mpya wa matukio mengine muhimu ambayo hayajaweza kuingia katka makala hii, pia makala hii imebeba mwendelezo wa matukio yajayo ili kuendeleza historia ya Parokia yetu pamoja na Jimbo Kuu Katoliki Arusha kwa kizazi kijacho.

Пікірлер
Nastya and SeanDoesMagic
00:16
Nastya
Рет қаралды 44 МЛН
Mom's Unique Approach to Teaching Kids Hygiene #shorts
00:16
Fabiosa Stories
Рет қаралды 39 МЛН
CHOCKY MILK.. 🤣 #shorts
00:20
Savage Vlogs
Рет қаралды 18 МЛН
Mama vs Son vs Daddy 😭🤣
00:13
DADDYSON SHOW
Рет қаралды 51 МЛН
MAKALA FUPI YA HISTORIA YA SHIRIKA LA MASISTA WA MT AGNES KATIKA NYUMBA YA IMILIWAHA NJOMBE
33:16
CV YA LUHAGA MPINA WASIFU NA HISTORIA YAKE
13:24
Klik Hapa TV
Рет қаралды 40 М.
Nastya and SeanDoesMagic
00:16
Nastya
Рет қаралды 44 МЛН