Рет қаралды 827
Waamini wametakiwa kuwa wamojaa kwa kuzungumza lugha ya upendo na amani na wanandoa kuishi fadhili za kusameheana na kuvumiliana katika maisha ya kila siku.
Wito huo umetolewa na Padre Solomon Bandiho, Paroko wa Parokia ya Mt. Augustino wa Hippo- Buyango Jimbo Katoliki la Bukoba, wakati wa homilia yake katika adhimisho la misa takatifu ya Sherehe ya Pentekoste, misa inayoambatana na kutoa Sakramenti takatifu ya ndoa kwa jozi 101 Parokiani hapo.
Katika homilia yake Padre Bandiho amesema kuwa, Kazi ya Mungu Roho Mtakatifu ni kuunganisha watu, ambaye anawafanya wanadamu kuongea lugha moja iliyojaa amani na upendo na kuwasihi waamini kuacha tabia ya ubinafsi badala yake wajazwe na nguvu ya Roho Mtakatifu na kusahau ya zamani na kuanza maisha ya matumaini, maelewano bila kuwepo maneno ya kufarakana.
Aidha Padre Bandiho amewataka wanandoa kuishi fadhili za kusameheana na kuvumilia katika maisha ya kila siku na kamwe wasikubali kumaliza siku bila kusameheana katika familia itakuwa uwanja na mlipuko wa ugomvi.
Padre Bndiho alihitimisha homilia yake kwa kuwataka mababa wa familia kuwa na upendo katika familia zao na kupatikana katika familia ili kujenga na kudumisha mawasiliano hai katika familia na kuacha tabia ya kurudi nyumbani kwa kuchelewa kwa kisingizio cha kutafuta.
www.radiombiu.co.tz
#RmSautiYaFaraja