Рет қаралды 13
Timu Ya Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania-JWTZ Lugalo Golf Imeibuka Kinara Wa Mashindano Ya Allince One Morogoro Open 2024 Yaliyofanyika Mjini Kasoro Bahari Mkoan Morogoro.
Akizungumza Mara Baada Ya Kumalizika Kwa Shindano Hilo Meneja Wa Klabu Ya Lugalo Kanali David Mziray Amesema Ni Walijipanga kushinda na sio Kushiriki ndio maana wameibuka na ushindi kwa kila kategoli mashindano na ameahidi kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mashindano Yanayokuja.
Kwaupande wake Mshindi Wa Jumla Enoshi Wanyeche Kutoka Klabu ya Lugalo Amesema Licha Ya uwepo wa ushindani Mkubwa Amepambana kuipa ushindi klabu ya lugalo kwa kuonesha uwezo mkubwa siku zote za mashindano Hayo.
Naye Salum Dilunga Mchezaji Wa Kulipwa Kutoka Lugalo Gofu Amesema Haikuwa Raisi kwakuwa ameshindana na wachezaji wanaojua mchezo Huo na sheria zake.
Insert: Salum Dilunga(Mchezaji Wa Kulipwa)
Mchezaji Vicky Elias Wa Lugalo Gofu Ameonesha Uwezo Mkubwa Wa Mchezo wa Gofu Kwa Kufanya Vizuri Kwenye Shindano Hilo.
Wachezaji wengine Walioshinda Michael Masawe Wa Lugalo akishika nafasi Ya Pili,Julius Mwinzani Wa Dar Gymkhana Akishika nafasi Ya Tatu,kwa upande wa wachezaji Wa Kulipwa Salum Dillunga Wa Lugalo akishika nafasi Ya kwanza,Abdalla Yusuph akishika nafasi ya pili na kwa wanawake Vicky Elias wa Lugalo akishika nafasi Ya Kwanza Akifatiwa na Loveness Frank wa killi Golf nafasi Ya pili kwenye shindano Hilo.